KUFANIKIWA NA MAONO YA KUFANIKIWA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU ujue Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.

Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Kufanikiwa ni kitu kizuri ambacho Kila Mtu anakihitaji.


2 Wafalme 18:7 "Naye BWANA akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia."


◼️Hata Kanisa la KRISTO linahotaji mafanikio ya Watu wake.

Mkristo akifanikiwa Kanisa limefanikiwa.

 Mkristo akiwa na uchumi mzuri Kanisa linakuwa na uchumi mzuri.


➡️Biblia inataka Mkristo afanikiwe.


3 Yohana 1:2 " Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo."


◼️Kufanikiwa ni Ahadi ya MUNGU Kwa watu wake wanaofuata Kanuni zake zinazoleta Mafanikio.


Kumbu 4:40 "Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele."


◾Mafanikio ni nini?


➡️Mafanikio ni kupata ulichokuwa unahitaji.


➡️Mafanikio ni kufikia malengo uliyokusudia.


Ili ufanikiwe wakati mwingine unahitaji vitu viwili muhimu.


◼️Unahitaji maono na ndoto, sina maana ya ndoto unazoota usiku au maono unayoona wakati hujalala bali Nina maana ya "Wewe unataka kuwa nani baadae?" Au unataka kufanya Nini baadae 


Mfano 

2  Nyakati 2:1 "Basi Sulemani alikusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, na kuujengea ufalme wake nyumba."


Ili uwe huyo wewe wa baadae unahitaji ndoto na maono.


➡️Ndoto hizi na maono haya ni nia, mipango na mikakati na ramani ya kupitia ili ufikie mafanikio yako.


Isaya 65:21 "Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake."


Je una maono gani?


◼️Ni vizuri sana kuwa na ndoto Yako na iombee katika Jina la YESU KRISTO.


Je una ndoto gani mteule wa KRISTO?


◼️Ni vizuri sana kuwa na Maono Yako yaombee Kisha Jifunze Neno la MUNGU namna ya Maono Yako yatafanikiwa kwa kanuni zipi.


Je unataka kuwa nani Mteule?


Shika Agano la MUNGU katika KRISTO YESU ambalo limebeba Mafanikio.


Kumbu 29:9 "Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo."


Nikupe mfano rahisi.

Mimi Peter Mabula Nina maono ya kuhubiri Injili ya KRISTO Tanzania nzima kisha Africa Mashariki na Kati nzima.

Nina ndoto ya kuhakikisha maelfu na mamia elfu elfu ya watu wanampokea YESU KRISTO kama Mwokozi ili majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha uzima Mbinguni.


Hayo ni maono yangu na ndoto yangu, naamini sasa umeelewa juu ya ndoto na maono katika ujumbe huu  niliokusudia kukupa muda huu?


Ayubu 22:28 "Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako."


Je una maono gani kuhusu kazi ya MUNGU?


Je una maono gani kuhusu maisha yako kiroho na kimwili?


Je una ndoto gani katika maisha yako?


Je una ndoto gani kuhusu kazi ya MUNGU?


Najua unatamani kufanikiwa kiroho na kimwili.

Mafanikio ninayoyazungumzia hapa sio Mali tu Bali ni pamoja na kuuletea faida ufalme wa MUNGU.


Vyanzo vya Mafanikio.


1. Kumcha MUNGU.


Kumbu 12:28 "Maneno haya nikuagizayo yote yatunze na kuyasikiza, ili upate kufanikiwa na watoto wako baada yako milele, hapo uyafanyapo yaliyo mema na kuelekea machoni pa BWANA, Mungu wako."


2. Kulifuata na kulitii Neno la MUNGU na Kanuni zake za kimafanikio.


Kumbu 28:1-3 " Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani."


3. Uwe mtu wa kutoa.


Mithali 3:9-20 " Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."


Maana Kanuni ya kwanza ya kufanikiwa kiroho ni kutoa.


Malaki 3:10-11 " Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi."


4. Tumia vyema kipaji chako, karama yako, ujuzi wako na hata ubunifu wako kufanya kazi  ili ufanikiwe.


Waefeso 4:28 "Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji."


5. Shirikisha mipango yako kwa watu sahihi.



1 Wafalme 5:5-8 " Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu. Basi uamuru wanikatie mierezi ya Lebanoni; na watumishi wangu watafuatana na watumishi wako; na ujira wa watumishi wako nitakupa kama utakavyosema; kwa kuwa wajua ya kwamba hakuna kwetu mtu ajuaye kukata miti kama Wasidoni. Ikawa, Hiramu aliposikia maneno yake Sulemani, alifurahi sana, akasema, Na ahimidiwe BWANA leo, aliyempa Daudi mwana mwenye akili juu ya watu hawa walio wengi.

 Hiramu akatuma watu kwa Sulemani, akasema, Nimeyasikia yale uliyoniletea; nami nitafanya kila ulitakalo katika habari ya miti ya mierezi, na miti ya miberoshi."


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments