![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Ukisoma Warumi 8:37 Biblia inasema "Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda."
➡️Kumbe tunaweza kushinda na zaidi ya kushinda Tena katika Mambo yote tunaweza kushinda.
◼️Ukisoma Yeremia 15:20 Biblia inasema "Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA."
➡️Kumbe ni mpango wa MUNGU kwamba Wewe Mteule wake katika KRISTO YESU usishindwe na Maadui wa kiroho wa namna yeyote ile.
◼️Biblia inasema"Watapigana" kumbe maadui Wapo na wanaweza kupigana na Wewe kabisa hivyo unapopigana nao usijisikie vibaya maana hao maadui wa Kiroho wapo tu ila Ahadi ya kudumu ya MUNGU kwako ni kwamba hata wakipigana na Wewe vipi lakini hawatakushinda.
◼️Uwe Muombaji shujaa kama huyu anayesema amewafuata adui zake na kuwapiga hadi walipokoma kabisa.
2 Samweli 22:38 "Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza; Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa."
✔️Ndugu adui zako ni Wakuu wa Giza, majeshi ya majini, mizimu na mawakala wengine wa shetani wanaotesa Maisha Yako.
◼️Mambo matano yanayoweza kukufanya uwashinde maadui zako wote ni haya.
1. Ukitaka umshinde Kila adui hakikisha una YESU KRISTO na omba katika Jina lake Takatifu.
1 Wakorintho 15:57 "Lakini MUNGU na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu YESU KRISTO."
◼️MUNGU hutupa kushinda kwa njia ya YESU KRISTO Mwokozi wetu, hivyo Hakikisha YESU KRISTO ni Mwokozi wako na uko naye.
◼️Mwamini Bwana YESU KRISTO maana ndio chanzo Cha ushindi wa watu wa MUNGU.
1 Yohana 5:5 "Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba YESU ni Mwana wa MUNGU?"
◼️Kuwa na YESU KRISTO kutakufanya kuwa mshindi dhidi ya adui zako wote maana Bwana YESU atakuwa pamoja na Wewe.
Yeremia 1:19 "Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe."
◼️Hakikisha una YESU KRISTO kama Mwokozi wako na omba katika Jina lake hakuna adui atakuweza.
Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."
2. Ukitaka umshinde Kila adui hakikisha una ROHO MTAKATIFU ndani Yako.
1 Yohana 4:4 "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia."
◼️Aliye ndani ya Wateule wa KRISTO waaminifu ni ROHO MTAKATIFU na yeye ndio chanzo Cha ushindi wao mkuu.
➡️Kwa namna gani utashinda Ukiwa na ROHO MTAKATIFU?
◼️Ni kwa kuomba katika yeye ROHO MTAKATIFU.
Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,"
➡️Ni kwa namna gani utashinda Ukiwa na ROHO MTAKATIFU?
◼️Ni kwa kumtii na Kumsikiliza anachokuambia yeye ROHO MTAKATIFU.
Wagalatia 5:16 "Basi nasema, Enendeni kwa ROHO, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."
3. Ukitaka umshinde Kila adui yako Hakikisha una Neno la MUNGU ndani Yako.
Tito 1:9 "akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga."
◼️Biblia inasema kwa Neno utawashinda Wenye kupinga, wenye kupinga Neno la MUNGU ni pamoja na mawakala wa shetani wote, hivyo utawashinda kwa Neno la MUNGU.
◼️Kuliishi Neno la MUNGU, Kufanya Maombi ukitumia Neno la MUNGU Kwa kulikiri juu ya ushindi wako lazima utashinda.
1 Yohana 2:14 "Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la MUNGU linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu."
◼️Biblia inasema Neno la MUNGU linakaa ndani yenu mmemshinda shetani.
◼️Ndugu Hakikisha Neno la KRISTO liko ndani Yako ili uwashinde mawakala wa shetani wote.
4. Ukitaka umshinde Kila adui hakikisha una Imani thabiti kwa YESU KRISTO.
◼️Watumishi wa MUNGU wa zamani walishinda kwa Imani thabiti kwa MUNGU.
Waebrania 11:33 "ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba,"
◼️Hakikisha una Imani kubwa kwa YESU ili Imani Yako kubwa ifanye kazi kwenye Maombi Yako na Maisha Yako.
➡️Omba kwa Imani na sio vinginevyo.
Mathayo 21:21 "YESU akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka, ukatupwe baharini, litatendeka."
5. Utawashinda adui zako kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO.
Mathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
◼️Uwe una muda wa Maombi.
◼️Tenga muda hata wa Kufunga maana ushindi upo ukiomba kwa Jina la YESU KRISTO.
Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana."
➡️Acha kuomba Ukitaja dhehebu lenu au ukimtaja baba Yako wa kiroho au ukitaja Mtumishi Fulani, Wewe omba ukimtaja Bwana YESU KRISTO maana ni kwa Jina lake tu ndio tunapata ushindi.
Zaburi 18:3 "Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu."
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments