MAOMBI MAALUMU (Day 14)

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 



Kipengele: MAOMBI YA KUVUNJA MADHABAHU ZA GIZA.


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze kisha tufanye maombi kutokana na tulichojifunza.

Somo hili ni pana sana ila nitapitia baadhi ya maeneo ili tupate ujumbe wa kutupeleka katika maombi ya ushindi.


Leo ki maombi tunavunja na kubomoa na kuharibu madhabahu za giza zote zilizoshikilia chochote kwetu.


Madhabahu za giza ni nini?


◼️Madhabahu za giza ni mahali ambapo vitu kutoka ulimwengu wa roho wa giza hupitia kabla ya kuja kwenye ulimwengu wa mwili.


◼️Madhabahu za giza ni mahali ambapo vitu vya kishetani hutengenezwa ili viwaletee madhara watu.


◼️Madhabahu za giza ni sehemu ambapo mawakala wa shetani hujiimalisha, hupata nguvu zao za kipepo, hufanya vikao na hupanga mipango yao ya kipepo.


◼️Madhabahu za giza ni mahali ambapo wakuu wa giza, wanadamu wanaotumika kipepo, majini, mizimu na kila mapepo hukaa kama kituo chao kikuu kabla ya kuwavamia wanadamu.


◼️Madhabahu za giza ni mahali ambapo shetani huabudiwa.


✓✓Siku zote agizo la Neno la MUNGU ni kwamba tuziangushe chini Madhabahu za giza zote, mfano ni huu

Waamuzi 6:25 "Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;"


Huyu alipewa maelekezo ya kuiangusha Madhabahu ya kishetani ya familia yake, ukoo wake na mji wao, aliambiwa atumie sadaka kuiangusha Madhabahu hiyo ya giza.

Madhabahu za giza ni eneo linalojengwa na mawakala wa kuzimu kwa ajili ya kutolea kafara za kipepo au kufanyia kafara za kipepo.

Mfano ni huu Zaburi 106:37 '' Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani."


Ni jambo la hatari sana mtu kutoa sadaka kwa mashetani ili kuufunga uzao wake mwenyewe.


✓✓Matatizo mengi ya watu hutokana na Madhabahu za giza pamoja na wafanya kazi wa Madhabahu hizo za giza.


✓✓Kuna magonjwa ya kipepo hutokana na Madhabahu za giza, kuna matatizo na ajali hutengeneza na Madhabahu za giza.


✓✓Mwenzi wako kama anamilikiwa na Madhabahu ya giza ujue ndoa yenu itakuwa na migogoro mingi mno.


Moja ya kitu hatari sana kwa mwanadamu ni Madhabahu za giza, ndio maana MUNGU aliwaonya sana wana wa Israeli ili wasishirikiane kivyovyote na Madhabahu za giza.

Kutoka 34:12-16 " Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao. Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni MUNGU mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao."


Ni maonyo mengi MUNGU aliyatoa kwa watu wake ili kujitenga mbali na miungu.


Kwanini tuharibu Madhabahu za giza?


1. Ukishirikiana na Madhabahu za utateseka sana, hivyo jitenge mbali na Madhabahu za giza.


2. Usipoiharibu Madhabahu inayokutesa ujue tatizo lako halitaisha.


3. Usipoziangusha Madhabahu za giza ujue matatizo yanayotokana na Madhabahu hizo kwako yataendelea.


◼️Umepewa kibali na MUNGU katika KRISTO YESU cha kuvunja, kubomoa na kuharibu Madhabahu za giza na utashinda.


Kumbu 7:5 "Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."


✓✓✓MUNGU amekupa kibali cha kuhakikisha unalifuta jina la Madhabahu za giza na zitafutika.


Wakati mwingine kwenye ndoto au maono huwa unaonyeshwa ilipo Madhabahu ya giza inayokutesa.

Ndugu leo bomoa na kuvunja Madhabahu za giza zinazokutesa au zilizoshikilia watu wako wa karibu.


Nini ufanye juu ya madhabahu za giza katika yako Leo?


Andiko hili linakujulisha juu ya mambo manne(4) ya kwanza.

Kumbu 7:5 '' Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.''


1. Vunja madhabahu za giza kwa maombi ya vita kwa kutumia Damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.


2. Bomoa nguvo zilizobeba madhabahu hizo za giza.


3. Kata maashera ya hiyo madhabahu.


4. Teketeza kwa moto sanamu zao zote kwenye ulimwengu wa roho.

MUNGU akubariki.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la MUNGU wa Mbinguni.

+255714252292

Ubarikiwe sana.

Comments