![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Pokea maarifa haya ya kimaombi Kisha Tumia maandiko haya kwenye Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Miujiza.
1. MUNGU wa Mbinguni akulinde dhidi ya mabaya yote ili yasifanikiwe kwako.
Zaburi 121:7 "BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako."
2. Bwana YESU KRISTO akulinde ili usinaswe na adui yeyote katika ulimwengu wa roho.
Mithali 3:26 "Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe."
3. MUNGU wa Mbinguni akulinde katika safari zako zote za Kila siku kwa mwaka mzima.
Zaburi 121:8 "BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele."
4. MUNGU wa Mbinguni akulinde ili uwe salama.
Zaburi 4:8 "Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama."
5. Malaika wa MUNGU wahusike na Wewe uliye na YESU KRISTO ili uwe salama daima.
Kutoka 23:20 "Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea."
Omba katika Jina la YESU KRISTO itakuwa.
Mithali 18:10 "Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments