WATU WANAOTANGULIWA NA MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU wa Mbinguni 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu zangu wote.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


◼️Kuna watu hutanguliwa na MUNGU katika Maisha yao, safari zao, kazi zao, kazi ya Injili n.k


Kutoka 13:21-22" BWANA naye AKAWATANGULIA MCHANA NDANI YA WINGU MFANO WA NGUZO, ILI AWAONGOZE NJIA; NA USIKU, NDANI YA MOTO MFANO WA NGUZO, ILI KUWAPA NURU; wapate kusafiri mchana na usiku; ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu."


MUNGU Kwa ajili ya Agano lake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo aliamua kuwaokoa uzao wao.


Kutoka 14:13-14 " Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."


Biblia inasema hapo juu kwamba MUNGU akawatangulia Mchana na Usiku.


✓✓Hii inatufunfisha kwamba wapo watu MUNGU anaweza kuwatangulia ili kuwalinda, kwa sababu watu hao wako katika kusudi lake au Agano lake.

Watu hao muda wote atakuwa anawatazama.


✓✓Watu hao kwanza ni yeye MUNGU hutangulia kuwachagua.


Waefeso 1:5 "Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya YESU KRISTO, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake."


◼️Kwa habari ya watu ambao MUNGU huwatangulia tunajifunza kwa Waisraeli kwamba wakati adui zao walipowakaribia Malaika aliyekuwa mbele alirudi nyuma ili kuwahakikishia usalama wao, Inawezekana na kwako pia katika KRISTO YESU Mwokozi.


Kutoka 14:19 "Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;"


Watu wanaotanguliwa na MUNGU ni watu gani?


1. Watu wanaomcha MUNGU katika KRISTO YESU na kutii sana Sauti yake katika ROHO MTAKATIFU.


Kumbu 13:4 "Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye."


2. Watu walio na ROHO MTAKATIFU 


Warumi 8:9 "Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake."


3. Watu wanaomtumikia Bwana YESU KRISTO 


Warumi 14:18 "Kwa kuwa yeye amtumikiaye KRISTO katika mambo hayo humpendeza MUNGU, tena hukubaliwa na wanadamu."


4. Watu wanaofanya mapenzi ya MUNGU.


Marko 3:35 "Kwa maana mtu ye yote atakayeyafanya mapenzi ya MUNGU, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu."


5. Watu walio katika kusudi la MUNGU.


Kutoka 23:23 "Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali."


◼️Kwa kumtumia Malaika MUNGU aliwangalia hawa kwa sababu walikuwa ndani ya kusudi lake.


✓✓Ndugu mpendwa Fanya yake yatakayomfanya MUNGU wa Mbinguni akutangulie.


✓✓Rafiki Fanya yake yatakayomfanya Bwana YESU KRISTO akutangulie.


◼️Akikutangulia MUNGU  utakuwa salama daima.


◼️Akikutangulia YESU KRISTO utakuwa mshindi daima.

Hakikisha uko naye moyoni mwako ili akutangulie, mpokee kama Mwokozi wako na atakuja maishani mwako.



MUNGU akikutangulia atafanya Nini?


1. Atawapiga adui zako ili wasikudhuru.


Kumbu 1:30 " BWANA, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu;"


2. Ili kukupa ushindi ambao hautauhangaikia.


Kumbu 9:3 "Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA."


3. Ili kuhakikisha haupungukiwi.


Kumbu 31:8 "Naye BWANA, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike."


4. Ili akupe kuwaona adui zako.


Zaburi 59:10 '' MUNGU wa fadhili zangu atanitangulia, MUNGU atanijalia kuwatazama adui zangu."


5.  Ili akuongoze sehemu salama.


Isaya 49:10 "Hawataona njaa, wala hawataona kiu; hari haitawapiga, wala jua; kwa maana yeye aliyewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza."


6.  Ili kukulinda.


Isaya 52:12 "Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na MUNGU wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde."


7. Ili kukuandalia kitu kilicho Bora .


Waebrania 11:40 "kwa kuwa MUNGU alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi."


✓✓Hawezi MUNGU kukuandalia kitu kilicho Bora harafu asikulinde na kukutangulia ili ukifikie hicho kilicho Bora.

◼️Lazima MUNGU atakulinda na kukutangulia kama amekuandalia kitu Bora na anataka ukipate au ukifikie.


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments