Jinsi ya kuandaa somo/ujumbe wa Neno la MUNGU kwa ajili ya kufundisha watu.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

Jinsi ya kuandaa somo/ujumbe wa Neno la MUNGU kwa ajili ya kufundisha watu.

Ziko njia nyingi za kuandaa ujumbe wa Neno la MUNGU, Moja kati ya hizo ni hii.


1. Ni lazima ujue Kichwa cha somo husika unalotakiwa kufundisha, 


2.Kiini cha somo 


3. Hitimisho.


Muhimu kujua.


✓✓ Lazima ulijue lengo la MUNGU juu ya kiini cha ujumbe wako.


✓✓Wakati wa kiini cha ujumbe wa somo wakati mwingine hasira ya MUNGU inahitajika na sio mawazo yako.


✓✓ Neno unalofundisha linaitwa Rhema yaani Neno la Ufunuo ambalo ROHO MTAKATIFU amekupa ufundishe. 


Neno hilo Rhema lazima litoke katika maandiko ya Biblia. 


Hapo ndipo tunaona tofauti ya Neno na andiko. 


Kwa sababu lazima ujumbe huo chanzo chake kiwe ROHO MTAKATIFU basi ni lazima uwe muombaji sana na mtii sana kwa ROHO MTAKATIFU ndipo utafundisha ujumbe sahihi kutoka kwa MUNGU.


✓✓ Usiandae ujumbe ukiwa na misimamo yako binafsi na usiandae ujumbe wa Neno la MUNGU ukiwa na watu moyoni ambao unawalenga bila kusudi la MUNGU.


✓✓ Usifundishe kidhehebu wala kidini bali fundisha Kiinjili yaani Injili ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.


✓✓ Kwenye fundisho lako usilenge kumsapoti mtu yeyote bali iseme injili.


Kila somo lako hakikisha linawafanya watu:


1. Waione ndani ya ujumbe huo injili ya KRISTO iokoayo.


2. Wampokee YESU KRISTO na kuokoka ambao hawajaokoka.


3. Wafunguliwe kutoka vifungo vya giza kama wakitii Neno la MUNGU.


4. Wamwamini MUNGU na kumtegemea katika maisha yao.


5. Wajitenge mbali  na dhambi na kila mambo ya dunia yachukizayo.


Ubarikiwe kwa dondoo hii.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

+255714252292

Mtenda kazi katika shamba la MUNGU wa Mbinguni.

Comments