![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Kanisa la MUNGU Jina lingine linaitwa Kanisa la KRISTO YESU.
1 Wakorintho 10:32 "Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la MUNGU,"
Mathayo 16:18 "Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."
◼️Kanisa la MUNGU ni watu waliompokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao Kisha wanaishi Maisha matakatifu ya Wokovu.
Yohana 1:13 "waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."
✓✓Kanisa la KRISTO wakati Mwingine linaweza likapitia upinzani mkubwa, kupitia wakati mgumu, adha, kuteswa, kuchukizwa, kutengeneza n.k
Mfano ni huu
Matendo 8:1 "Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume."
Nakuletea maadui 5 wabaya zaidi kwa Kanisa kulingana na maandiko matakatifu.
1. Wanadamu wenye roho mbaya juu ya Kanisa la KRISTO.
Matendo 8:3 "Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani."
Wapo watu wana chuki binafsi juu ya Kanisa, andiko hapo juu linaonyesha Paulo wakati hajaokoka alikuwa na chuki binafsi kwa ajili ya Kanisa.
Watu wa aina hiyo ni maadui mabaya wa Kanisa.
Mtu wa namna hii namna ya kumshinda ni kuzidi kutenda mema.
1 Petro 2:15" Kwa sababu ndiyo mapenzi ya MUNGU, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;"
2. Viongozi wa serikali za Duniani wasio na hofu ya MUNGU wa Kanisa.
Matendo 12:1-5 " Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.
Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba MUNGU kwa juhudi kwa ajili yake."
◼️Katika historia ya Kanisa ni mara nyingi Kanisa limepitia vita na viongozi wa kiserikali mfano wa Herode.
Vita na watu wa namna hii ni maadui wabaya sana sana maana watu hao wana majeshi, hao ni maadui mabaya.
◼️Katika nchi Yako au mji uliopo Ukiona Kanisa Lina vita na serikali ujue ni vita mbaya.
✓✓Kuwashinda maadui wa namna hii kuomba kwa MUNGU katika KRISTO YESU.
3. Washirika waleta fitina Kanisani
1 Wakorintho 11:16 "Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya MUNGU."
Fitina ni Nini?
Fitina ni maneno ya kuchonganisha watu; maneno ya kuleta ugomvi baina ya watu, maneno ya kuwafanya watu wasielewane.
Aikiwemo katika Kanisa mwenye tabia hizi huyo ni adui mbaya sana.
◼️Kama Kanisa jitengeni mbali ni Mtu wa namna hii maana ni adui mbaya sana kwa Kanisa.
Tito 3:10 "Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;"
4. Mtu mbaya mwenye Lengo la kuwatoa watu Kanisani.
3 Yohana 1:10 Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa."
Watu hawa ni wabaya sana, unahitajika ukali wa kiroho ili kuwanyamazisha maana wengi wao huwa ni mawakala wa shetani wanaotumia Nguvu za giza.
Paulo alipogundua Mtu anayetaka kuwatoa watu wema kwa YESU alikuwa mkali sana ndivyo wanavyotakiwa kufanyiwa watu wa namna hiyo.
Matendo ya Mitume 13:8-11 " Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa ROHO MTAKATIFU, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza."
5. Shetani na mawakala zake.
Waefeso 6:12-13 " Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama."
Mawakala wa shetani ni wachawi wote, waganga wa kienyeji, mizimu wote, Majini wote na Wanadamu wote wanautumika kishetani.
◼️Hao kuwashinda ni kupambana nao kiroho mtawashinda.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments