DHABIHU NI NINI?

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.

Rafiki yangu mmoja aliniandikia hivi "Bwana YESU asifiwe Mabula  Mtumishi Wa MUNGU.

Nimesoma mafundisho yako jinsi ya kutunza nguvu ya MUNGU naomba kujua maana ya dhabihu maana umesema kuhusu matoleo ya zaka,sadaka na dhabihu. sina ufahamu juu ya dhabihu lakini zaka na sadaka navifahamu.

barikiwa Mtumishi"


Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.


◼️Kwa kifupi Dhabihu ni Sadaka unazozitoa baada ya Fungu la kumi.


Yaani mfano mshahara wako ni laki moja.

Unatoa elfu 15 kama Zaka.

Kiroho Zaka hapo ni elfu 10 na iliyobaki yote ni dhabihu.


Kumbu 12:6 "pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo;"


➡️Hawa Waliambiwa na MUNGU wapeleke Sadaka za kuteketezwa hizi zinafahamika, wapeleke huko Dhabihu na Zaka, hapo Zaka inafahamika ni 10% kwenye 100% ya Mtu lakini ile atakayotoa baada ya Zaka ni Sadaka ya dhabihu.


◼️Dhabihu pia ni Sadaka maalumu ambayo ROHO MTAKATIFU anakupa msukumo rohoni mwako  kutoa au anasema na Wewe utoe.


➡️Sadaka hiyo ya dhabihu isiwe umeshawishiwa na Mtu yeyote yaani chanzo ni Wewe binafsi na ROHO MTAKATIFU ndani Yako.


➡️Ni sadaka Maalumu sana kwa sababu zamani ilihisisha umaalumu mkubwa katika kuitoa.


➡️ Dhabihu ni Sadaka ya kipekee inayotokana na Mtu kuitoa kwa kujitoa sana, ni Sadaka nzuri inayohitaji maamuzi magumu sana ndani ya moyo wa Mtu husika.


Kuna matolea ya aina 3 ambayo MUNGU ameagiza watu watoe.

1. Sadaka

2. Zaka/Fungu la kumi 

3. Dhabihu.


Kuhusu Sadaka tu hii inaunganisha Sadaka zote na za Kila namna Wanaotoa watu kwa MUNGU nje na Zaka na Dhabihu.

Sadaka Mfano wake ni Sadaka za jumapili, changizo, Sadaka ya kusafirisha Watumishi, Sadaka za kununua vyombo, Sadaka za Uinjilisti au kuipeleka Injili n.k


➡️Wakristo wengi huwa hawatoi dhabihu kwa sababu hawajui dhabihu ni nini ndio na wanakosa baraka zilizo ndani ya dhabihu.


Zaburi 54:6-7 " Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema. Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu."


Baadhi ya faida za dhabihu kwa ufupi


1. Baraka zilizo ndani ya dhabihu ni MUNGU kulikumbuka agano kati ya wewe na yeye kupitia dhabihu ulizotoa mbele zake.


Zaburi 50:5 "Nikusanyieni wacha MUNGU wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu."


◼️MUNGU akilikumbuka agano lililo ndani ya dhabihu yako usitarajie maagano ya giza yaliyokufunga yatabaki.


2. Majibu ya Mtu yanaweza kutoka kutoka kwenye tukio la utoaji dhabihu.


Mfano hai ni Daudi kuwa Mfalme.


1 Samweli 16:3 "Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako."


3. Dhabihu inayoambatana na utakatifu inaleta kukubaliwa na MUNGU.


Mambo  22:29 "Tena mtakapomchinjia BWANA dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa."


4. Majibu ya MUNGU Kwa Mtu yanaweza kusababishwa pia na utoaji wa Dhabihu.


Zaburi 20:3 -4 "Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote."


5. MUNGU anaweza kutoa adhabu kwa wabaya wakati wa Dhabihu.


Sefania 1:8 Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni.


◼️Dhabihu ni sadaka ya muhimu sana.


◼️Kuna dhabihu hadi ilifanya kazi ya kusafisha nakala za mambo ya Mbinguni, hiyo ni dhabihu ya Bwana YESU KRISTO.


Waebrania 9:23 "Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo."


Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments