PENDA KUKAA KATIKA USIKIVU.

Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu atukuzwe rafiki.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ninayekuletea Neno la MUNGU siku ya leo naitwa Mwl Peter Mabula.
Leo tunajifunza  umuhimu wa kipekee wa kukaa katika Usikivu wa Ki MUNGU.

"Usikivu ni Nini?"
Usikivu ni tabia ya uelekevu

✓✓Usikivu kwa MUNGU ni hali ya kufanya kama ulivyoamriwa kwenye hiyo Sauti ya MUNGU uliyoisikia.

Ndugu, penda sana kukaa katika Usikivu maana ndani ya Usikivu Kuna Majibu Yako.

✓✓Usikivu ninaouzungumzia ni Usikivu wa kumsikia   MUNGU wa Mbinguni anaposema kupitia Neno lake, ndani ya Usikivu huo Kuna Majibu Yako hakika.
Waisraeli waliwahi kuambiwa na MUNGU kwamba wakiwa wasikivu na watii watakuwa watu wa kitofauti Duniani na ndivyo ilivyokuwa kila wakati walipozingatia Usikivu.

Kutoka 19:5 "Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,"

✓✓Usikivu ninaouzungumzia Mimi ni Usikivu wa kumsikiliza ROHO MTAKATIFU  na kufuata anachokitaka yeye.

Zekaria 4:6" Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi."

✓Ni kwa Roho wa MUNGU utashinda

✓ni kwa Roho wa MUNGU mambo yako yakataa sawa.

✓Ni kwa Roho wa MUNGU hakuna wakala wa shetani atakayekuweza.

✓✓ Usikivu ninaouzungumzia Mimi ni kuwa makini na kuzingatia Sauti ya Bwana YESU KRISTO inayozungumza na Wewe.

Mwanzo 17:1" Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni MUNGU Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu."

Ibrahimu alipoizingatia sauti ya MUNGU akawa Mtu wa tofauti na  yote yalikuwa yameshindikana kwenye Maisha yake yakaanza kuwezekana, mfano ni kupata Uzao na mali nyingi.

Ndugu unajua Bwana YESU KRISTO anaweza akasema na Wewe kwa namna nyingi sana, ukizingatia umefanikiwa maana kupata baraka zako unazozihitaji kumeambatanishwa na wito anaokupa yeye Bwana YESU KRISTO.

Bwana YESU KRISTO anaweza akasema "Nitumikie" zingatia sana ndugu.

MUNGU anaweza akasema "Nitolee Sadaka" zingatia maana utii huo unaweza ukapelekea milango Yako ya Uzao au huduma au uchumi au kazi au Ndoa n.k, hiyo milango ikafunguka na asiwepo wa kuifunga tena.

Ufunuo  3:8 "Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu."

ROHO MTAKATIFU anaweza akasema "Acha dhambi " hiyo ni kwa faida Yako zingatia sana.

ROHO MTAKATIFU anaweza akasema "Usiende" zingatia sana maana ukienda utapata hasara na usipoenda kama alivyokuambia utapata faida.

ROHO MTAKATIFU anaweza akasema "Usishirikiane nao" ni watu wema kwako na unawaona ni watu sahihi au ni Mtu sahihi lakini kama MUNGU akikuambia kwamba Usishirikiane nao zingatia sana maana hiyo ni kwa faida Yako.

MUNGU anaweza akasema"Nenda" zingatia maana utapata faida.

Usipokuwa msikivu na mzingatiaji wa kila MUNGU anakuambia unaweza ukapishana na kusudi la MUNGU kwako na unaweza ukawa Mtu wa kupata hasara kila mara au majanga kila mara.

Rafiki mpendwa nakusihi katika Jina la Bwana wetu YESU KRISTO hakikisha kuanzia leo unakuwa msikivu kwa MUNGU.
Jitahidi kujua kile Bwana YESU KRISTO anakusemesha kupitia mahubiri, Neno Mtandaoni au Kanisani n.k
MUNGU akusaidie katika hili.
Pia kama hujampokea YESU KRISTO kuwa Mwokozi wako nafasi hiyo unayo Sasa, nakusihi sana Mpokee Leo awe Bwana na Mwokozi wako, jiunge na Kanisa la kiroho wanaomhubiri YESU KRISTO huko uliko na utafanya vyema sana 
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni.
+255714252292
Ubarikiwe 

Comments