Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Katika safari ya Maisha wakati mwingine Kuna kupitia vipindi vigumu, kuvunjwa Moyo, kusalitiwa, kukatishwa tamaa, kuumizwa, kuonewa, kushushwa na kutengwa n.k lakini Wewe mtumaini Bwana YESU KRISTO daima katika MUNGU maana Wamtumainio MUNGU msaada wa Mbinguni utawazunguka.Zaburi 32:10" ......... Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka."
✓✓Amtumainie MUNGU wa Mbinguni atafanikiwa.
Mithali 28:25 "........... Bali amtumainiye BWANA atawandishwa."
✓✓Ukimtumaini MUNGU utakaa salama dhidi ya maadui wote wa kiroho na wa kimwili.
Mithali 29:25 "Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama."
✓✓Ndugu yangu, katika Hali zote mtumaini MUNGU katika KRISTO YESU.
Katika mazingira yote magumu ya Afya, uchumi, wazao wako , ushindi n.k nakusihi katika Jina la YESU KRISTO chagua kumtumaini MUNGU Baba wa Mbinguni.
Maombolezo 3:24" BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye."
✓✓Ndugu Mtumaini MUNGU maana anaweza kukupa vyote unavyohitaji.
1 Timotheo 6:17" ............. bali wamtumaini MUNGU atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha."
✓✓Mtumaini MUNGU kwa ajili ya
Watoto wako maana atatenda jambo jipya la kuleta furaha kwako.
✓✓Mtumaini Bwana YESU kwa ajili ya uchumi wako.
✓✓Mtumaini MUNGU kwa ajili ya Afya Yako maana Magonjwa yatakaa mbali na Wewe kwa Jina la YESU KRISTO.
✓✓Mtumaini MUNGU wa Mbinguni kwa ajili ya kibali chako katika maeneo yote.
Siku Moja nilipata Msukumo wa kumueleza rafiki yangu mmoja na Leo ujumbe ule ule imenilazimu kukulelea na Wewe rafiki yangu unaeusoma Sasa ujumbe huu
MUNGU wa Mbinguni sana na akutendee mema sawasawa niliyoyaandika katika ujumbe huu maana nimeyaombea na MUNGU wa Mbinguni akutendee mema unayoyahitaji kwake.
MUNGU wa Mbinguni akupe kumaliza mwaka kwa ushuhuda na ushindi na akupe kuanza mwaka Mwingine ambao Njia yake ameichora yeye kwa ajili Yako ili utembee kwenye njia hiyo mwaka mzima.
Bwana YESU KRISTO awe pamoja na roho Yako.
Asante rafiki yangu kwa kujifunza Neno hili la MUNGU leo.
Kabla sijahitimisha leo ninalo Neno la mwisho kwa ajili yako.
Je umeokoka?
Kama umeokoka endelea na Wokovu wa Bwana YESU KRISTO hadi mwisho wa maisha yako.
Na wewe ambaye hujaokoka nakuomba okoka leo maana tunaishi siku za Mwisho.
Ni YESU tu ndio anayeweza kuliandiika jina lako kwenye kitabu cha uzima hata upate Uzima wa milele, nakuomba sana mpokee YESU KRISTO leo kwa ajili ya Wokovu.
Huko huko uliko tafuta Kanisa la kiroho wanaohubiri Wokovu Wa KRISTO ukamweleze Mchungaji atakuongoza sala ya toba na utakuwa umeokoka.
Fanya hivyo kwa faida ya roho yako milele
MUNGU akubariki.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU.
+255714252292(Sadaka ya kupeleka Injili, Maombi na ushauri)
Ubarikiwe sana
Comments