![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni |
Bwana YESU KRISTO asifiwe.
Unao maadui katika ulimwengu wa roho na inawezekana pia unao maadui wengi katika ulimwengu wa mwili.
Maadui zako ni pamoja na majini wote, mizimu, miungu na kila maroho ya kuzimu.
Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Adui zako wengine ni wanadamu wanaotumika kishetani dhidi yako, hawa wanaweza kuwa wachawi, waganga wa kienyeji, washirikina, wasihiri, watu wa kawaida wanaokuchukia na kila wakala wa shetani aliye mwanadamu.
Kama si MUNGU kuwazuia kukudhuru hakika wangekumeza hai.
Zaburi 124:2-3 " Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Wanadamu walipotushambulia. Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu"
Hivyo unahitaji pia kumwambia MUNGU kwa mwaka huu wote aendelee kuwazuia adui zako ili wasikudhuru.
●Inawezekana wapo maadui zako wanawinda uhai wako au ndoa yako au uchumi wako au uzao wako au wanawinda mwili wako.
Unahitaji sana kuomba kwa MUNGU ili awazuie hao adui zako kukudhuru.
Ayubu 33:18 "Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga."
●Inawezekana nguvu za giza wanapanga kukuondoa duniani mwaka huu, ndugu unamhitaji sana YESU KRISTO ili upone na uwe salama.
●Inawezekana wanawinda uchumi, inawezekana wanapanga kukuletea magonjwa n.k
Ashukuriwe MUNGU Baba wa mbinguni maana anaweza kuwazuia adui zako mwaka huu mzima.
Ezekieli 28:26 "Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya
mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote,
wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu
wao."
Ndugu omba na MUNGU atatenda sawasawa na maombi yako.
Ukiomba MUNGU awazuie wachawi na majini kukudhuru hakika itakuwa hivyo.
Ndugu omba katika jina la YESU KRISTO na utamuona MUNGU anayetenda.
Ishi pia maisha matakatifu maana maisha ya dhambi yatamfanya MUNGU asizuie mabaya kwako.
Amosi 1:11 "Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararua-rarua daima, akaishika ghadhabu yake milele;"
Nini ufanye katika Maombi?
1. Omba Maombi ya kutubu ili uwe safi kiroho na kwa njia hiyo utamruhusu MUNGU kukujibu maombi yako yanayofuata baada ya toba.
Yoshua 3:5 "Yoshua akawaambia watu, Jitakaseni; maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu."
2. Omba MUNGU akuokoe kwenye mitego ya maadui zako wanaokuwinda mwaka huu.
Zaburi 91:2-3 " Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo."
3. Omba MUNGU awazuie mawakala wa shetani kukufanya lolote.
Ezekieli 28:26 "Nao watakaa humo salama; naam, watajenga nyumba, na kupanda mashamba ya mizabibu, na kukaa salama; nitakapokuwa nimetekeleza hukumu zangu juu ya watu wote, wanaowatenda mambo ya jeuri pande zote; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu
wao."
4. Omba MUNGU apigane nao hao wanaotoka kuzimu wanaopanga kupigana na wewe mwaka huu.
Zaburi 35:1 "Ee BWANA, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami."
5. Mshukuru MUNGU ukiamini amekushindia na amewazuia maadui zako wote kukudhuru mwaka huu.
Zaburi 7:17 "Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu."
Ndugu omba na utamuona MUNGU.
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kueleea naamini ameelewa .
Hapa chini ni MAOMBI YA KUOMBA MUNGU AWAZUIE ADUI ZAKO KUKUDHURU MWAKA HUU.
Maombi haya ni kwa ajili ya mtu ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba.
Kwa waombaji wazoe
fu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea.
MAOMBI YA KUOMBA MUNGU AWAZUIE ADUI ZAKO KUKUDHURU MWAKA HUU.
Eee MUNGU Baba wa Mbinguni, ninakushukuru kwa neema ya ulinzi ulionipa mimi na familia yangu hadi wakati.
Pokea sifa, heshima na utukufu wote Eee MUNGU Baba uliyeniumba na ukanilinda hadi leo.
Ninaomba msamaha pia mbele zako MUNGU wangu, naomba unisamehe dhambi zangu zote na maovu yangu yote na makosa yangu yote pia.
Ninaomba unisamehe kwa neno lolote nililokosea mbele zako.
Naomba unisamehe kwa kila tendo baya nililolifanya.
Bwana YESU KRISTO naomba unipe neema niishi maisha matakatifu siku zote za maisha yangu.
Neno lako MUNGU Baba linasema katika Zaburi 91:2-3 kwamba " Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, MUNGU wangu nitakayemtumaini. Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo."
Hivyo ninaomba MUNGU Baba ukaniokoe dhidi ya kila mitego ya kichawi na kiganga mwaka huu wote.
Nakuomba MUNGU Baba ukaniokoe dhidi ya kila mitego ya majini na mizimu mwaka huu wote.
Eee Bwana YESU KRISTO nakuomba uniokoe dhidi ya kila mitego ya watu wabaya waliyonipangia mimi mwaka huu, mitego hiyo ivunjike kwa jina la YESU KRISTO.
Niokoe Bwana YESU dhidi ya kila mitego ya madhabahu za giza iliyopangwa kwa ajili yangu au uzao wangu au familia yangu mwaka huu.
Kila mitego ya watu wasionipenda, hiyo mitego ya kipepo naivunja kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mitego ya makuhani wa giza, hiyo mitego ya kipepo naivunja kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mitego ya wachawi na waganga wa kienyeji, hiyo mitego ya kipepo naivunja kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mitego ya mwanaume au mwanamke, hiyo mitego ya kipepo naivunja kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa kishetani uliopangwa kuhusu mimi mwaka huu, huo mtego wa kipepo nauvunja kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mtego wa kishetani uliopangwa asubuhi au mchana jioni au usiku katika siku yeyote ya mwaka huu, huo mtego wa kipepo nauvunja kwa jina la YESU KRISTO.
Eee MUNGU Baba ninaomba uwazuie kila maroho wa kuzimu wasifanikiwe lolote kwangu mwaka huu.
Eee MUNGU Baba ninaomba uwazuie majini na mizimu wote, uwazuie kunidhuru au kudhuru familia yangu au ndoa yangu au biashara yangu.
Ninaomba Baba MUNGU upigane nao wote waliopanga lolote baya kwa ajili yangu, pigana nao BWANA kama Neno lako linavyosema katika Zaburi 35:1.
Kila mchawi na uchawi wake hatafanikiwa kwangu mwaka huu, katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu.
Kila uganga na ushirikina hautafanikiwa kwangu mwaka huu, katika jina la YESU KRISTO Mwokozi.
Kila jini au mzimu au mwanadamu mbaya, wote hawa hawatafanikiwa kwangu mwaka huu katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Nakushukuru MUNGU Baba maana utawazuia wanadamu, mawakala wa shetani na nguvu za giza, utawazuia mwaka huu kunidhuru.
Nikae salama mwaka mzima katika jina la YESU KRISTO.
Familia yangu na ndoa yangu itakaa salama mwaka huu katika jina la YESU KRISTO.
Uchumi wangu na kazi yangu vitakaa salama mwaka huu katika jina la YESU KRISTO.
Wazazi wangu na watoto wangu wote wakataa salama mwaka huu katika jina la YESU KRISTO.
Mwili wangu na afya yangu na miili ya watu wa nyumba yangu wote watakaa salama mwaka huu katika jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru MUNGU Baba maana umetenda.
Neno lako linasema katika Zaburi 7:17 kwamba "Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu."
Hivyo ninakushuru sana MUNGU Baba wa Mbinguni.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
Amen, amen, Ameeeeeeeeeeeeen.
Hakika ndugu umeshinda.
Omba na utamuona MUNGU.
By Peter Mabula
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Whatsapp)
Comments