![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KKRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
◾Katika ulimwenngu wako miungu wengi sana na watu wengi huwatambua na kuwaabudu, ni ubatili na upotovu mkubwa sana.
➡️Hata ukisooma Biblia wako miungu wengi sana kama akina Dagoni, Baali, Ashera, Mooleki,Milkom, Baal-zebuli,nisrok, Rimmon n.k
Hiyo yote nii miungu na ni maroho wa kuzimu.
Miungu hii sio MUNGU ndio maana MUNGU wa kweli anaweza kuiadhibu.
Kutoka 12:12 "Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; NAMI NITAFANYA HUKUMU JUU YA MIUNGU YOTE ya Misri; Mimi ndimi BWANA."
◼️Ingawa miungu ni wengi sana lakini MUNGU wa kweli ni mmoja tu na Biblia inatupa siri yake kwa usahihi.
1 Wakorintho 8:5-6 " Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini KWETU SISI MUNGU NI MMOJA TU, ALIYE BABA, AMBAYE VITU VYOTE VIMETOKA KWAKE, NASI TUNAISHI KWAKE; YUKO NA BWANA MMOJA YESU KRISTO, AMBAYE KWAKE VITU VYOTE VIMEKUWAPO, NA SISI KWA YEYE HUYO."
◼️MUNGU wa kweli ni mmoja tu na yuko na Mwanaye wa pekee YESU KRISTO.
➡️Hakuna Mwanadamu yeyote hata mmoja anayeweza kumfahamu MUNGU wa kweli nje na KRISTO YESU.
Yohana 1:18 "Hakuna mtu aliyemwona MUNGU wakati wo wote; MUNGU Mwana pekee aliye katika kifua cha BABA, huyu ndiye aliyemfunua."
◼️Hivyo kama kuna mtu yeyote duniani anadhani ana Mungu wa kweli nje na MUNGU katika KRISTO YESU jibu ni kwamba mtu huyo ana miungu.
➡️Leo duniani kuna dini zaidi ya 15 na watu wengi ni waumini wamefuata dini hizo, ukweli mmoja ni kwamba watu wote wa dini zote zilizo nje na Wokovu wa KRISTO YESU, Watu hao wanaabudu miungu na sio MUNGU.
Matendo 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
➡️Leo kuna madhehebu maelfu ya dini mbalimbali, ukweli mmoja ni kwamba kila dhehebu au madhehebu yaliyo kinyume na Wokovu wa KRISTO, mtu huyo anahusika huko anaabudu miungu na sio MUNGU wa Mbinguni.
◼️Bwana YESU alisema aliyemuona yeye huyo ndie amemuona MUNGU wa kweli mmoja.
Yohana 14:9 "YESU akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? ALIYENIONA MIMI AMEMWONA BABA; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe BABA?"
◼️◼️Hiyo ina maana kila anayemfuata YESU huyo ndiye anayemfuata MUNGU wa kweli.
◼️Ndugu, unayemfuata YESU KRISO wewe umemfuata MUNGU wa kweli.
◼️Ukimuona YESU umemona MUNGU wa kweli.
Yohana 14:7 "Kama mngalinijua MIMI, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona."
➡️Ndugu amua kuanzia leo kujitenga na miungu maana MUNGU wa kweli umemfahamu.
1 Yohana 5:20 "Nasi twajua kwamba Mwana wa MUNGU amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake YESU KRISTO. Huyu ndiye MUNGU wa kweli, na uzima wa milele."
➡️Ndugu, hata kama dini yako ni nzuri sana, ina mafundisho mazuri, ina tamaduni nzuri kama dini hiyo iko kinyume na Wokovu wa KRISTO YESU hiyo dini ni ya shetani, ondoka kwenye dini ya shetani.
1 Timotheo 4:1 "Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;"
◼️Ndugu amua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kuanzia leo.
Ndugu amua kuokoka ili sasa uanze kuumwabudu MUNGU wa kweli.
Yohana 4:23-24 " Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu BABA katika roho na kweli. Kwa maana BABA awatafuta watu kama hao wamwabudu. MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
➡️Kumbuka miungu ni wengi ila MUNGU ni mmoja.
Je wewe hadi sasa uko kwa MUNGU au kwa miungu?
◼️◼️Nakushauri njoo kwa YESU KRISTO.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments