USISAHAU KUMKIRI YESU KRISTO KAMA MWOKOZI WAKO.

 


Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 


Imani ya kumkiri YESU KRISTO kuwa Bwana na Mwokozi ndio sifa ya kwanza ya wateule wa MUNGU.

Hakuna kuwa mteule wa MUNGU bila kumkiri YESU KRISTO kama Mwokozi.

Warumi 10:9-10 " Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."

✓✓Ndugu, mkiri YESU KRISTO katika maisha yako, matendo yako.

Mtu yeyote duniani asiyemkiri YESU KRISTO kama Mwokozi wake, mtu huyo Moja kwa Moja hana MUNGU wa kweli.

1 Yohana 2:23 "Kila amkanaye MWANA, hanaye BABA; amkiriye MWANA anaye BABA pia."

Ukimkataa YESU KRISTO Moja kwa Moja umemkataa MUNGU.

✓✓Mkiri YESU kwa kinywa chako kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

✓✓Kumpokea YESU kama Mwokozi kisha ukaanza kuishi maisha matakatifu katika yeye huko ndio kuwekea muhuri ukiri wako kwa YESU.

Kutenda dhambi ni kumkana YESU hata kama ulishawahi kumkiri zamani kisha ukamwacha na kuifuata dunia.

Ndugu, mkiri YESU kwa kinywa chako ya kwamba ndiye Mwokozi wako, acha dhambi na kataa machukizo ya dunia maana hayo yanafuta ukiri wako kwa YESU.
Wanaomkiri YESU inawapasa kutembea katika utakatifu.
Mkiri YESU KRISTO siku zote za maisha yako maana Iko faida.

Mithali 3:6 "Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako."

MUNGU akubariki.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments