LEO OMBA UKIBOMOA MADHABAHU YA KISHETANI INAYOFANYA VITA NA WEWE.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu!


Leo omba Maombi ya kubomoa Madhabahu za kishetani.


◼️Kuna Madhabahu za kishetani za familia.


◼️Kuna Madhabahu za kishetani za ukoo.


◼️Kuna Madhabahu za kishetani za jamii.


◼️Kuna Madhabahu za kishetani za mji uliopo.


◼️Kuna Madhabahu za kishetani za nchi.


Ukisoma Waamuzi 6:25 Biblia inasema " Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, UKAIANGUSHE MADHABAHU YA Baali, ALIYO NAYO BABA YAKO, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;"


Hii madhabahu ya shetani ilikuwa nyumbani kwa mzee Yoashi ambaye ni Baba yake Gideoni.

Madhabahu hii ilikuwa madhabahu ya kifamilia na kiukoo ndio Maana Mtu wa MUNGU aitwaye Gideoni aliambiwe ahakikishe kwa kutumia sadaka anaiangusha madhabahu hiyo ya shetani.


Ukitaka ujue kwamba hii pia ilikuwa madhabahu ya giza ya jamii na ilikuwa madhabahu ya giza ya mji soma Waamuzi 6:28  inayosema kwamba "Hata WATU WA MJI walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa."


Biblia inaonyesha kwamba watu wa mji  walichukia sana hadi wakataka wamuue Gideoni kwa sababu ndiye  aliyeiangusha kwa sadaka.


Kwanini watu wa mji wachukie madhabahu yao kuangushwa?

Ni kwa sababu ilikuwa pia madhabahu ya shetani ya mji.


Nini tunajifunza?


Wako watu wa MUNGU wanateswa na madhabahu za giza za familia, za ukoo, za jamii na za miji.


Gideoni alikuwa mtu wa MUNGU halisi lakini mambo mengi yalizuiliwa kwake na madhabahu ya shetani ndio Maana Malaika wa MUNGU akatumwa ili ampe Maarifa ya Nini Cha kushughulikia ili kuleta baraka na ushindi.

Ndio Maana Baada ya Gideoni kuiangusha madhabahu ya shetani mambo mengi yalibadilika kwake katika uchumi, kibali na n.k


Ndugu, Mimi Peter Mabula nawiwa tu muda huu nikusihi uombe kubomoa Madhabahu ya giza inayokusumbua.

Ibomoe na kuiangusha madhabahu hiyo katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.


Ndugu ni kwamba; Mji unaweza ukakukataa na usiweze kufanikiwa ukiwa katika mji huo, hadi utakapofanikiwa kuvunja Madhabahu za kishetani za mji huo.


✓✓Leo katika jina la YESU KRISTO omba ukivunja Madhabahu za kishetani.


✓✓Leo katika jina la YESU KRISTO omba ukiharibu Madhabahu zote za kishetani.


✓✓Leo katika jina la YESU KRISTO omba ukibomoa Madhabahu zote za kishetani.


✓✓Leo katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai omba ukiangamiza Madhabahu zote za kishetani.


Unaweza ukafungua biashara katika  mtaa Fulani au kijiji Fulani ambapo ndani ya kijiji hicho kuna mganga wa kienyeji ambaye hutaka ukajipendekeze kwake ndipo utafanikiwa, Ndugu usipomwita Bwana YESU kwenye biashara yako hakika mganga atakuzuilia mafanikio yako, hadi utakapoivunja Madhabahu yake ya kishetani kwa Maombi ndipo utafanikiwa na kustawi kibiashara. 


Ni muhimu sana kila uendako uwe kwanza unavunja Madhabahu za kishetani katika eneo hilo.


Leo omba ukivunja Madhabahu zote za waganga na wachawi, vunja Madhabahu zote za ardhi, vunja Madhabahu zote za manuizi ya kipepo na makafara ya kishetani. Ni rahisi sana kushinda kupitia jina la YESU KRISTO Mfalme wa uzima. 


Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."


√√Utayaweza yote kwa YESU Mwokozi wako.


✓✓Utawashinda wa kishetani ukiwa na YESU tu.


✓✓Mtii YESU kupitia Neno lake na omba kwa imani na utakatifu. 


Kama wachawi hawajawahi kukukimbia basi wakati huu mmoja watakukimbia na hata kukutazama hawataweza. 

Kama waganga wanakuchezea mchezo wa kukufilisi, wakati huu watashangaa Madhabahu zao zikiwadondokea na nguvu zao zikifutika kwa jina la YESU KRISTO Mwamba wa milele.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.

+255714252292(Whatsapp, Maombezi, Ushauri, sadaka n.k)

Ubarikiwe sana

Comments