![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe Ndugu zangu wote.
Ukisoma 1 Nyakati 16:29 Biblia inasema "Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;-
◼️Kumbe ni vizuri kwenda mbele za MUNGU tukiwa na Sadaka.
Zaburi 96:8 "Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka mkaziingie nyua zake."
◼️Kumbe ni vizuri kwenda Ibadani tukiwa na Sadaka.
◼️Kuna mazingira ni MUNGU Mwenyewe anataka tutoe Sadaka ndio maana anaagiza kutoa Sadaka na Kuna kazi sadaka zinaweza kufanya kiroho.
Matendo 10:4 "Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za MUNGU."
Sadaka na Zaka ni takwa la kiroho hivyo ni Muhimu sana kutoa.
Kosa kubwa la watoaji Sadaka na Zaka huwaangalia wapokeaji wa matoleo hayo ambao ni Watumishi na sio kumwangalia MUNGU anayeihitaji sadaka hiyo.
Kuna watu dhambi yao ilionekana ni kubwa sana mbele za MUNGU Kwa sababu ya kuidharau sadaka ya MUNGU.
1 Samweli 2:17 ''Hivyo dhambi yao wale vijana ilikuwa kubwa sana machoni pa BWANA; kwa maana hao watu walidharau sadaka ya BWANA.''
Kuna mpaka Watumishi baada ya kuinuliwa kiuchumi huanza kuhubiri mafundisho tofauti kuhusu Sadaka na Zaka, ni dhambi kufanya hivyo na unaweza hata usidumu kwa sababu unapotosha kuhusu Sadaka.
1 Samweli 2:29-30 " Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema? Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu."
Ukitaka kujua Nguvu ya Sadaka na Zaka tafuta Mtumishi hata mmoja ambaye alianza kukashifu Zaka harafu kwa muda mrefu katika mafundisho yake harafu Mtumishi huyo akadumu, kwa utafiti wangu sikuwahi kumwona Mtumishi wa namna hiyo.
✓✓Ndugu, ukiinuliwa elewa kanuni ya meno la MUNGU Iko pale pale usibadilishe ukweli wa Neno la MUNGU Kwa namna yeyote ile.
◼️Sadaka na Zaka ni za Muhimu sana kutoa maana ni MUNGU Mwenyewe anataka tutoe.
Mathayo 6:4 "sadaka yako iwe kwa siri; na BABA yako aonaye sirini atakujazi."
Kuna faida nyingi sana za utoaji Sadaka na Zaka.
Mfano hai ni huu
1 Samweli 7:9 "Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli; BWANA akamwitikia."
✓✓MUNGU akamwitikia Samweli baada ya sadaka na Maombi.
Ngoja nikupe ushuhuda wangu mwenyewe Mimi Peter Mabula.
Kuna kipindi nilikaa muda mrefu sana bila MUNGU kusema na Mimi kwa uwazi, ilinisumbua sana lakini siku Moja nikiwa Ibadani katika Kanisa fulani Kijijini nilikokuwa nimeenda, wakati wa Matangazo Ibadani Mchungaji wa Kanisani pale alitoa Tangazo akisema inahitajika Tsh 150,000 ili kuweka umeme Kanisani hapo maana umeme ndio ulikuwa unapita pale Kijijini.
Watu wote walikuwa kimya lakini nikajisikia nasema "Mimi nitaitoa hiyo Sadaka ya ujenzi ili kuleta umeme Kanisani" na pesa Pekee niliyokuwa nayo ni hiyo laki na elfu hamsini, nikaitoa.
Baada ya pale tukaanza kuabudu ili Neno la MUNGU lianze kuhubiriwa MUNGU wakati huo alisema na Mimi mambo mengi sana.
Nilianza kufunuliwa Ufunuo wa live kuhusu watu wengi ambao nimekuwa nawaombea, niliona mambo mengi hadi nikashangaa, nikagundua Kuna faida zingine za ajabu zilizojificha zinazotokana na utoaji Sadaka.
Niligundua kabla ya hapo nilikuwa na muda mrefu sana sijatoa na hata pale MUNGU aliponihimiza nilikuwa mzito.
Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu unaweza usinielewe kwa ukubwa unaostahili ninapokuambia haya yaliyonitokea lakini ROHO MTAKATIFU ashuhudie ndani Yako ili ujue faida za Siri zilizojoficha zinazotokana na utoaji Sadaka na Zaka.
MUNGU wa Mbinguni akupe Neema hiyo katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments