![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
MUNGU anaweza kukusaidia.
Neno "Kusaidia" Lina maana hizi.
◼️Kusaidia ni kuweka kitu kinachoondoa shida au tatizo.
◼️Kusaidia ni kutoa msaada utakaowezesha kuondoa changamoto au tatizo.
✓✓Sasa habari njema ni kwamba MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kukusaidia.
Isaya 41:13 "Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia."
Mimi sijui tatizo lako ni nini ila MUNGU wa Mbinguni alishawahi kuwasaidia watu wasiuawe na hawakufa, alishawahi kuwasaidia wagonjwa walioambiwa hawatapona ila yeye alipoingiza msaada wake walipona.
Wako watu waliambiwa hawataolewa au hawatazaa lakini MUNGU aliwapa Ndoa njema na watoto walio bora.
Naipenda Biblia takatifu maana ndani yake MUNGU anaahidi kutusaidia wakati wowote tutakapohitaji msaada wake sisi wateule wake katika KRISTO YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Waebrania 13:6" Hata twathubutu kusema, BWANA ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?"
Mimi Peter Mabula niliwahi kupata ajali ambayo madaktari walisema sitapona ila Bwana YESU KRISTO akanitokea na kuniponya ghafla hadi siku natoka hospital madaktari walishangaa wakisema hawajawahi kuona mgonjwa kama nilivyokuwa Mimi amepona tena ndani ya siku 6 tu na siku ya 7 nikatoka hospital.
Ndugu hakuna ujanja wowote ila ni MUNGU tu katika KRISTO YESU alinisaidia.
Ipo Neema ya MUNGU ya msaada wa ajabu katika KRISTO YESU.
Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."
✔️Ndugu, kwa taarifa Yako wapo watu waliosaidiwa na MUNGU katika huduma zao, Ndoa zao na biashara zao ndio maana wakafanikiwa.
✔️Wako watu waliosaidiwa na MUNGU kuwashinda wachawi, waganga, mizimu majini na Kila Nguvu za giza.
✔️Hata Wewe Ndugu mwamini Bwana YESU KRISTO na omba msaada wake katika hitaji lako utafanikiwa.
Ndugu kama ulikuwa hujui ni kwamba MUNGU kupitia ROHO MTAKATIFU katika KRISTO YESU anaweza kukusaidia katika mambo magumu yote.
Warumi 8:26 "Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa."
Kwa namna gani MUNGU katika KRISTO YESU anaweza kukusaidia?
1. Ishi Maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO.
2 Nyakati 7:14 "ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao."
2. Mwamini MUNGU anaweza kukusaidia na omba akusaidie Ukitaja ni katika jambo gani akusaidie.
Isaya 41:10 ''usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu."
3. Uhitaji msaada wa MUNGU kwa Imani na utarajie maana utakuja kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
Isaya 50:7-9 " Maana BWANA MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimekaza uso wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa sitaona haya. Yeye anipatiaye haki yangu yu karibu; ni nani atakayeshindana nami? Na tusimame pamoja; ni nani aliye hasimu yangu? Na anikaribie basi. Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mkosa? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala."
4. Uwe Mtu wa shukrani mbele za MUNGU .
1 Wathesalonike 5:18 ''shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU.''
5. Msikilize ROHO MTAKATIFU daima na kufuata anachokuambia.
Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments