MAOMBI MAALUMU (Day 9)

 

Na Mwl Peter Marco Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai 



Kipengele; MAOMBI YA KUOMBEA AFYA.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU Kisha tuombe Maombi ya ushindi.
Leo tunaombea Afya.

Afya ni nini?

◼️Afya ni hali nzuri ya mwili ya kukaa bila maradhi/Magonjwa.

Hiyo ndio maana ya afya kiroho na kimwili pia.

-Afya sio unene.
-Kuwa na ngozi laini ya mwili sio afya.
-Kula sana sio afya.

Kwanini afya ni muhimu sana kwako?

✓✓Kwa sababu afya ikiondoka magonjwa yanachukua nafasi.
Afya ni jambo la kiroho hivyo usisahau kuomba kuhusu afya.

Yeremia 30:17 "Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye."

◼️Biblia inasema kwamba MUNGU atakurudishia afya ina maana pia ya kwamba afya haikuwepo ndio maana kwa neema yake MUNGU anairudisha afya hiyo.

✓✓Sio kwamba ni mwili tu unahitaji afya, hapana, hata ndoa inahitaji afya,uchumba unahitaji kuwa na afya ndipo mtafikia hatua ya kufunga ndoa, n.k japokuwa leo Mimi nitajikita zaidi katika afya ya mwili.

Hakikisha leo unaomba maombi ya kuiita afya ndani yako, kwa familia yako, watoto wako, wazazi wako, ndugu zako, rafiki zako na watu wanaokuhusu ambao utapata msukumo kuwaombea.

◼️Kumbuka sana afya ikiondoka ujue magonjwa yanachukua nafasi mwilini.

Biblia inaposema katika Yeremia 30:17 kwamba MUNGU atairudisha afya maana yake hiyo afya ilikuwa haipo ndio maana MUNGU anairudishwa.

Kama afya ilikuwa haipo maana yake kuna aliyeichukua.

Anayeweza kuichukua afya yako hata ukawa mtu wa kuumwaumwa ni shetani na mawakala zake,hao ndio wanaweza wakaiondoa afya ndani ya mtu na kumwekea magonjwa.

Dhambi zako pia zinaweza kuondoa afya ndani yako, ndio maana Bwana YESU baadhi ya aliowaponya aliwaambia "Umesamehewa dhambi zako"
Mathayo 9:2 "Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako."

Kumbe tunagundua kwamba dhambi ndio ilikuwa chanzo cha kuumwa kwao, baada ya afya kuondoka ndani yao.

Kwa hiyo afya inaweza kuondoka ndani yako, ndani ya mtoto wako au mwenzi wako n.k kwa sababu tu ya kurogwa yaani nguvu za giza na dhambi.

Kuna watu kwa sababu ya kukosa afya ndio maana wao kila Mara wanaumwa na wengine wameweka hadi bajeti ya dawa kila wakipokea mshahara.

Ndugu, afya ni suala la kiroho, usipolishughulikia kiroho unaweza kuteseka sana.

Kuna watu wamerogwa afya zao zikaondoka, kinachofuata hapo ni magonjwa kuchezea miili yao.
Kuna watu wamefungwa vifungo vya kipepo na afya zao zikaondoa, magonjwa yanachukua nafasi.
Mimi Peter Mabula kwa kuombea watu mbalimbali na kufunuliwa kwa mafunuo juu ya kinachowasibu nimewahi kuona mambo mengi ngoja nikupe shuhuda mbili kutoka katika huduma yangu ya kuombea watu.

Baba mmoja alikuwa anaumwa kila Mara na hali ilikuwa ni mbaya, akiponishilikisha nikamuombea na kwenye ulimwengu wa roho nikaona alivikwa vazi la magonjwa nilishangaa sana. Yaani wachawi walipokuwa wanamroga walimvalisha vazi liitwalo ugonjwa, kila akienda hospitalini hakupona, lakini maombi ya kulivua vazi la magonjwa alipona.

Mtu mmoja alikuwa anaumwa muda mrefu kumbe alirushiwa mapepo ya magonjwa, akipima hospitalini hakuna ugonjwa lakini katika hali halisi anaumwa sana, tulipofanya maombi ya kung'oa hizo nguvu za giza ndani yake akapona saa ile ile.

Wachawi huwinda afya yako au ya mtu wako wa karibu, wakiiondoa hiyo afya ujue magonjwa yanachukua nafasi, na mpaka kuna watu wengi walioshindwa kumfuata YESU KRISTO Mwokozi walikufa kwa magonjwa hayo ya kichawi.

Kuna watu walirogwa na magonjwa yao yaliwaua kwa sababu hawakujua siri ya kupona kwamba ni kuufuata Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.

Nini ufanye katika maombi leo.

1. Kwa njia ya maombi ihitaji afya itokayo kwa MUNGU.

Yeremia 33:6" Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli."

Afya ya MUNGU ikiingia tu ndani yako unapona.

2. Kataa magonjwa kwa Maombi.

Zaburi 91:10" Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako."

Tauni inawakilisha magonjwa hiyo kataa magonjwa kwako, kwa familia yako, kwa mwenzi wako wa ndoa, kwa watoto wako n.k

3. YESU KRISTO anaponya magonjwa yote, hivyo mwambie akuponye kama unaumwa, aponye na watu wako wanaoumwa.

Mathayo 9:35 "Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina."
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
+255714252292
Ubarikiwe sana 

Comments