USHAURI KWA WANANDOA NA WANAOTARAJIA KUINGIA KATIKA NDOA.

 

Peter na Jemimah Mabula 
Watenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Leo natoa ushauri kwa walio kwenye Ndoa na wanaotarajia kuingia kwenye Ndoa.

1. Msiwe watu wa kufarakana katika ndoa yenu.

1 Wakorintho 1:10" Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu YESU KRISTO, kwamba nyote mnene mamoja; WALA PASIWE KWENU FARAKA, BALI MHITIMU KATIKA NIA MOJA NA SHAURI MOJA."

✓✓Na mafarakano mengi ya Wanandoa huanzishwa ama na Ndugu au marafiki.

Mithali 16:28 "Mtu mshupavu huondokesha fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki."

Isiwe Baba anataka mfanikiwe jambo fulani jema lakini Mama anafanya kila mbinu kulizuia jambo hilo, mkifanya hivyo hamtafika popote.

Sio Mama anataka mzae lakini Baba hataki kuzaa wakati katika ndoa yenu mna mtoto mmoja au hata mtoto mmoja hamna, ni vyema wanandoa kunia mamoja.

Pataneni kwa upendo katika mambo yote ili mfanikiwe pamoja.

Wafilipi 2:2-3 " ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake."


2. Mmeshafunga Ndoa hakikisheni mnajitegemea.

Kama haujafunga Ndoa hakikisha Mkishafunga ndoa hakikisheni mnajitegemea makazi na sio kuishi kwa wazazi au ndugu.

Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."

✓✓Mwanaume uliyeoa au unayetaka kuona lijue hili vyema.
Sio wengine wakusaidie kukulelea mke wako kwa sababu mnaishi kwao.
Sio wengine wakusaidie kukulelea watoto wako, ukifanya hivyo unaweza kuwafanya watoto wako baadae wakuone wewe wa kawaida tu huku wakiwathamini walezi wao au waliojitaabisha kwa ajili yao.

✓✓Kuna madhara mengi zaidi yanayoweza kujitokeza kama mtafunga ndoa kisha kwa muda mrefu muendelee kuishi kwa wazazi au ndugu.

Ni heri hata kabla hamjajenga mkapange na muwe na maisha yenu.

Kuishi kwa watu kunaweza kuwafanya nini hata msiwe na uhuru na ndoa yenu, pia migogoro mingi na maneno maneno yanayoweza kuharibu ndoa yenu ni rahisi kujitokeza.

Ni heri uwaache Baba yako  na Mama yako na uambatane na Mume wako au Mke wako katika maisha yenu ya ndoa kama Biblia hapo juu inavyosema.

3. Wanandoa  ishini maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.

2 Wakorintho 6:2 "Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; TAZAMA SIKU YA WOKOVU NI SASA"

Utajisikiaje Mume wako au Mke wako anaenda mbinguni huku wewe unaenda jehanamu?

Utajisikiaje Mume wako au Mke wako anaenda jehanamu huku wewe unaenda mbinguni?

✓✓Mbinguni hakuna kuoana lakini mliishi duniani kama Mke na Mume  ili msaidiane pia ili wote muipate Mbingu.

✓✓Ni jukumu la kila mmoja kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.

✓✓Msaidie mwenzi wako kama ameanza kukengeuka, muonye, muombee na mshauri ili aishi maisha matakatifu siku zote.

✓✓Kuishi maisha matakatifu kwenu nyote kutasababisha ROHO MTAKATIFU awe na ninyi, na huyo akiwa na ninyi hata ndoa yenu itakuwa baraka kuu kwa watu wote.

Naamimi ndugu Kuna kitu umejifunza katika somo hili fupi

✓✓MUNGU awape neema ya kuishi maisha matakatifu ya ndoa yenu.

✓✓MUNGU awape watoto wa kiume na wa kike katika ndoa yenu.

✓✓Katika ndoa yenu mpingeni shetani naye atawakimbia.

✓✓Iweni na ibada ya familia kila siku, iweni na maombi ya pamoja kama familia huku mkimtanguliza MUNGU katika yote kuhusu ndoa yenu, uchumi, uzao na familia yenu.

✓✓Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri. 
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU KRISTO Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU KRISTO? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU KRISTO Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU KRISTO Kwako.
By Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
+255714252292(Ushauri, Whatsapp,Maombi, Sadaka ya kuipeleka Injili)
Uki-share somo hili kwa maandishi  naomba share  kama lilivyo,usibadili jina wala chochote.
Ubarikiwe 

Comments