![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni |
Kipengele: OMBA MUNGU AFANYE KAZI YAKE KUPITIA WEWE.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote, hili ni somo Muhimu sana.
1 Wakorintho 3:9 " Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na MUNGU; ninyi ni shamba la MUNGU, ni jengo la MUNGU."
Andiko hapo juu linaanza na kitu cha muhimu sana sana kwamba Sisi tu wafanya kazi pamoja na MUNGU.
✓✓Kumbe hatutakiwi kuwa wafanya kazi katika kazi ya MUNGU tu bali tunatakiwa tuwe tunafanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU.
Sio watu wote wanaofanya kazi ya MUNGU hufanya kazi pamoja na MUNGU, ndugu hitaji sana kufanya kazi ya MUNGU ukiwa na MUNGU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU.
◼️Kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU ni wewe kulitumia Neno la MUNGU kwa uhalali katika utumishi wako huku ukifundishwa na ROHO MTAKATIFU.
✓✓Kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU ni wewe kulijua kusudi la MUNGU katika utumishi huo na wewe ukaifanya kazi hiyo sawasawa na Neno la MUNGU huku ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
Wafilipi 2:13 "Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema."
Unaweza ukafanya kazi ya MUNGU ili watu wakuone lakini MUNGU hayuko pamoja na wewe na hajakuagiza chochote, hiyo ni hatari.
◼️Kumbuka kufanya kazi na MUNGU sio kazi ya utumishi tu hata kazi zingine kama serikalini, kwenye kampuni n.k
✓✓Mfano hai ni Yusufu alikuwa Waziri mkuu au makamu wa Rais wa Misri, akifanya kazi hiyo pamoja na MUNGU ndio maana alifanyika msaada kwa mataifa mawili ili wasife njaa yaani Israeli na Misri.
Yusufu anakiri katika andiko hili kwamba ni MUNGU ndio alimpeleka na kuwa pamoja naye ili kuokoa Maisha ya watu.
Mwanzo 45:5 "Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana MUNGU alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu."
✓✓Hata kufanya kazi ya ndani, unaweza ukaifanya kazi hiyo ukiwa pamoja na MUNGU.
Mwanzo 39:2" BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri."
✓✓Hata kazi Yako ya ualimu, Udaktari, unesi,Uwaziri,Urais, ubunge, udiwani, uuzaji duka,ukulima n.k kazi hiyo njema unaweza ukaifanya pamoja na MUNGU.
◼️Kwa habari ya Watumishi waaminifu wa MUNGU katika KRISTO YESU Hili ni jambo la muhimu sana sana la kufanya kazi pamoja na MUNGU.
Mathayo 7:22-23 '' Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.''
◼️Unaweza ukafanya kazi ya MUNGU hata bila kumtii lakini huwezi kufanya kazi pamoja na MUNGU kama humtii MUNGU, ndugu unahitaji sana kuwa na utii kwa MUNGU katika KRISTO YESU.
✓✓Watu wengi tu hufanya kazi ya MUNGU lakini sio wote wanafanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU mwenyewe.
◼️Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanya kazi ya MUNGU na kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU.
◼️Kufanya kazi ya MUNGU ni nini?
✓✓Kufanya kazi ya MUNGU ni kufanya kitu chochote ambacho kipo kwenye kazi ya MUNGU lakini sio lazima MUNGU aambatane na wewe.
✓✓Kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU ni ROHO MTAKATIFU kuambatana na wewe katika kazi ya MUNGU na kukujulisha nini cha kufanya katika kulitimiza kusudi la MUNGU.
Zaburi 32:8 ''Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
◼️Kama ulikuwa hujui ni kwamba hata mtenda dhambi anaweza kufanya kazi ya MUNGU ila MUNGU hawezi kuwa naye katika kazi hiyo, ndio maana kuna wachungaji wazinzi au wachawi au wameingia mikataba ya kishetani lakini ni watumishi wa MUNGU ila MUNGU hajawahi kufanya nao kazi yake, na mbinguni hawajulikani.
Inawezekana ni wewe ni kiongozi Kanisani labda ni kiongozi wa vijana au kwaya au wamama n.k na unatenda dhambi kwa siri huku ukidhani MUNGU anafanya kazi yake pamoja na wewe, ndugu, kama ni hivyo tambua kwamba YESU KRISTO hafanyi kazi yake pamoja na wewe na mbinguni wewe haujulikani japokuwa duniani unaitwa Mtumishi wa MUNGU.
◼️Kila mtu duniani anaweza kufanya kazi ya MUNGU lakini sio kila mtu anaweza kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU.
Hata mtenda dhambi yeyote anaweza kufanya kazi ya MUNGU lakini huyo hawezi kufanya kazi ya MUNGU pamoja na MUNGU.
Unaweza ukafanya kazi ya MUNGU kwa sababu tu una muda wa kuifanya kazi hiyo lakini MUNGU asiwe pamoja na wewe maana humtii.
◼️Ndugu yangu nakuomba usiogope kumtumikia MUNGU ukiwa pamoja na yeye bali ogopa kumtumikia MUNGU ukiwa peke yako bila yeye MUNGU.
Nini ufanye kwenye Maombi?
1. Tubu kwa ajili ya dhambi, maovu na makosa yako vilivyosababisha MUNGU asifanye kazi yake pamoja na wewe. Tubu na rudi kwenye nafasi Yako mbele za MUNGU.
Zekaria 1:3 "Basi, uwaambie, BWANA wa majeshi asema hivi, Nirudieni mimi, asema BWANA wa majeshi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi."
2. Omba ROHO MTAKATIFU akusaidie ili umtumikie Bwana YESU KRISTO huku yeye ROHO MTAKATIFU akiwa pamoja na wewe.
Zekaria 4:6 "Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, SI KWA UWEZO, WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO YANGU, asema BWANA wa majeshi."
3. Omba MUNGU alifunue kusudi lake kwako la utumishi ili uwe unamtumikia ukiwa ndani ya maagizo yake.
Zaburi 32:8 ''Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.''
4. Omba ROHO MTAKATIFU akupe kuelewa wito wako ulioitiwa na MUNGU ili umtumikie ukiwa pamoja na yeye.
Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."
5. Omba Bwana YESU KRISTO akufunulie kuelewa maandiko ikupasavyo ndipo utaweza kumtumikia ukiwa pamoja na yeye.
Luka 24:45 "Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko."
Omba Ndugu na utamuona MUNGU wa Mbinguni katika Maisha yako.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
+255714252292(Whatsapp, sadaka ya kuipeleka Injili, ushauri n.k)
Ubarikiwe sana

Comments