KUNA NENO NI KWA AJILI YAKO USILIKWEPE, JIFUNZE KUPITIA USHUHUDA HUU.

 

Na Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Huu ni Ushuhuda wa  Mwanamke mmoja siku moja alinitembelea Kanisani ili nimuombee MUNGU amtoe katika mikataba ya kishetani aliyokuwa ameingia, na mikataba hiyo ya kishetani ilikuwa imemletea vifungo vingi na magonjwa ya ajabu ajabu.

 ◾Nakumbuka siku hiyo anakuja Kanisani kwetu ilikuwa katika ibada ya jumatano jioni.

◾Tukamuombea kisha akaondoka, baada ya siku kadhaa akaniambia kwamba yuko huru sasa, magonjwa amepona na majini yaliyokuwa yanamtesa kila siku usiku hayakuja tena, kisha akaniambia maneno haya hapa chini, nayaleta kama yalivyo.

◼️ " Mtumishi Peter Mabula unajua kama wewe ulikuwa ndiye mtu niliyekuwa nakuchukia kuliko watu wote mtandaoni? 
Maana hata sikujua ilitokeaje ukawa rafiki yangu Facebook mwaka 2015, baada ya wewe kuwa rafiki yangu nilianza kukutana kila siku na masomo yako ambayo sikuyahitaji na yalinifanya nikuchukie, kila siku naona masomo yako yakinionya na nikisoma kidogo naumia, baadae nikawa sisomi nikiona tu somo umepost wewe,  lakini masomo mengine nilijikuta nasoma kidogo, masomo yalipozidi sana ndio nikawa nakuchukia zaidi, nikaamua kuku unfriend hivyo masomo yako nikawa siyaoni.

Baada ya kama mwaka mmoja na nusu bila kuona masomo yako nikashangaa siku moja naona somo zuri la Maombi kwenye group nikaanza kusoma bila kuangalia kapost nani. Nilipomaliza kusoma nashangaa naona jina lako, kumbe nilikublock lakini tulikuwa wote group Fulani la Facebook.

Nililia siku hiyo ila kwa sababu nilikuwa nahitaji msaada ilibidi nikague profile yako ili nione umeandika nini, niliona mambo mengi ya kunionya, kunielimisha na kunisaidia.

Baadae vita na nguvu za giza ikawa kubwa sana kwangu, wachawi wakawa wananiijia live usiku na wanasema ndani ya mwezi mmoja watakuwa wameshaniua, na kwa maagano niliyoingia nao hakuna wa kunifungua. Niliamua kuokoka lakini kila ninakoenda kusali najikuta tu nawachukia ghafla watu wa Kanisani pale kuanzia na Mchungaji, hata kama hawakunikosea lolote.

 Nilizunguka makanisa mengi hali ikiwa ni hiyo hiyo.
Nikaamua kutokwenda Kanisani.

 Baada ya muda nikaota ndoto ninazikwa yaani naona live nakufa na watu wanalia. Kiukweli niliogopa na kuwa kama nimechanganyikiwa, nikamua kuwa naomba nikitumia masomo yako, hali ikawa inapungua kidogo lakini haikuisha, siku moja nikaota ndoto niko sehemu nataka kuzama kwenye maji na watu wote wakanikimbia ghafla nikakuona wewe ukiwa na watu wawili ukanitoa kwenye maji yale ambayo nilikuwa nimebakiza kichwa tu kuzama. Kwa njia hiyo nikagundua kabisa kwamba unaweza kunisaidia ili nitoke katika mikataba ya giza ndio maana nikaja Kanisani ili uniombee"

◼️Baada ya ndugu huyo kuniambia hayo nilijiuliza sana.

✓✓Wapo watu hulidharau Neno la MUNGU la kuwasaidia na kuwatoa katika maangamizo.

✓✓Wako watu huwachukia Watumishi wa Bwana YESU ambao wanaweza kuwasaidia kiroho na wakashinda.

◼️MUNGU ana watumishi wake wengi sana kwa ajili ya kuwafanya watu kufunguliwa vifungo na kutubu.

✓✓Inawezekana hata wewe ndugu unayesoma ujumbe huu huwa unamdharau Mchungaji wako.

◼️Naomba Jifunze kwa watu wa Ninawi ambao walipohubiria Neno la MUNGU ambalo walikuwa hawalitaki walitii na kuepuka maangamizo ya MUNGU.

Yona 3:3-5 " Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama BWANA alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamsadiki MUNGU; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.

✓✓Inawezekana ni wewe huwa ukiwaona wainjilisti wanahubiri mitaani unashiriki kuwatukana na kuwasema vibaya.

Ndugu, Jifunze kwa Wakwe za Lutu ambao Lutu aliwahibiria Neno la MUNGU kwamba waondoke Sodoma wasije wakaangamia, wao wakashupaza shingo wakawa wamamuona Lutu kama Mtu anayecheza ngoma kesho yake  wakaangamia.

Mwanzo 19:14 "Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze."

✓✓Inawezekana ni wewe kuna Mtumishi huwa anakusihi sana uache dhambi na maovu lakini unamtukana.

◼️Ndugu, geuka Leo, Mpokee YESU KRISTO kwa upya na Acha Dhambi zote.

◼️Kumbuka YESU KRISTO alikuja kwa ajili Yako na yangu, Ndugu zingatia Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.

Yohana 3:17-18 " Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

◼️Ndugu, kuna watumishi katika eneo lako inawezekana wamebeba msaada wako kiroho, au kuna Watumishi wanaweza kuja katika eneo lako na kumbe ni kwa ajili ya kufunguliwa kwako.

Zingatia Neno la KRISTO wanalofundisha utaitwa heri.

Mithali 1:33 "Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya."

✓✓Kuna Mtumishi inawezekana huwa unamdharau ukiona masomo yake na kumbe huyo amebeba kufunguliwa kwako.

✓✓Ndugu, kama ulikuwa hujui ni kwamba MUNGU hulituma neno kwako ili upone na kufunguliwa.

◼️Neno hilo huwa nalijileti Bali linaletwa na watumishi wa YESU KRISTO.

✓✓Inawezekana umeomba sana bila mafanikio lakini kumbe MUNGU ameshakuletea Mtumishi wake mwenye Neno, kitendo cha wewe kumpuuzia Mtumishi huyo utajikuta unabaki na kifungo chako.

◼️MUNGU hulituma Neno kwa ajili yako, ndugu uwe unalipokea Neno la kweli la MUNGU.

Zaburi 107:20-22 " Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba."
Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana 

Comments