![]() |
| Peter na Jemimah Mabula Watenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◾Kicho ni Nini?
◼️Kicho Ina maana ya kumcha MUNGU katika KRISTO YESU.
Matendo 9:31 "Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha BWANA, na faraja ya ROHO MTAKATIFU."
◼️Kicho ni kumcha MUNGU.
Zaburi 2:11 "Mtumikieni BWANA kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka."
➡️Kumcha MUNGU ni Nini?
◼️Kumcha MUNGU ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako, ukaacha dhambi Kisha ukaanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
◼️Kumcha MUNGU ni kumpenda MUNGU katika KRISTO YESU Kisha ukafuata daima ayatakayo MUNGU ukiongozwa na Neno lake.
➡️Mtu Mcha MUNGU ndio Mtu mwenye kicho.
◼️Mtu mwenye kicho ni Mtu anayemcha MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi.
Waefeso 5:21 "hali mnanyenyekeana katika kicho cha KRISTO."
➡️Je Wewe unamcha MUNGU wa Mbinguni?
Mithali 28:14 "Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote; Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara."
➡️Je Wewe una kicho?
Malaki 1:6 "Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?"
◼️Katika Maisha Yako yote Hakikisha una kicho yaani Hakikisha unaambatana na kumcha MUNGU wa Mbinguni.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments