NDOTO ZA KUSAFIRI NA NDOTO ZA SHULE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.

Rafiki yangu mmoja aliuliza maana ya ndoto hizi mbili, aliuliza kwa ufupi hata iwe rahisi kupata maana Kibiblia, alisema

◾"Shalom mtumishi, Bwana Yesu apewe sifa mimi ni binti na nimekuwa nikikufatilia masomo yako, nipo katika mahusiano lakini nimekuwa nikiota ndoto nasafiri lakini sifiki Mahali nakwenda na ndoto zimekua zikijirudia lakini.
Kuna siku nilikuwa nasoma masomo yako mara nikakutana na shuhuda hii Kuna binti alikuwa na mahusiano ya uchumba yanavunjika aliota anafanya mtihani lakini hajamaliza hapohapo nikaanza kufikiria ndoto zangu nilizokuwa naota imepita siku kadhaa nimeota nafanya mtihani lakini wenzangu wapo darasani wamekusanya pepa lakini mimi nipo na mtihan nje sijamaliza sjui nini maana ya ndoto hizi mtumishi tafadhali."

◾Majibu yangu Mimi Peter Mabula yalikuwa Haya.

◼️Kuhusu Ndoto za kusafiri muda mrefu bila kufika.

✓✓Kuota unasafiri muda mrefu sana na hufiki mwisho wa safari hiyo maana yake kuna baraka yako fulani imecheleweshwa kufika.

✓✓Inaweza kucheleweshwa  na MUNGU ingawa ni mara chache sana, ila zaidi ya asilimia 90 baraka hiyo hucheleweshwa na nguvu za giza au wewe mwenyewe kwa sababu ya dhambi au kutokujielewa.

Ngoja nikupe wa MUNGU kuchelewesha .

◼️Kwa sababu ya kuabudu sanamu safari ya Waisraeli kutoka Misri hadi Kaanani ilicheweshwa na MUNGU mwenyewe kwa sababu ya dhambi zao.

Hesabu 14:33-34 " Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani. Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu."

✓✓Safari hii ingechukua wiki moja kufika lakini ilichukua miaka 40 kwa sababu ya dhambi, dhambi ilitengeneza adhabu.

✓✓Uwe makini kama hupati baraka yako kwa sababu hiyo, kama ni hivyo tubu kwa MUNGU na ujitenge mbali na dhambi.

◼️Unaweza kuota unasafiri muda mrefu sana bila kufika kumbe unajulishwa Dhambi au makosa Yako yanachelewesha kufika kwako.

◼️Kuhusu nguvu za giza na mawakala wa shetani Biblia inasema shetani akija mahali ni ili kuiba, kuua na kuharibu Yohana 10:10a " Mwivi(shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;"

◼️Sasa shetani huwakilisha nguvu zote za giza, mawakala wa kuzimu na hata wanadamu wanaotumika kipepo, na kazi yao ni kuiba yaani yaani wanaweza kuiba hata baraka yako ndio maana ukajiona unasafiri bila kufika.
✓✓wanaweza wakaua uchumba ili uchelewe kufika katika safari yako ya kuingia katika Ndoa.

✓✓ wanaweza kuharibu uchumi ili usifike katika safari yako ya kufanikiwa kimaisha.

Kwa ujumla kuota unasafiri na haufiki baadhi tu ya sababu za kucheleweshwa huko ni hizi:

1. Safari inaweza ikacheleweshwa na dhambi kama unafanya dhambi, mfano kama unafanya ngono na mchumba wako ujue ataishia kukuacha hivyo safari yako ya kuingia katika ndoa ikawa haifiki kuanzia kwenye ulimwengu wa roho ulikoona ndotoni hadi kwenye ulimwengu wa mwili, yaani haitatokea maana shetani mmempa nafasi ili awafunge vifungo na kuwachelewesha.

2. Safari inaweza kucheleweshwa kwa kurogwa kama ulirogwa.

3. Safari inaweza kucheleweshwa kama sio kusudi la MUNGU.

4. Safari Inaweza kucheleweshwa kama kuna roho za kipepo za kufuatilia na Wewe hauko vizuri na YESU KRISTO hata uombe na kushinda.

5. Safari Inaweza kucheleweshwa kama una vifungo vya giza, mfano laana, mapepo, maagano, kupelekwa kwa mganga n.k

Nini ufanye ili ufanikiwe kuipata baraka yako.

1. Mche MUNGU kwa kutengeneza maisha yako na Bwana KRISTO YESU.

Mathayo 11:28 " Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."

2. Tubu dhambi na kuziacha zinazosababisha usifikie baraka yako.

Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"

3. Uwe mtu wa maombi katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi.

Mathayo 7:7 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"

4. Haribu kila nguvu ya giza iliyotumwa kukuchelewesha au kukuharibia ili usifanikiwe.

Kumbu 12:3 "nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."

5. Jitamkie mema huku ukikaa katika kusudi la MUNGU.

✓✓Kumbuka Ukijitamkia mabaya yanaweza kukufunga.

Mithali 6:2 "Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,"

6. Mjue adui yako na pambana naye kimaombi na vitendo utamshinda.

Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

◼️Adui yako anaweza kuwa dhambi mfano uasherati, adui yako anaweza kuwa wachawi, maagano ya giza, kafara zilizotolewa, kuwekewa nguvu za Giza ndani yako n.k

7. Acha tabia mbaya kama zipo.

Zaburi 34:14 "Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie."

◼️Kuhusu Ndoto za shule zina mojawapo ya hii maana hapa chini.

Kuota uko shule ina maana zifuatazo kulingana na ulivyoona.

1. Kuota ndoto uko Shule hata kama ulishamaliza shule tafsiri yake ni uhitaji wa maarifa fulani ambayo yanatakiwa yakutoe sehemu moja na kukupeleka sehemu nyingine bora zaidi.

✓✓Yaani kuna maarifa ya Neno la MUNGU unahitaji ili uvuke hatua uliyopo.

Mithali 12:1 " Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama. mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA."

2. Kuota ndoto uko darasa ambalo umeshavuka kwa jinsi ya mwili maana yake kufikiri kwako kuko chini ya kiwango MUNGU anachotegemea.

 mfano hai ni mtu umeshamaliza chuo kikuu lakini kila mara unaota uko shule ya msingi.

✓✓Maana yake kiwango chako cha kufikiri vyema ni cha chini sana.

Waebrania 5:12 " Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya MUNGU; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu."

✓✓Kwa maana nyingine unapoota uko darasa ambalo ulishalipitia siku nyingi maana yake umekwama kufikiri, wewe ni mchanga kiroho,hufikiri vyema yaani inavyotakiwa, unahitaji sana kujifunza Neno la MUNGU.

✓✓Au fikra zako zimekamatwa na shetani.

3. Kuota umeyarudia maisha ya utotoni au shule ya msingi au sekondari wakati ulihitimu huko zamani maana yake unafuatiliwa na roho ya kuanguka, pia hii ni dalili ya kufungwa na roho za mizimu au roho za kurithi za mababu.

4. Kuota uko shuleni maana yake nyingine ni hii. 
Kuna eneo umekwama katika maisha yako Unamhitaji sana YESU KRISTO kwenye Maombi ili uvuke.

5. Kuota uko shule maana yake katika hatua Fulani ya ki maisha unayoiendea unahitaji maandalizi ya kutosha.

6. Kuota upo darasani au mazingira ya shule ambayo ulishavuka, maana yake katika maisha yako, kuna eneo bado hujaivuka kimaisha. 

✓✓Mahali ulipo sipo unapotakiwa uwepo, kinachohitajika ni kujifunza sana Neno la MUNGU na kumsikiliza ROHO MTAKATIFU.

7. Kuota uko shule maana yako uko chini kiviwango vya kiroho.

◼️Ndugu hakikisha unajifunza Biblia na Neno la MUNGU litakusaidia kujua pia maana ya ndoto yako.

✓✓Ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa YESU KRISTO na hakikisha sana unaenda katika ROHO MTAKATIFU.

◼️Kama umeokoka na hauhusiki na baadhi ya makosa au baadhi ya vifungo nilivyoeleza basi omba kulingana na baadhi ya vipengele unavyohisi unahusika ili MUNGU akusaidie.

◼️Kama hujaokoka hakikisha kwanza unampokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.

✓✓✓✓Uzuri wa Ndoto za shule ni kwamba ukishinda tu kiroho juu ya jambo husika na ndoto hizo zinakoma, Ukiona linaendelea kila baada ya wiki kazaa au miezi kadhaa au Miaka kadhaa ujue bado hujashinda eneo hilo.

Zingatia  na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292( Kwa Sadaka ya kuipeleka Injili mbele, Whatsapp n.k)

N:B Naomba ujifunze kitu na wewe kama utakiona hicho cha kujifunza kutoka kwenye hizi ndoto 2 nilizoulizwa.
Pia huwa pia sipendi sana kujibu kila ndoto ya kila mtu ila namwambia tu aombe maana watu wanaota ndoto kila siku hivyo ukimjibu mtu ndoto yake Leo ujue na kesho atakuuliza, maana ataota tena, sasa wakiwa Watu 200 na kila siku wanakuuliza maana ya ndoto zao mpya walizoota utaweza kuwajibu? Unaweza hata ukasahau Neno la MUNGU ukikazania tu ndoto, kwa jinsi hiyo mnisamehe tu wale ambao mmewahi kuniuliza ndoto na sikuwajibu, huwa natamani kujibu ndoto ambayo nina uhakika nayo tu na iwe ndoto ambayo itawasaidie na wengine kujua maana yake , mnisamehe maana watu ni wengi mno na mimi binafsi huwa nina majukumu mengi sana sana na kazi yangu ni kuomba ili ROHO MTAKATIFU anipe Neno la MUNGU la kuwafundisha watu katika kusudi la MUNGU, hiyo ndio kazi muhimu kuliko zote. 
Nimesema hayo kwa sababu baadhi ya watu hulaumu kwanini siwajibu ndoto zao.
Mbarikiwe sana wote.

Comments