![]()  | 
| Na Mwl Peter Marco Mabula  Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu.  | 
Kipengele: MAOMBI YA KUZIFUNGA KAZI ZA SHETANI.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe!
Karibu tujifunze Neno la maombi ya Leo.
Leo tunaomba ili kuzifunga kazi zote za shetani katika maisha yetu.
✓Nini maana ya kufunga kazi za shetani?
✓✓Neno "kufunga kazi za shetani" lina maana ya kuzuia nguvu za giza ili zisifanye kazi.
✓✓✓Wewe mteule wa KRISTO unayo mamlaka ya kufunga kazi ya shetani yeyote popote duniani na kazi hiyo ya giza ikaacha kufanya kazi.
Mathayo 16:19 "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."
◼️Mamlaka ya kuzifunga kazi za shetani umepewa wewe Mteule wa MUNGU katika KRISTO na mamlaka ya kufungulia ushindi wa ki MUNGU umepewa pia wewe mteule wa KRISTO.
Muhimu tu tambua ni wapi kuna kazi za shetani zinazoleta madhara kwako.
Kumbuka Biblia inaonyesha shetani yaani nguvu za giza huzunguka duniani, tena hutembea huku na huku humo.
Ayubu 1:7 "BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo."
Kama mashetani huzunguka duniani basi hata wewe uko duniani, hata biashara yako iko duniani, hata watoto wako wako duniani, hata ndoa yako iko duniani hivyo anaweza kuvamia akipata nafasi.
Kama shetani huzunguka duniani katika eneo ambalo linaitwa "Huku na huku humo" kama Biblia inavyosema basi ujue nguvu za giza zinaweza kuvamia familia, ukoo, biashara, kazi, uchumba, ufahamu, mwili n.k
◼️Haijalishi shetani anaweza kuvamia maeneo mengi lakini katika KRISTO YESU tumepewa mamlaka ya kuzifunga kazi za shetani na hazitaweza tena kufanya kazi.
Tena Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu ametupa mamlaka kubwa sana yaani tuna mamlaka ya kuzidi nguvu za giza zote.
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
Tena MUNGU wetu ametupa kibali cha kukusudia mambo ya ushindi wetu na yanatokea.
Ayubu 22:28 "Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako."
Leo hebu zifunge kazi za shetani kokote katika Maisha yako.
Kama kuna kazi za shetani kazini kwako ili kukuharibia kazi, Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa katika jina la YESU KRISTO.
Kama kuna kazi za shetani katika ndoa yako au katika uchumba ili kuua ndoa au kufuta uchumba wako, Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Kama kuna kazi za shetani zimeinuka katika familia yako au ukoo wako ili kukutenga wewe au kukudhulumu,Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Kama kuna kazi za shetani zimeinuka katika ndoa yako hata mwenzi wako hakutaki tena, hakuhitaji na anahudumia wengine,Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Inawezekana pepo la uzinzi au la usaliti au la uasherati au la uongo au wivu wa kipepo limevamia ndoa yako au familia yako, Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Inawezekana nguvu za giza za magonjwa, kukataliwa, kuonewa, nguvu za giza zimetawala kwako au kwa watoto wako, Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Inawezekana wewe au wapendwa wako wanaandamwa na roho za ajali, roho za balaa au mikosi au majanga, Leo zifunge kazi hizo za shetani, zifunge kwa jina la YESU KRISTO.
Ukizifunga kazi za shetani kwa maombi hakika hizo kazi za shetani hazitafanya kazi kuanzia Leo, huo ndio uhakika ambao Mimi Peter Mabula nakueleza Wewe rafiki yangu maana katika Jina la YESU KRISTO itakuwa hivyo hivyo ukiomba.
Nini ufanye?
1. Omba maombi ili kuzifunga kazi za shetani zote katika maeneo yako(Yataje moja baada la lingine maeneo hayo)
2. Hakikisha kimaombi maeneo haya matano ya kwako yako salama bila kuvamiwa na nguvu za giza.
Maeneo haya ni mwili, ndoa yako, familia yako, kibali chako na uchumi wako.
3. Wasambaratishe mawakala wa shetani ambao hukaa kikao na kuandaa nguvu za giza za kukuvamia.
4. Futa maagano yote ya kipepo kati yako na nguvu za giza, mwenzi wako na mashetani, katika ya familia na Madhabahu za giza, katika ndugu zako au mtu wa karibu na mawakala wa giza, futa agano hilo.
5. Futa mikataba ya kishetani yote inayokuhusu au inayomhusu mtu wako yeyote wa karibu.
Wewe ni mshindi hakika.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU wa Mbinguni.
+255714252292
Omba katika Jina la YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Miujiza.
Ubarikiwe

Comments