![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Walawi 18:22 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo."
◼️Neno la MUNGU hapa linakataza Mwanaume kumwingilia kimwili Mwanaume mwenzake, ni machukizo makuu kwa MUNGU.
◼️Neno la MUNGU hapa linakataza Mwanaume kumuoa Mwanaume mwenzake kama ambavyo Mwanaume humuoa Mwanamke na kulala naye kimwili wakiwa wanandoa.
Walawi 20:13 "Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao."
◾Hivyo Wewe Mwanaume kamwe Usikubali kugeuzwa Mke na Mwanaume mwenzako na kuingiliwa kingono.
◾Hivyo Wewe Mwanaume kamwe Usikubali kumwingilia kimwili Mwanaume mwenzako Kwa namna yeyote ile.
Kwa Sheria ya Neno la MUNGU zamani Mtu Mwanaume anayemwingilia kimwili au anayeingiliwa kimwili waliuawa wote.
Walawi 18:29 "Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao."
◼️Ni dhambi mbaya Mwanaume kuingiliwa kimwili lakini pia ni dhambi mbaya sana Mwanamke kuingiliwa kimwili kinyume na maumbile.
➡️Biblia inakataza Mwanamke kuingiliwa kinyume na maumbile, ni machukizo makuu.
Warumi 1:26 " Hivyo MUNGU aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;"
➡️Biblia pia inakataza Wanaume kuwakiana tamaa ya ngono na Wanaume Wenzao na inakataza Wanaume kuzini na Wanaume Wenzao.
Warumi 1:27 "wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao."
✓✓Ndugu, tendo la Ndoa ni katika Ndoa tu Tena ni Ndoa ya Mwanaume mmoja na Mwanamke mmoja, nje na hapo ni dhambi mbaya.
Kinachofanyika nje ya Ndoa Takatifu ni uzinzi na uasherati na Biblia inakataza dhambi hiyo.
Waebrania 13:4 ''Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."
Kitendo Cha Mwanamke kuingiliwa kinyume na maumbile au kitendo Cha Mwanaume kuingiliwa kimwili au kuingilia kimwili, kitendo hicho kinaitwa ufirwaji, ufiraji au ulawiti , ni machukizo makuu.
◼️Na Biblia ipo wazi sana kwamba Wafiraji na Walawiti sehemu yao ni jehanamu na sio Mbinguni.
1 Wakorintho 6:9 "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,"
◼️◼️Ndugu, kama unafanya kitendo hicho Cha kufira au kulawiti tubu, okoka na usirudie Tena kufanya hivyo.
◼️◼️Kama unafanyiwa kitendo hicho Cha kufirwa au kulawitiwa tubu, okoka na usikubali kamwe Tena kufanyiwa kitendo hicho
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments