![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
Walawi 20:10 "Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa."
◼️Zamani Mke wa Mtu na Mume wa Mtu wakikutwa wanazini walikuwa wanauawa wote.
◼️Kama ambavyo ni dhambi Mtu kuzini na Mtu Mwingine yeyote nje na Mke wake au Mume wake hivyo hivyo ni machukizo makuu kwa Mume wa Mtu kuzini na Mke wa Mtu.
◼️Katika Maisha Yako yote Usikubali kamwe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mke wa Mtu au Mume wa Mtu.
Walawi 18:20" Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye."
✓✓Ukifanya hivyo maana yake utajinajisi kiroho.
Kujinajisi maana yake kujichafua kiroho.
Ukichafuka kiroho ni rahisi kupata laana au magonjwa au mikosi au balaa.
◼️Zamani Waisraeli ili kuondoa tabia ya Mume wa Mtu na Mke wa Mtu kuzini walikuwa wanauawa wote.
Kumbu 22:22 "Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli."
Ndugu Inawezekana umewahi kufanya kitendo hicho MUNGU anasema yeye ndiye Shahidi.
Yeremia 29:23 "kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA."
◼️➡️Ndugu, tubu, okoka na kuacha dhambi hiyo.
◼️➡️Mkimbilie Bwana YESU KRISTO Kwa Wokovu.
Amua kumpokea kama Mwokozi wako na badilika tabia.
◼️Biblia inamtaka Kila Mtu aiheshimu Ndoa yake na Ndoa za wengine zote.
Waebrania 13:4" Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments