NJIA 4 RAHISI ZA KUPATA BARAKA ZA MUNGU.

 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu atukuzwe rafiki.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ninayekuletea Neno la MUNGU siku ya leo naitwa Mwl Peter Mabula.
Leo tunajifunza njia 4 Rahisi za kupata baraka za MUNGU.

1. Kuomba kwa MUNGU ili akubariki baraka husika.

Zaburi 2:8 "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako."

✓✓Njia hii inakuhitaji uwe umempokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako,  unaishi Maisha matakatifu katika yeye na unafuata kanuni zote za kiroho za utoaji na kusikiliza sauti ya MUNGU Kisha uombe MUNGU akubariki na atakubariki.
Zingatia kanuni za ki MUNGU katika KRISTO YESU Kisha omba utabarikiwa.

✓✓Ndugu, chagua kumwita YESU KRISTO kwa Maombi na utabarikiwa.

2. Kutoka familia iliyobarikiwa.

Kumbu 5:29 "Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, WAPATE KUFANIKIWA WAO NA WATOTO WAO MILELE!"

✓✓Kumbe Kuna uwezekano wa baraka ya MUNGU kuanzia kwa Babu, watoto wake hadi Wajukuu zake kama Mtu huyo alizingatia maelekezo ya MUNGU wa Mbinguni katika KRISTO YESU.
Biblia inasema WAPATE KUFANIKIWA WAO NA WATOTO WAO, inawezekana kubarikiwa kwa sababu umetokea familia iliyobarikiwa na MUNGU wa Mbinguni.

Mwanzo 28:4" Akupe MBARAKA WA IBRAHIMU, WEWE NA UZAO WAKO pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, MUNGU aliyompa Ibrahimu."

✓✓Kumbe Ibrahimu alikuwa amebarikiwa na hadi Uzao wake umebarikiwa, vipi kama Wewe unatokea familia iliyobarikiwa na MUNGU kama familia ya Ibrahimu?

Ukweli ni kwamba hutatumia Nguvu nyingi kupata baraka nyingi.
Maana Mtu kutoka Uzao wa Ibrahimu alikuwa amebarikiwa tayari hata kabla hajaanza kutafuta baraka maana alikuwa anatoka familia iliyobarikiwa.
Hata Mimi Peter Mabula namwomba MUNGU anipe kutembea kwenye kusudi lake na kanuni zake ili nipate kubarikiwa na Uzao wangu ili baadae Wajukuu zangu wajue wamebarikiwa kwa sababu Babu yao alifuata maagizo ya ROHO MTAKATIFU.
Kuna Mtu nashuhudiwa rohoni wakati huu anapata maumivu makubwa moyoni anaposoma ujumbe huu wakati huu maana Babu zake hawakuleta baraka Bali laana zinazomtesa hadi yeye leo, ndugu Kuna ushindi katika damu ya YESU KRISTO kwa Jina la YESU KRISTO.

Hata Wewe unayesoma somo hili Wala usiumie kwa ajili ya Babu zako ambao badala ya kusababisha baraka kwako walisababisha laana kwa Uzao wao kwa sababu walikuwa wanaabudu sanamu na kushirikiana na waganga wa kienyeji hivyo wakamkosea MUNGU Baba wa Mbinguni.

Lakini Iko wazi kabisa kwamba Kuna baraka ambazo chanzo Chao ni kutoka familia iliyobarikiwa.

✓✓Nakusihi ndugu mche MUNGU katika KRISTO YESU ili usababishe watoto wako na Wajukuu zako na vitukuu wawe wametoka katika familia iliyobarikiwa ambayo chanzo Cha familia hiyo ni Wewe. MUNGU atakubariki Wewe na Uzao wako.

✓✓Usikubali kufuata Mawakala wa Shetani na usikubali kufuata mizimu au kwenda kwa waganga wa kienyeji ili familia Yako isilaaniwe.

3.  Kuwa na mahusiano mema na Mtu aliyebarikiwa.

Ngoja nianze na mfano huu, ni kwamba tunafahamu kwamba Ibrahimu, Isaka na Yakobo walikuwa wamebarikiwa na MUNGU.

Mwanzo 27:29 "Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, NA ATAKAYEKUBARIKI ABARIKIWE."

Hii Ina maana gani?
✓✓Ukimbariki Ibrahimu au Isaka au Yakobo  unabarikiwa hivyo chanzo Cha baraka Yako kinakuwa ni kwa sababu una uhusiano mzuri na Mtu aliyebarikiwa na MUNGU.

✓✓Huwezi ukambariki Yakobo au Isaka kama unamchukia hivyo baraka  ya MUNGU iliyo ndani yake haiwezi kuja kwako.

✓✓Chanzo Cha baraka ni kuwa na uhusiano mzuri na Mtu aliyebarikiwa na MUNGU wa Mbinguni katika KRISTO YESU.

✓✓✓Na kwa taarifa Yako tu ni kwamba kama unahitaji baraka ya MUNGU basi hakikisha unakuwa na uhusiano Mzuri na Bwana YESU KRISTO ambaye amebarikiwa.

Mathayo 23:39 "Kwa maana nawaambia, Hamtaniona kamwe tangu sasa, hata mtakaposema, Amebarikiwa ajaye kwa jina la BWANA."

✓✓Bwana YESU KRISTO ni mbarikiwa hivyo ukiwa na uhusiano mzuri naye utabarikiwa.

Tatizo la watu wengi ni kwamba hawataki Kutunza mahusiano yao na Bwana YESU KRISTO aliyebarikiwa.

Yeye Leo katika kuwataka watu wawe na uhusiano mzuri naye anasema  "Mkinipenda, mtazishika amri zangu."-Yohana 14:15
Hakikisha ndugu unakuwa na uhusiano mzuri na YESU KRISTO mbarikiwa.

4. Kutii maagizo ya MUNGU na kanuni zake za namna ya kumfanya Mtu kubarikiwa.

Kumbu 28:1-6 " Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo."

✓✓Kuna kanuni nyingi za MUNGU zinazotengeneza baraka mfano ni kutoa Sadaka,Zaka na Dhabihu.

Malaki 3:10-11 " Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi."

✓✓Ndugu, kufanya Maombi tu bila kufuata Kanuni zingine za kubarikiwa huwezi kubarikiwa.
Hakikisha unaomba na unafuata kanuni za ki MUNGU zinazoleta baraka.

Ndugu chanzo  Cha baraka ni kuwa mtii katika maagizo ya MUNGU na kutembea kwenye kanuni zake zinazotengeneza baraka.

Njia kuu na Bora zaidi ya baraka za MUNGU ni kuwa ndani ya KRISTO huku ukiwa mtii wa maagizo yake  na kufanyia kazi kanuni zake zinazoleta baraka,wanaozingatia kanuni hizi ni wachache sana na ndio maana waliobarikiwa na MUNGU ni wachache.
MUNGU akusaidie katika hili.
Pia kama hujampokea YESU KRISTO kuwa Mwokozi wako nafasi hiyo unayo Sasa, nakusihi sana Mpokee Leo awe Bwana na Mwokozi wako, jiunge na Kanisa la kiroho wanaomhubiri YESU KRISTO huko uliko na utafanya vyema sana 
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments