MAANA 6 ZA KUNENEPA NDOTONI

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe Ndugu.
Jifunze kitu kuhusu Ndoto za kujiona Ndotoni umenenepa.

Ndoto hizi ni zile Kujiona wewe Ndotoni  au kumuona Ndotoni Mtu Mwingine mwembamba amenenepa au Mtu wa akawaida amenenepa au  Mtu mnene.
Sio kila unene Ndotoni una maana mbaya na sio kila unene Ndotoni una maana nzuri, inategemea ndoto uliyoona juu ya unene inaelekea upande gani.

1. Kujiona Ndotoni Wewe au kumuona Ndotoni Mtu mwembamba amenenepa sana ni ishara ya Mtu kutenda maovu bila kikomo, yaani amemwacha YESU KRISTO Mtu kwa kugeukia uovu ambao anaufanya uovu huo kama Kuna Mtu anashindana naye kufanya hayo machukizo.

 Mtu huyo kwa Sasa anafanya dhambi bila kiasi yaani ni mfululizo.

Yeremia 5:28 "WAMEWANDA SANA, wang'aa; NAAM, WAMEPITA KIASI KWA MATENDO MAOVU; ............"

Kuwanda maana yake kunenepa.
Kama ni Wewe amua Kuokoka up ya kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako Kisha chagua kuanza kuishi Maisha matakatifu haraka sana 

2. Kuota umenenepa au Kuna Mtu unamfahamu amenenepa sana Ni ishara ya kuufurahia wema wa MUNGU katika KRISTO YESU.

 Nehemia 9:25 "Wakaitwaa miji yenye boma, na nchi yenye neema, wakazitamalaki nyumba zilizojaa vitu vyema, birika zilizochimbwa, mizabibu, na mizeituni, na miti mingi yenye matunda; HIVYO WAKALA, wakashiba, wakanenepa, wakajifurahisha KATIKA WEMA WAKO MWINGI."

Unaweza ukamuona Mtu amenenepa ndotoni maana yake ataufurahia wema wa Bwana YESU KRISTO baada ya kutendewa Miujiza na yeye.
Unene wa Ndotoni unaweza kuwa ni taarifa ya kiroho kwamba siku sio nyingi utaufurahia wema wa MUNGU wa Mbinguni.

3. Kunenepa Ndotoni ni ishara ya kwamba Mtu husika atanenepa katika ulimwengu wa mwili.

Ni Hali yake ya baadae katika kuishi kwake, hivyo ni ama amshukuru MUNGU kama anafurahia kunenepa au azingatia ulaji ili isipate tatizo la kimwili au kiafya linalosababishwa na unene.


4. Kunenepa Ndotoni maana yake unakula Sasa siku hizi hivyo tambua kwamba Matokeo yake ni kunenepa, hivyo chagua unatakaje.

Kama hutaki kunenepa fanya yatakayokufanya usinenepe sana.

Kama unapenda kunenepa endelea na utaratibu uliopo maana utanenepa.


5.  Kunenepa Ndotoni ni ishara ya kwamba Mtu husika asipojiangalia anaweza kujikuta amemwacha YESU KRISTO au amedharau Wokovu wa MUNGU.


Kumbu 32:15 "Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha MUNGU aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake."

Hivyo ukiota ndoto ya kunenepa na ukagundua ndoto hiyo inaangukia kundi hili basi uwe makini usije ukamwacha YESU KRISTO maana ni hatari sana kwako.

6. Kunenepa Ndotoni ni ishara ya kujisahau na kuanza kuabudu miungu.

Kumbu 31:20 "Kwa kuwa nitakapokwisha kuwatia katika nchi niliyowaapia baba zao, imiminikayo maziwa na asali; nao watakapokwisha kula na kushiba, na kuwanda; ndipo watakapoigeukia hiyo miungu mingine, na kuitumikia, na kunidharau mimi, na kulivunja agano langu."

Ndugu, katika hali halisi usije ukajisahau na kusahau Wokovu wa KRISTO.

Ndugu usijisahau ukamwacha YESU KRISTO na kufuata miungu.
Usijisahau ukaanza kuabudu miungu.
MUNGU wa Mbinguni akubariki.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni.
Ubarikiwe 



Comments