![]() |
| Na mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe.
Haya ni Maombi ya adui katika ulimwengu wa roho au wa mwili Maombi ni haya hapa chini.
✓✓MUNGU ataniokoa dhidi Yako adui yangu hata kama una Nguvu sana.
2 Samweli 22:18 "Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia; Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
✓✓Adui yangu, kwa sababu Mimi nina YESU KRISTO kama Mwokozi wangu Wewe hutafanikiwa mipango Yako mibaya dhidi yangu.
Ayubu 27:7 "Adui yangu na awe kama huyo mwovu, Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki."
✓✓Adui yangu, hata kama unanichukia sana MUNGU ataniokoa dhidi Yako katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu.
Zaburi 18:17 "Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi."
✓✓Adui yangu, Wala usifurahi juu yangu unapoona nimekwama au nimeanguka maana nitasimama Tena katika Jina la YESU KRISTO.
Mika 7:8 "Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu."
◼️Kama ulidhani Ndoa au afya yangu haitasimama, nakuhakikishia itasimama kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
◼️Kama adui unadhani kazi yangu au biashara yangu haitasimama nakutangazia Leo katika Jina la YESU KRISTO itasimama upya.
✓✓Adui yangu, chochote chema changu unachodhani hakitasimama nakutangazia kitasimama Tena kwa Jina YESU KRISTO Mwokozi wangu aliye hai.
Katika Jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Amen Amen Amen Amen
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments