SADAKA NI NINI?

 

Na Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Sadaka ni Nini?

✓✓Sadaka ni Matoleo ya hiari ambayo Mwanadamu humtolea MUNGU katika KRISTO YESU kupitia Madhabahuni zake takatifu au kupitia Watumishi wa Bwana YESU waaminifu.


✓✓Kuhusu kutoa sadaka Madhabahuni kwa MUNGU katika KRISTO YESU.

Kumbu 12:11 "wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA."



✓✓Kuhusu kupitia Watumishi wa MUNGU waaminifu mfano ni Musa aliyeambiwa na MUNGU apokee Sadaka kwa Watu wanaotoa kwa MUNGU.


Kutoka 25:2" Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda MTATWAA KWAKE SADAKA YANGU."


Hivyo sadaka Yako njema unaweza ukaipeleka Madhabahuni kwa MUNGU ambako ROHO MTAKATIFU huonyesha Nguvu zake na Sadaka zako njema unaweza ukampa Mtumishi Mwaminifu wa Bwana YESU KRISTO ambaye amani ya KRISTO ndani Yako itaamua utoe kwa MUNGU kupitia huyo Mtumishi Mwaminifu wa Bwana YESU KRISTO.


✓✓Sadaka kwa MUNGU ni kitu Cha kudumu kwa Wanadamu katika vizazi vyao vyote, ndio maana tunaona Wanadamu wema walimtolea MUNGU sadaka tangu kizazi Cha Kwanza hadi kizazi Cha leo.


Kizazi Cha Kwanza mfano hai aliyetoa sadaka njema kwa MUNGU ni Habili


Mwanzo 4:4 "Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;"


Habili huyu ni Mtu wa kizazi Cha Kwanza maana waliowahi kuishi kabla yake ni watu 3 tu kukingana na Biblia Takatifu, yaani Adamu, Eva na Kaini.


Hadi kizazi Cha leo Biblia inaagiza utoaji Sadaka kwa MUNGU katika KRISTO YESU kuwa ni jambo jema sana na lenye faida nyingi kwa mtoaji.


2 Wakorintho 9:7 " Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana MUNGU humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."


Hivyo ukisoma Biblia Kuna mambo mema mengi yaliyodumu vizazi vyote vya Wanadamu ikiwemo sadaka.


Sadaka ni Ibada hivyo ukitoa sadaka kwa Madhabahu za Giza au kwa mawakala wa Shetani ujue umeshiriki katika Ibada ya sanamu au Ibada ya miungu.


1 Wakorintho 10:20 " Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa MUNGU; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha BWANA na kikombe cha mashetani."


Pia ni Muhimu kujua pia kwamba sadaka za waovu ni chukizo kwa MUNGU.


Mithali 21:27 "Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!"


Hivyo usijifariji kwa kuiba Kisha sehemu ya pesa Yako ukatoa sadaka ukidhani kwa njia hiyo utasamehewa au utampendeza MUNGU, jua sadaka Yako ni machukizo.

Mtu asifanye ukahaba Kisha ujira wa ukahaba akatoa Sadaka akidhani ni sawa tu, ukweli mmoja sadaka ya Mtu huyo ni machukizo kwa MUNGU.

Hivyo ni Muhimu sana kutoa sadaka safi inayotokana na usafi wa Mtu au inayotokana na kazi njema na halali.

Sadaka ni ya Muhimu sana ila ni Muhimu sana pia kujajua haya.


Hivyo usiache kutoa sadaka na Zaka ila usitoe kamwe kwa watu ambao YESU KRISTO sio Mwokozi wao.

Hakikisha unatoa unatoa Sadaka kwa MUNGU wa Mbinguni anayeabudiwa katika KRISTO YESU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.

MUNGU wa Mbinguni aikumbuke sadaka zako na Zaka zako na akutendee mema kila akizikumbuka.

Zaburi 20:3-4 " Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote."

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

+255714252292

YESU KRISTO anaokoa hivyo amua Kuokoka leo.

Comments