MAOMBI YANGU KWA AJILI YA MARAFIKI ZANGU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
MUNGU akubariki sana kwa kuendelea kujifunza Neno la MUNGU kupitia masomo yangu mbalimbali ambayo ROHO MTAKATIFU amenipa neema ya kuyaleta kila mara kwa miaka mingi Sasa.
Ni maombi yangu mbele za MUNGU kwa ajili yako rafiki yangu.

1. Nguvu za ROHO MTAKATIFU ziambatane na wewe.

Warumi 15:13 "Basi MUNGU wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za ROHO MTAKATIFU."

2. MUNGU apigane na adui zako kwa ajili yako.

Isaya 41:11-13 " Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.  Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako. Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia."

3. Malaika wa MUNGU wakuhudumie ili uwe na ushinde timilifu.

Waebrania 1:14 "Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?"

4. ROHO MTAKATIFU akufunulie mafumbo yote.

1 Wakorintho 2:10 "Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU."

5. Bwana YESU KRISTO akuokoe dhidi ya kila hila za shetani.

Yohana 10:28-30 " Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja."

6. MUNGU Baba akufunike adui zako wasikuone.

Zaburi 17:6-9 "Ee MUNGU, nimekuita kwa maana utaitika, Utege sikio lako ulisikie neno langu. Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume Uwaokoe nao wanaowaondokea.
 Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako; Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho yangu wanaonizunguka."

7. Upate mahitaji yako katika jina la YESU KRISTO na anga lako lifunguke.

3 Yohana 1:2 "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo."

8.  MUNGU aligane nao wanaokutesa na  mipaka ya kipepo iliyokuzuia iondolewe.

Zaburi 143:12 "Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.''

9. Ndoa yako, afya yako, uchumi wako, uzao wako na kibali chako vyote hivyo viwe salama na viwe baraka kwako kutoka kwa MUNGU.

Zaburi 121:5 "BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume."

10. MUNGU Baba akupe miaka mingi ya kuishi duniani yenye furaha, baraka na amani.

Mithali 3:16-17 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto. Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

Ndugu yangu hakikisha tu umeokoka.
Hakikisha Bwana YESU KRISTO ni Mwokozi wako binafsi maana umeshampokea kama Bwana na Mwokozi wako.
Hakikisha tu unaishi maisha matakatifu ya Wokovu siku zote.
Uwe na moyo wa ibada na maombi katika jina la YESU KRISTO.
Mwabudu MUNGU katika Roho na kweli.
MUNGU akukumbuke akulinde akupe mahitaji yako na akupe maisha marefu ya kuishi yenye amani na furaha na baraka.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO.
+255714252292
Ubarikiwe sana 

Comments