JINSI GANI KIJANA AISAFISHE NJIA YAKE?

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

 

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.

Karibu ujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


Je ni jinsi gani kijana aisafishe njia yake?

Kwa maana nyingi ni kwa jinsi gani gani kijana atunze Maisha yake katika wakati wake wa ujana?


Zaburi 119:9 "Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako."


Andiko hili katika tafsiri ya BHN Biblia inasema "Kijana atatunzaje maisha yake kuwa safi? Kwa kuyaongoza kadiri ya neno lako."


◼️Kumbe kulingana na andiko hilo tunagundua kwamba ili kijana aishi maisha safi na yenye ushuhuda siku zote ni lazima aishi kwa kulifuata Neno la MUNGU.


✓✓Yaani ni kama kusema hivi " Ni kwa namna gani kijana atatunza maisha yake ili yawe maisha matakatifu mbele za MUNGU na yawe maisha safi mbele ya watu wa MUNGU. Ili iwe hivyo kwa kijana basi inampasa kijana huyo aishi kwa kulitii na kulifuata Neno la MUNGU inavyosema?"


✓✓Sasa jiulize swali hili kijana


 " Ni jinsi gani nitaishi maisha matakatifu nikiwa kijana hadi nikiwa mzee"


Kisha wewe mwenyewe jijibu hivi


 "Ni kama tu nikiishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU huku nikiwa na bidii katika kulitii Neno la MUNGU na kulifanyia kazi daima. "


Ni jinsi gani kijana asafishe maisha yake hata yawe safi mbele za MUNGU siku zote?


◼️Ni kwa kijana huyo kuisha maisha matakatifu katika KRISTO YESU huku akiwa na msingi mzuri katika Neno la MUNGU na maombi.


Ujumbe huu ni kwa kila kijana.


 ◼️Kijana ni nani?


✓✓✓Kijana ni Mwanadamu yeyote wa kiume au wa kike asiye mtoto wala mzee.


Naamini umejitambua Sasa Kijana.

Mimi Peter Mabula leo nimewiwa sana nilete ujumbe huu na natamani kila Kijana Duniani ausome ujumbe huu na kuufanyia kazi.


✓✓Kijana isafishe safari yako ya maisha ya duniani kwa kulitii Neno la MUNGU huku ukilifuata Neno la MUNGU linavyokuambia.


◼️Ukilifuata Neno la MUNGU litakufanya uwe mtii hata kwa wazazi wako na watu wengine.


Utawatii kwa utii unaoelekezwa na neno la MUNGU.


Waefeso 6:1 "Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika BWANA, maana hii ndiyo haki."


◼️Kijana wa kike au wa kiume nakuomba anza kuisafisha njia yako ya safari ya kuishi kwako duniani, kwa wewe kulitii Neno la MUNGU na kulifuata.


MUNGU akukumbuke na kukubariki ukizingatia.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

Ubarikiwe

Comments