![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana atukuzwe Ndugu zangu wote.
Nisikilize na unielewe.
Baada ya kuokoka December 2008 nilianza kujifunza Biblia mwenyewe kwa kuisoma Neno kwa Neno na mstari kwa mstari bila kuruka hata Neno Moja.
Awamu ya kwanza niliisoma Biblia nzima kwa muda wa miezi 8 nikaimaliza yote.
Baada ya hapo nikakaa Mwaka mmoja na nusu nikaanza Tena kuisoma Biblia Neno kwa Neno na ajabu Neno la MUNGU lile lile likawa jipya Kama sijawahi kulisoma, nikagundua ni kwa sababu Neno la MUNGU Lina pumzi ya MUNGU ndani yake hivyo ni jipya Kila leo.
Sasa wakati wa kuisoma Biblia awamu ya kwanza na awamu ya pili baadhi ya maandiko niliyawekea alama mfano ni hapo kwenye picha.
Lengo la kuweka alama ni ili nifanyie kazi, ili nizingatie zaidi kuliko maandiko mengine kwa wakati huo, ili nikaulize kwa Mchungaji kwa sababu sikuelewa andiko, ili niwe na Neno la MUNGU la kufundishia ikitokea nafasi maana nilikuwa muoga sana kufundisha Neno la MUNGU, ili nilifanye andiko hilo kuwa langu kama linazungumza mambo mema, ili nijue kama andiko hilo nimeshalisoma n.k
Baada ya miaka mingi sana kupitia imefika 2025 ROHO MTAKATIFU akanisemesha juu ya maandiko ambayo wakati nayasoma niliyawekea alama kwa kuchora mistari, akanisemesha kwamba maandiko hayo nitumie kuandaa masomo ya kufundisha mwaka 2026.
Ni miaka 16 imepita tangu niweke alama katika Biblia yangu ya kujifunzia Neno la MUNGU maana ninazo Biblia 4 ambapo Biblia zingine siweki alama ila hiyo Moja tu niliiweka alama.
Na Biblia niliyoiweka alama maandiko ni Biblia yangu ya kwanza kumiliki ambayo pia sikuinunua Mimi Bali nilipewa na Mama yangu Mdogo Judith Mabula July 2008, ni baada ya Mimi kuondoka Nyumbani Mwanza na kwenda kuanza Maisha ya peke yangu Zanzibar.
Rafiki yangu unayesoma ujumbe huu Mimi Peter Mabula nilimshangaa sana MUNGU wa Mbinguni kwa jambo ambalo nililifanya miaka 16 iliyopita na MUNGU akanisemesha kwa ajili ya 2026, kwangu ni Muujiza wa MUNGU.
Naamini kila mmoja atajifunza Neno la MUNGU Mwaka huu na atalizingatia maana ni Neno la MUNGU la baraka, maonyo, ushauri, maelekezo, Maarifa ya kiroho, elimu na Ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.
◼️Siku zote Neno la MUNGU liko hai na Lina Nguvu daima.
Waebrania 4:12-13" Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu."
◼️Kila anayependa Neno la MUNGU la Biblia takatifu anakuwa amechagua kupenda maarifa sahihi.
Mithali 12:1 "Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama."
Karibu sana 2026 kwa ajili ya Neno la MUNGU na Mtumishi Peter Mabula.
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292
Ubarikiwe sana.

Comments