![]() |
| Na Mwl Peter Marco Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni |
Maombi ya toba.
Kipengele: KILA JAMBO LILILOKWAMA LINAHITAJI TOBA KWANZA ILI KUFANIKIWA.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe.
Ukisoma Ufunuo 2:5 Biblia inasema "Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."
Biblia inasema kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu.
✓✓Kumbuka chanzo cha tatizo lako kilisababishwa na nini ili utubu kwa ajili ya chanzo hicho ndipo utapata mpenyo wa kuelekea ushindi.
Mfano unaumwa ukimwi au homa ya ini au homa ya manjano usihangaike tu kusema "Bwana YESU KRISTO niponye" Anza kuomba hivi "Ee MUNGU ninatubu kwa ajili ya tabia yangu ya uzinzi iliyopelekea ugonjwa huu"
Yaani Inawezekana MUNGU alikuonya kabla juu ya madhara ambayo ungeyapata kwa sababu ya dhambi hiyo Wewe ukashupaza shingo, unaporudi kwa MUNGU wakati huu tubu sana kwa ajili ya chanzo Cha tatizo ndipo uombe msaada wa MUNGU.
Kumbuka tamaa huzaa dhambi na dhambi huzaa mauti yaani uharibifu au madhara.
Yakobo 1:15 "Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti."
Sasa usiombe tu MUNGU atoe tatizo au atoe madhara au atoe mauti bali Kumbuka kabla ya mauti ikianza dhambi na kabla ya dhambi ikianza tamaa, Anza kutubia tamaa na dhambi ili mauti Sasa itoke.
Inawezekana wakati wa tamaa tu MUNGU alikuonya ukadharau, kutokuifuata sauti ya MUNGU katika KRISTO YESU ni dhambi hivyo Anza kutubia kiburi chako ndipo uombe tatizo litoke litatoka.
Mfano hupati kazi kwa sababu ulirogwa, chanzo cha tatizo lako ni uchawi ukiofanyiwa, ili MUNGU akusaidie hapo unahitaji kwanza kutubu maana inawezekana ulifunuliwa kuomba ili usirogwe wewe ukadharau na ndio maana ukarogwa, inawezekana ulikuwa mtu wa dhambi ndio maana wachawi wakapata mlango kuingia kwako na kukuroga, usilalamike tu bali tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo ndipo mbingu zitafunguka kwa ajili ya ushindi wako unaouhitaji.
Kuna mahitaji ili ufanikiwe inakupasa kutubu kwanza kwa ajili ya chanzo cha tatizo.
Inawezekana wewe kwa sasa unateseka na vifungo mbalimbali kwa sababu ya makosa ya babu zako au wazazi wako walioingia katika maagano ya kishetani yanayofuatilia hadi vizazi ukiwemo wewe, mababu au wazazi walishakufa lakini mateso unayapata wewe sasa maana wewe unatokana na wao.
Maombolezo 5:7-10 " Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao. Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani. Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo."
Kuna makosa sio yako lakini unateseka wewe kwa sababu ya makosa ya wazazi wako.
Mfano wewe ni mtoto wa muuaji kama Kaini, muuaji huyo ambaye ni baba yako au babu yako alilaaniwa yeye na uzao wake, maana kuna laana ukimwaga damu isiyo na hatia
Mwanzo 4:11-12 " Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani."
Vifungo kama hivyo inakupasa utubu kwa ajili ya chanzo kilichosababisha ukapatwa na tatizo hilo.
Chanzo cha tatizo lako kinaweza kuwa ni wewe mwenyewe, wazazi wako, laana, kurogwa, matambiko, mazindiko, kafara, babu zako, ukoo kuabudu shetani, kupelekwa kwa waganga, ardhi ya eneo n.k
Sasa ukitaka ushinde hapo anza na toba.
✓✓Inawezekana hakuna wa kukuajiri, tubu kwa ajili ya chanzo kinachokuzuia.
✓✓Inawezekana hakuna wa kufunga ndoa na wewe,tubu kwa ajili ya chanzo kinachokuzuia.
✓✓Inawezekana kila ukifanikiwa kidogo unapata na majanga,tubu kwa ajili ya chanzo kinachokuzuia.
✓✓Inawezekana una roho ya kukataliwa,tubu kwa ajili ya chanzo kinachokuzuia.
✓✓Inawezekana unafuatiliwa na roho za mauti au uharibifu, tubu kwa ajili ya chanzo kinachokuzuia.
Ndugu, kila tatizo lako linalokutesa lina chanzo, tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo kisha omba MUNGU akutoe kwenye tatizo, tanguliza Toba ya kina na mtego wa tatizo lako utakuwa umeteguliwa na sasa utafanikiwa.
Isaya 58:9 "Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;"
Katika Maombi
1.Omba Toba kwa ajili ya makosa Yako yaliyosababisha tatizo.
2. Tubu kwa ajili ya makosa ya wazazi wako yaliyosababisha tatizo.
3. Baraka Yako iliyozuiliwa tubu kwa ajili ya kikichozuia Kisha idai Sasa kwa Maombi katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi Katika shamba la Bwana YESU KRISTO.
+255714252292
Ubarikiwe

Comments