![]() |
Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu.
Hili ni sehemu ya somo la kitabu ninaloliandaa linaloitwa SILAHA ZA MAOMBI YA VITA ZA KIMAANDIKO.
Kwa sababu ya kuharibika laptop yangu ninatoitumia kuandalia masomo, ngoja nikupe maarifa machache kwa simu ili upate kitu cha kuombea leo kwenye maombi yako. Ukipenda kuninunua laptop yeyote kwa ajili ya kuandalia Neno la MUNGU nitafurahi sana na MUNGU hatakuacha.
◼️Giza la ki MUNGU ni silaha mojawapo ya kiroho unayoweza kuitumia wewe Mteule wa KRISTO ili kuwashinda mawakala wa kuzimu wanaokufuatilia.
Kuna mfano kadhaa katika Biblia ambapo Giza la MUNGU likitumika kama silaha ya kiroho.
Tuone mfano hai ambapo giza kama silaha ya kiroho kwa wateule wa MUNGU ilivyofanya kazi ili kuwafedhehesha maadui za Watu wa MUNGU.
Kutoka 10:21-23 " BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. Basi Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri muda wa siku tatu; hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao."
✓✓Musa alitumia giza katika vita ya kiroho na maadui ambao ni wamisri hawakufanya chochote siku tatu.
Giza hili ni la MUNGU na ni Giza la ajabu sana maana katika Nchi Moja ya Misri kulikuwa na Wamisri na Waisraeli ajabu kwa Wamisri kulikuwa giza kiasi Mtu hawezi kumuona Mtu Mwingine yeyote lakini wakati huo huo Waisraeli wanaonana na kwako hakuna hilo giza ingawa wote walikuwa Misri.
Giza la ki MUNGU sio kama giza unaliliona wewe, giza hili la kawaida la usiku majini na Mawakala wa Shetani wanaona kama mchana.
◼️Giza la ki MUNGU linalitumika kama silaha ya Watu wa MUNGU dhidi ya nguvu za giza ni giza la rohoni ambalo kiumbe wa kiroho linamfanya asione katika hali yake ile ile ya kiroho.
✓✓Yaani unaweza ukaliamuru giza liwafunike wachawi wote wanaokuwinda na watashangaa hawakuoni, hawaioni nyumba yako na ni wao ndio wamefunikiwa na giza hilo.
✓✓Wamisri kwa siku 3 hawakufanya chochote dhidi ya Waisraeli maana giza la MUNGU lililotokana na maombi ya Musa likiwafunika wamisri, giza hilo huwafunika mawakaka wa shetani tu.
✓✓Mfano Mwingine ni yule mchawi Elima ambaye alikutana na Giza la MUNGU lililomfanya kuwa kipofu kwa muda ili asizuie Injili ya KRISTO YESU kwenda mbele.
Matendo 13:11-12 " Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya BWANA."
✓✓Huyu mchawi giza la MUNGU likimpata ghafla tu baada ya Maombi ya Mtume Paulo.
✓✓Unakumbuka tukio la giza nchi yote wakati Bwana YESU KRISTO Yuko msalabani?
Mathayo 27:45 "Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa."
✓✓Hii Ina maana MUNGU anaweza kutumia chochote kwa kusudi lake.
◼️Hivyo Giza ya MUNGU inaweza kuwazuia mawakala wa shetani wasikufanye lolote hata kama Wana nguvu kubwa kiasi gani.
◼️ Bwana YESU KRISTO unaweza kuomba katika Jina lake na Giza la MUNGU likawafunika wachawi na majini hata wasifanikiwe kukuonea popote.
✓✓Musa aliomba giza liwapate wamisri kwa siku tatu, wewe unaweza ukaomba kwamba giza la MUNGU liwafunike majini wote, wachawi wote, wakuu wa giza na kila mwanadamu anayetumika kipepo dhidi yako au kuvaa umbo la kiroho ili alete madhara kwako.
✓✓Amuru leo mawakala wa shetani wote wanaokuwinda, wanaowinda ndoa yako, uchumba wako, mwili wako, watoto wako, kazi yako, uchumi wako na kila baraka yako, amuru giza la MUNGU liwavae wasikuone kamwe, amuru njia yao ya kuna kwako iwe giza na utelezi, wasifanikiwe kamwe kukufikia.
Zaburi 35:6 "Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia."
Kwa Maombi Inawezekana hakika.
Ndio maana andiko la Zaburi 35 hapo juu linaonyesha Daudi akiomba giza la MUNGU liwe katika njia za adui zake na ikawa hivyo katika Jina la YESU KRISTO.
Inawezekana bado hujaelewa kama ambavyo Mimi Peter Mabula nataka uelewe.
Giza ni nini?
✓✓Giza ni hali ya kutokujua kitu.
◼️Sasa unapoita giza la MUNGU na giza hilo likawapata mawakala wa shetani maana yake hao hawatajua kitu kuhusu wewe, hawatakufikia maana hawajui uliko, hawataifikia familia yako au nyumba yako maana hawajui iliko kwa sababu ya giza la MUNGU lililowafunika.
Kumbuka giza hili ni silaha ya kiroho ya kimaandiko ya vita vya kiroho hivyo giza hilo huwapata mawakala wa shetani tu na sio Watu wa MUNGU
Nini ufanye katika Maombi?
1. Tubu dhambi zako zote na kuziacha, tubu kwa kilichosababisha uonewe na nguvu za giza.
Isaya 59:1-2 " Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."
2. Kama nguvu za giza ziko ndani yako ziamuru ziondoke ndani yako na mkaribishe Bwana YESU KRISTO ndani Yako, maana aliko YESU hakuna giza.
Yohana 8:12 "Basi YESU akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima."
3. Funga milango ya kiroho iliyokuwa imefunguliwa ili nguvu za giza ziingie kwako, iwe mwilini,kwenye ndoa, kwenye familia n.k
Mathayo 18:18 "Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."
4. Tumia giza la MUNGU kuwafunika mawakala wa shetani ili wasikutese tena, wataje katika maombi yako ili giza liwapate.
Zaburi 69:23 Macho yao yatiwe giza wasione, Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
5. Amuru kila njia ambazo huwa wanazitumia kuja kwako, hizo njia ziwe giza na utelezi huku malaika wa MUNGU akiwaangusha chini.
Zaburi 35:6 "Njia yao na iwe giza na utelezi, Malaika wa BWANA akiwafuatia."
6. Amuru giza la MUNGU kwenye vikao vyao na madhabahu zao.
Zaburi 105:28 "Alituma giza, kukafunga giza, Wala hawakuyaasi maneno yake."
7. Amuru silaha zao nazo giza lizipate, zisikuone.
Isaya 54:17 "Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA."
8. Mshukuru MUNGU kwa ushindi mkuu aliokupa.
2 Samweli 22:50 "Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako."
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ni namba hii kupiga, sadaka ya kuipeleka Injili,kuandika meseji na whatsapp).
Ubarikiwe sana.
Comments