MAOMBI MAALUMU (Day 4)

 

Na Mwl Peter Marco Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele 

Kipindi: Kuombea misingi ya utakatifu.


Kipengele: OMBA MUNGU AKUPE ROHO YA KUMCHA YEYE.


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni Kisha tuombe Maombi maalumu yanayoleta ushindi.


◼️Ipo misingi ya utakatifu ambayo ni Kumpokea YESU kama Mwokozi, Kuishi maisha ya kulifuata Neno la MUNGU, Kuongozwa na ROHO MTAKATIFU n.k


Maombi yenu leo tunaomba ili MUNGU katika KRISTO YESU atupe roho ya kumcha yeye.


✓✓Kumcha MUNGU ni kuishi maisha yanayompendeza MUNGU.


✓✓Kumcha MUNGU ni kuambatana na YESU KRISTO moyoni mwako.


✓✓Kumcha MUNGU ni kuwa na hofu ya MUNGU ndani yako ambayo hukupelekea kumheshimu MUNGU katika KRISTO YESU kwa kiwango cha juu, kumpa nafasi ya kwanza anayostahili, kumtii, kushika maagizo yake yote, kumwabudu katika ROHO MTAKATIFU, kumpa heshima na utukufu na maisha yako kuamua kumtumikia kwa moyo wa upendo.


Kumcha MUNGU ni wajibu wa kila Mteule wa KRISTO YESU ,na kadiri unavyoambatana na YESU na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU na kuishi kwa kusudi la MUNGU basi kuna Roho 7 za MUNGU na moja ya Roho hizo ni Roho ya kumcha MUNGU, hii Roho kuna wateule wanayo, hata wewe omba Leo MUNGU akupe Roho ya kumcha yeye.

Isaya 11:2-3 "Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na YA KUMCHA BWANA; na furaha yake itakuwa katika kumcha BWANA; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;"


✓✓Kwa ujumla hizi Roho saba za MUNGU ni "namna" saba za "tabia" ya utendaji kazi wa ROHO MTAKATIFU ndani yetu.

Hizo Roho saba za MUNGU sio ROHO MTAKATIFU saba bali hizo ni jinsi saba za utendaji wa ROHO MTAKATIFU yule yule.

ROHO MTAKATIFU ni mmoja tu na si vinginevyo, jina lingine ROHO MTAKATIFU anaitwa Roho wa MUNGU na pengine katika maandiko anaitwa Roho wa KRISTO, huyo ni mmoja tu.

Sasa Roho ya kumcha MUNGU ni sehemu ya utendaji wa ROHO MTAKATIFU ndani ya wateule wa KRISTO.


Hata hizo Roho 7 za MUNGU zote ziko na ROHO MTAKATIFU na ni haki ya Mteule wa KRISTO kuwa nazo akijaaliwa na MUNGU.


◼️Ukisoma hiyo Isaya 11:2-3 tunaona Mtu akiwa na Roho ya kumcha MUNGU atakuwa na sifa hizi.


1. Furaha yake itakuwa katika kumcha MUNGU.


2. Hataamua kwa kwa aonavyo kwa macho tu bali atamsikiliza ROHO MTAKATIFU ndani yake, maana huyo ana Roho ya kumcha MUNGU.


3. Hataamua kulingana na anachosikia kwa masikio yake tu bali atamsikiliza ROHO MTAKATIFU ndani yake ili kumsaidia katika maamuzi, maana mtu huyo ana Roho ya kumcha MUNGU.


Ndugu tamani sana uwe na ROHO MTAKATIFU na ukiwa naye omba upewe Roho ya kumcha MUNGU.

Hizi Roho saba za MUNGU katika Ufunuo 5:6 Biblia inasema kwamba zimetumwa duniani,

Ufunuo 5:6 "Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za MUNGU zilizotumwa katika dunia yote."


Kama Roho saba za MUNGU zimetumwa duniani kwanini usitamani wewe kuwa na ROHO wa MUNGU ambaye ni ROHO MTAKATIFU na ndiye katika yeye


 Roho Saba za MUNGU zitafanya kazi kwako?

Kwanini usiwe na Roho ya kumcha MUNGU?

Hivyo Roho saba za MUNGU zipo na zitakuwa hata kwako ukiamua kuambatana na ROHO MTAKATIFU, ndugu leo omba upewe na MUNGU Roho ya kumcha yeye ili uishi maisha matakatifu ya Wokovu siku zote huku ukimpendeza kabisa MUNGU siku zote.

Wakolosai 1:10-12 " mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa BWANA, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya MUNGU; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha;

mkimshukuru Baba(MUNGU), aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru."


Kama kuna kitu muhimu sana unahitaji ndugu basi ni kumcha MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi, omba ROHO MTAKATIFU akujalie kuwa na huo uwezo wa kumcha MUNGU daima, hiyo ndio Roho ya kumcha MUNGU.


Katika Maombi.


1. Tubia dhambi zako maovu na makosa yote.


2. Kama hujaokoka okoka kwanza  Kisha kwa Maombi mkaribishe ROHO MTAKATIFU Maisha mwako.


3. Omba roho ya Kumcha MUNGU Baba wa Mbinguni iingie ndani Yako.

MUNGU akubariki sana.

By Peter Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.

+255714252292

Ubarikiwe

Comments