TUPATE WAPI MTU MWENYE ROHO WA MUNGU?

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

Tupate wapi MTU mwenye Roho wa MUNGU?

Mwanzo 41:38 "Farao akawaambia watumwa wake, TUPATE WAPI MTU KAMA HUYU, MWENYE ROHO YA MUNGU NDANI YAKE?"

◼️Swali hili alijiuliza Siku Moja Farao baada ya kukosa kabisa Mtu mwenye ROHO wa MUNGU katika Taifa la Misri hadi alipotokea Yusufu.

Zamani kabla ROHO MTAKATIFU haijaanza kufanya kazi na watu walio na KRISTO ilikuwa vigumu sana kumpata Mtu mwenye ROHO wa MUNGU ingawa walikuwepo wachache na aliowapa Neema yeye.

◼️Leo watu wenye ROHO wa MUNGU ni wengi maana ni wakati wa ROHO MTAKATIFU.

Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye BABA atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."

✓✓Zamani za akina Yusufu kwa sababu taifa Zima la Misri walikuwa wanaabudu Miungu ni Yusufu Pekee aliyekuwa na ROHO wa MUNGU.
Kuabudu miungu kunaweza kumuondoa ROHO MTAKATIFU kwa Mtu 


◼️Ukiwa na ROHO MTAKATIFU ujue kibali Cha MUNGU kitakuwa juu Yako ndio maana tunaona baadhi ya Sheria za kiungozi katika taifa la Misri akizileta Yusufu.

Mwanzo 47:26 "Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao."

◼️Watu wenye ROHO MTAKATIFU ni watu wa Muhimu sana kwa watu wote na wamebeba misaada mingi ya kiroho kwa watu wengi.

Kuna faida kubwa nyingi za kuwa na ROHO MTAKATIFU, baadhi ni hizi

1. Paulo akijaa ROHO MTAKATIFU alimjua Mchawi Elima na akamzuia kuwaroga watu.

Matendo  13:8-11" Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa ROHO MTAKATIFU, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza."

✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza akukupa kulijua jambo kiroho ambalo kwa macho ya kimwili usingelijua.

2. Stefano akijaa ROHO MTAKATIFU alipaona Mbinguni na aliuona utukufu wa MUNGU na Stefano pia alikuwa akifanya Miujiza 

Matendo  7:55 "Lakini yeye akijaa ROHO MTAKATIFU, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa MUNGU, na YESU akisimama upande wa mkono wa kuume wa MUNGU."

✓✓ROHO MTAKATIFU anaweza kukupa kuona mambo makubwa ambayo hukuwa unayajua.

✓✓Ukiwa na ROHO MTAKATIFU ni rahisi kufanya Miujiza ya ki MUNGU.

3. Petro akijaa ROHO MTAKATIFU alihubiri watu wengi wakaokoka.

Matendo  4:8 "Ndipo Petro, akijaa ROHO MTAKATIFU, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,"

✓✓ROHO MTAKATIFU anatupa ujasiri wa kufanya kazi ya MUNGU ambapo bila ROHO MTAKATIFU tusingeweza.

✔️✔️Wewe Mhubiri mhitaji sana ROHO MTAKATIFU.

✔️✔️Wewe  mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili ufanye kazi ya MUNGU katika KRISTO YESU.

✔️✔️Wewe muimbaji wa nyimbo za Injili unamhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili ufanye kazi ya MUNGU inayoishi.

4.  Yusufu akiwa na ROHO MTAKATIFU alitafasiri ndoto.

Mwanzo 41:25 "Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; MUNGU amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu."

✓✓ROHO MTAKATIFU anayo maarifa ya ki MUNGU ambayo Ukiwa naye anaweza kukupa.

Ndugu mhitaji sana ROHO MTAKATIFU ili siku Moja watu waseme "TUPATE WAPI TENA MTU KAMA HUYU MWENYE ROHO WA MUNGU?"

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments