SHUHUDA MBALIMBALI KUTOKANA NA MASOMO NA MAOMBI. 
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu, hizi hapa chini ni baadhi ya shuhuda walizonitumia baadhi ya marafiki zangu kutokana na masomo yangu na maombi tuliyoomba pamoja. Sifa, heshima , adhama, ukuu na utukufu wote ni kwa MUNGU Baba wa mbinguni tu.
1. Bwana Yesu asifiwe mtumishi, Mimi ni mfuatiliaji sana wa masomo yako facebook, yananibariki sana nimewahi kukuandikia kuwa nilikuwa na changamoto kanisani yakuwa watu kuwa wapinzani kwa Idara ya wanawake(wwk) hata wazee wa kanisa, Mimi ni mwenyekiti wa wwk, tulikuwa tunajiandaa na sikukuu ya wamama Kanisani kwetu ila kulikuwa na vita kubwa na upinzani mkubwa sana hadi sikujua kama sherehe itafanyika vyema, nikakupigia simu ukaniombea na ukaniambia sikukuu inaenda kufanyika kwa kishindo na ndivyo ilivyokuwa, na sasa Mchungaji wangu kaniteua niendelee na uongozi.
2. BWANA YESU Asifiwe mtumishi . Nashukuru Mungu Binti yangu kapona lile tatizo, asante kwa maombi yako na Mungu akubariki sana Mtumishi.
3. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Hakika Mungu ametenda kupitia maombi yako mtu wa Mungu, maombi uliyonitumia usiku wa saa sita jana kwa audio whatsapp ulikamilisha ushindi wangu na Bado ukanihakikishia kuwa nimeshinda jana mchana kwa maandiko ubarikiwe sana, nilipita kwenye wakati mgumu sana moyo ulikuwa ukiuma sana lakini masomo yako kwenye google yalinipa nguvu mpya kila wakati na nikajifunza kuona tatizo limekwisha kabisa kiroho lakin kimwili bado lipo, Mungu aendelee kakutumia kwa ajili yangu na wengine zaidi, kuna wakati huwa nawaza kama Mungu asingeniletea wewe mtumwa wake sijui ningekuwa wapi maana mawakala wa shetan wangeshanishinda, ubarikiwe sana sana sana.
4. Bwana asifiwe mtumishi.
Nashukuru mtumishi kwa maombi, nilikuwa nalala sioti ndoto, nashukuru uliniombea sasa naota ndoto.
5. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Ninashukuru kuwa pamoja na wewe kupitia mtandao huu,mimi ni mtumishi wa Mungu katika kanisa la Uamsho la Makerubi. Kanisa hili lilianzia katika kambi la wakimbizi kutoka DRC na Burundi la Nyarugusu mkoa wa Kigoma,wilaya ya Kasulu.
Mimi ninafuata masomo yako unayofundisha na kurusha mtandaoni ,masomo hayo yananivutia na yananisaidia sana katika utumishi wangu. Mungu akubariki akutie nguvu kwa maono hayo makubwa ulio nayo ya kujenga mwili wa Kristo.Tutazidi kuombeana ili Mungu azidi kujifunua zaidi na zaidi katika maono hayo.
Ubarikiwe salamu kwa wote wakuzungukao ofisi mwako.
6. Bwana Yesu asifiwe mtumishi.
Mimi ni yule dada niliyekupigia kuwa nina shida katika sehemu zangu za siri zinatoa maji sana hata kama nimekaa nahisi maji yanamwagika ,yaani hata tendo la ndoa na mume wangu nilikuwa na hofu kushiriki kwani maji yanamwagika akiingia, nikawa namuona mume wangu hafurahii pia mume wangu hata hamu ya tendo la ndoa na mimi akawa hana kabisa, nilikueleza mengi kisha ukaniombea. Namshukuru Mungu tangu siku ile umeniombea nikaona tofauti ya ajabu, yaani sasa hivi najihisi mkavu kabisa yaani nikikaa hivi sisikii maji kutoka na niliposhiriki na mume wangu NIKAWA MAJI YAMEPUNGUA KABISA NA TUSEME HAYAPO ...SASA IVI NAJISIKIA MKAVU SANA SANA SANA, NAMSHUKURU SANA MUNGU, PIA MTUMISHI ULINIOMBEA KUHUSU JINI MAHABA LILILONISUMBUA SIKU NYINGI UKAFUNGA MLANGO WA NDOTO ANAOTUMIA YAANI MPAKA LEO SIJAMUOTA KABISA ,,ILE SIKU NAKUPIGIA SIKUWA NA AMANI KABISA ILA BAADA YA MAOMBI NIKAJAWA AMANI MNO ..NAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YAKO ,PIA NILIKUAMBIA NILIKUWANA TATIZO LA KUTEMBELEWA NA VITU MWILI TOKA MWAKA 2003 ULINIOMBEA SASA HIVI SIVISIKII KAMA MWANZO YANI NI KWA MBALI YANI NI KWA MBALI MNO MNO NAJUA VITATOWEKA JUMLA.
7. Bwana Yesu asifiwe milele Mtumishi. Nakusalimu katika Jina lipitalo majina yote la YESU KRISTO wa Nazareti. Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru sana MUNGU kwa ajili yako kwa kukutanishwa nawe maishani mwangu. Nakushukuru sana Mtumishi wa MUNGU kwa Maombi unayoniombea mara kwa mara. Kama tulivyoongea nilikuwa safari ambayo pia uliniombea nikiwa tayari safarini. Kabla ya safari kutokana na mazingira tuliyokuwa tunayaendea hayakuwa mazuri maana tulikuwa tunaenda ukweni, hasa nilipozingatia mume wangu ambaye tulikuwa naye safarini bado hajapata neema ya wokovu. Baadhi ya mambo huko yalikuwa ni ya uonevu kwa mume wangu naye huwa ana hasira mbaya...kwa sababu nilishafahamu hayo niliingia kwenye maombi kumweleza MUNGU kuwa nakataa hali yoyote ya kumfanya mume wangu kuwa na hasira mbaya ya kutuondolea amani..pia nilikataa kabisa kukutana na watu ambao ni adui au wabaya wetu na kila ambaye MUNGU hajapanga tukutane naye...ikiwa ni pamoja na wachawi wote, wakala wa shetani wote nikaweka mpaka kwenye ulimwengu wa roho kwa ukuta ili tusionane... niliamini MUNGU ametenda nikashukuru.
Ushuhuda :
Tulipofika nyumbani Roho Mtakatifu aliniongoza kabla ya kulala zunguka nyumba niachilie Damu ya YESU...nilifanya hivyo...nikiwa kitandani sijalala..nilikuwa nimefumba macho niliona vitu vya ajabu sura za kutisha za wanadamu si wanadamu. .majoka! Vitu vikitibuka ardhini Yaani ardhi kama vile ilikuwa inapinduliwa pinduliwa...kwa kweli yalikuwa ni mambo yanatisha....wakati nashangaa nikafumbua macho .... nilipofumba tena nikaonyeshwa hivyo hivyo .... nikaambiwa endelea kuachilia Damu ya YESU niliendelea kufanya hivyo mpaka nikapata usingizi. ..lakini katika Roho niliendelea kukesha..MUNGU alinipa ujasiri wa ajabu!
Mume wangu siku hiyo alielezwa mambo magumu ambayo kwa kawaida kibinadamu huwezi kuvumilia bila uwezo wa MUNGU lakini alivumilia na kumkiri MUNGU ndiyo mwamuzi wake...bila hasira yoyote. ..kwa kweli nilimuona MUNGU hapa. .amedhulimiwa Kiwanja, mashamba mawilina fedha taslimu milioni kumi...
Wakati tunarudi nikiwa njiani nilidondosha simu yangu ya Android SAMSUNG. Nilipogundua sina simu...nikamwambia mume wangu simu yangu imepotea ...akapiga akasikia inaita moyoni sikuwa na mashaka...nilimwambia YESU simu yangu isipotee kwa sababu kupitia hiyo simu nakutumikia kwa kusoma Neno lako na kupata maarifa...nikamwambia YESU malaika wapo kwa ajili ya kutuhudumia wamsake huyo aliyechukua simu yangu anirudishie. wakati anaendelea kupiga akapokea aliyeiokota... akamwambia ni kweli simu ameokota na kwa wakati huo alikuwa ameshafika mbali sana yaani mji mwingine kutoka tulipokua.... ilibidi tumuombe arudi tutamrudishia gharama, akasema Sawa. Tulisubiri zaidi ya masaa mawili lakini hakutokea. ..mimi niko naendelea kuomba...ghafla akatokea mtu mhitaji mwenye njaa akatuomba sh. Elfu moja ili akale chakula. .. mwenzangu akamwambia hapa tulipo usituone hivi tuna shida! Mhitaji akasisitiza nipe tu hata sh mia tano akaongeza akasema Neno la MUNGU linatuambia tusaidiane. ..niliangalia kwenye pochi yangu mume wangu akaniambia una mia tano? Nikampa sh elfu moja. ...alishukuru sana na kutuombea baraka za MUNGU ziambatane nasi...nilishuhudiwa ndani yangu kuwa yule hakuwa mtu wa kawaida.....basi tuliendelea kumtafuta yule aliyeokota simu mume wangu akaniambia ongea naye nimechoka huyu anatudanganya....nikaongea naye akaniambia ameshafika eneo hilo... baada ya dakika tano akaja tulipokuwa akatusalimia akatuambia mimi ndiye niliyeokota simu... akanipa simu yangu ikiwa salama kabisa. ..nami nilimpa hela kidogo kama shukrani kwake na gharama aliyotumia kurudi. NILIMUONA YESU!
Pia katika kumuomba MUNGU simu yangu irudishwe pamoja na kumuambia kuwa hiyo simu inanisaidia katika kumtumikia na kusoma Neno lake na kupata maarifa. Vile vile nilimkumbusha MUNGU kuwa ninamtolea sadaka, zaka (fungu la kumi) na dhabihu...nikamwambia ahadi alizotuahidi katika Malaki 3:....
Namshukuru sana MUNGU maana simu yangu nilipata na safari ilikuwa njema.

Comments