Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Haya ni maono niliyopewa tarehe 16 April 2016 nikayaandika katika daftari zangu za kuandalia masomo lakini daftari niliyoandikia maono haya ikapotea kabla ujumbe husika sijauandika katika computer ili kuwahubiria watu kwa njia ya mitandao ya kijamii, nami nikasahau. Lakini kwa neema ya MUNGU tarehe 1 May 2020 daftari niliyoandika maono haya nikaipata katika mazingira ya ajabu sana, baadae nikaliandika somo hili ambalo leo nakuletea maono husika kama nilivyokuwa nimeandika siku nafunuliwa.
Maono.
Tarehe 16 April 2016 nilipata maono yaliyonifanya nitafakari sana maono hayo.
Nilisikia sauti ikisema "Mwanadamu nimemuumba kwa mfano wangu Mimi, lakini Mwanadamu amenisahau kama Mimi ndio Muumba wake"
Baada ya kuisikia sauti hiyo ikiyozungumza nami nikaanza kuona maono, nilianza kwa kumuona binti mmoja akiwa amevaa tu nguo ya ndani(Wanaita taiti) nyeusi na juu kavaa blausi nyeupe akitembea kwa madaha kwenda kufanya dhambi.
Baadae kidogo nikamuona Mwanaume mmoja akiwa uchi akizozana na binti mmoja aliyebeba begi mgongoni.
Mwanaume yule nilipomuona tu niliambiwa "ana ukimwi" ila binti hakujua kama mwanaume yule ana ukimwi. Yule mwanaume nilimuona akimlazimisha binti kufanya ngono.
Baada ya kuona maono hayo ile sauti ya kwanza ikarudia tena kusema "Mwanadamu nimemuumba kwa mfano wangu Mimi lakini Mwanadamu amenisahau kama Mimi ni Muumba wake"
Maono Yale yakaishia hapo.
Katika maono Yale hasira ya MUNGU ilikuwa kali dhidi ya Mwanadamu mtenda dhambi.
✓✓Ndugu zangu, Neno hili naomba lituamshe kutoka katika dhambi ili sasa kila mmoja ampokee YESU KRISTO kama Mwokozi wake na aanze kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.
✓✓Ni kweli kabisa Mwanadamu ameumbwa kwa Mfano wa MUNGU.
Mwanzo 1:27" MUNGU akaumba mtu kwa mfano wake, KWA MFANO wa MUNGU alimwumba, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA."
Sisi wanadamu tumeumbwa kwa Mfano wa MUNGU kwa sababu tumepewa akili kuliko ndege, wadudu na wanyama viumbe.
Sisi wanadamu ni kwa Mfano wa MUNGU kwa sababu ni sisi tu wanadamu ambao MUNGU ametuumba tukiwa na roho na nafsi.
MUNGU akupe neema ndugu ya kuishi maisha matakatifu katika Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.
✓✓Mbingu zishuhudie kuanzia leo kwamba wewe unaacha dhambi na maovu ili sasa uambatane na Bwana YESU KRISTO aliye Mwokozi.
Mathayo 3:2 "Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."
Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;"
MUNGU anataka ndugu yangu ubadilike matendo yako kutoka mtenda mabaya na uanze kuishi tu katika matendo mema yanayoagizwa na Biblia. Badilika matendo ndugu yangu kwa kumrudia MUNGU aliyekuumba.
✓✓✓MUNGU ameamuru uzima wa milele katika Mwanaye wa pekee YESU KRISTO, hivyo ndugu hakikisha YESU KRISTO ni Bwana na Mwokozi wako binafsi.
Yohana 3:16-19 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu."
MUNGU akubariki kama umeelewa.
Ndugu zangu, huo ndio ulikuwa ujumbe wa tarehe 16 April 2016 ambao Mimi Peter Mabula nilikuja kuupata ten tarehe 1 May 2020.
Ni miaka 4 ilipita lakini MUNGU alinipa neema tena ya kuusema ujumbe ule.
Namshukuru sana MUNGU Baba kwa kusema nami na Namshukuru Sana yeye maana aliuhifadhi katika mazingira ambayo sikutarajia kabisa hadi kupitia mtoto mdogo aliyeniletea daftari hii, na nikabaki namshangaa MUNGU.
✓✓Ndugu yangu, Mimi naamini ujumbe wa MUNGU wa Mbinguni nimeufikisha mahali sahihi, ukiweza hata usambaze kwa marafiki zako na MUNGU aliowakusudia kuwajulisha atakuwa amewajulisha.
Ndugu kama hujaokoka nakuomba okoka leo.
Wewe uliyeokoka tayari nakuomba ongeza utakatifu.
MUNGU akubariki Sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU.
+255714252292( Whatsapp)
Comments