SWALI JUU YA ZAKA/FUNGU LA KUMI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze kitu kupitia ujumbe huu uliotokana na swali ambalo mmoja wa marafiki zangu wanaofuatilia masomo yangu aliniandikia.


Rafiki huyo aliandika hivi "Bwana Yesu asifiwe Mtumishi Mabula.

Nimeona somo lako kuhusu zaka na nikabarikiwa lakini baadae nikaona Mtumishi mmoja anafundisha kwamba kutoa Zaka sio lazima ikanichanganya ingawa naungana na Wewe kama ulivyo fundisha au una ufafanuzi zaidi ili na wengine wajifunze"


Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.


◼️Kwanza kuhusu kutoa Fungu la kumi ni kwamba MUNGU anasema usiache kutoa.


Kumbu 14:22 "Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka."


◼️Hii Ina maana usiache kutoa Fungu la kumi kutoka mwaka mmoja hadi Mwingine yaani usiache kutoa Zaka siku zote katika unavyoipata.


➡️Katika maandiko kwa kuchunguza kwangu Kuna mambo machache ambayo Biblia inasema "USIACHE" Moja ya hayo ni USIACHE kutoa Zaka kama andiko linavyosema hapo juu.


Kama unaambiwa usiache maana yake kiroho ni Muhimu sana kutoa kwa faida Yako mtoaji.


Matendo  20:35 "......................... Ni heri kutoa kuliko kupokea."


◼️Katika Kanisa la leo kuna baadhi ya watu kwa tamaa zao huacha kutoa fungu la kumi na kisha kutafuta watu wa kuwasapoti.


➡️Wengi akili yao hudhani kwamba hawawezi kutoa zaka kwa sababu agano jipya halizungumzii sana kuhusu zaka, wala hiyo sio sababu ila ni watu hao kutawaliwa na kuipenda dunia.


Hagai 1:6-7 " Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu."


➡️Watu hao hao hutoa pesa zaidi ya fungu la kumi kwenye mambo yao mengine ambayo wala hayo hayajawahi kutengeneza hazina zao mbinguni.


➡️kuna watu hudhani Biblia imejigawanya kiasi kwamba yaliyo Agano la kale hayahusiki na sasa.

Tunatakiwa kuisoma Biblia kwa jinsi ya KRISTO ndipo tutaielewa.


◼️Hebu muulize mtu anayebisha kutoa Zaka, muulize kwamba ni wapi YESU alikataza kutoa zaka?

Mwambie akupe andiko hilo.


◼️Tunajua  Bwana YESU alisahihisha baadhi ya mambo yaliyokuwepo kabla ya Agano jipya Mfano alisahihisha kuhusu vyakula akisema     " kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.-Marko 7:19"  na baadhi ya mambo mengi

lakini hakuwahi kuisahihisha Zaka au kuikataza maana Zaka haikuanza kwa sababu ya torati bali zaka ipo kabla ya torati.


➡️Akina Ibrahimu hawakujua hata torati ni nini lakini walitoa zaka.


➡️Akina Yakobo hawakujua torati ni nini lakini walitoa zaka.


Zaka ni jambo la lazima kwa kila Mkristo.


◼️Utofauti wa utoaji kati yetu  na watu wa Torati ni kwamba sisi tunatoa Zaka kamili lakini tunatoa kwa moyo safi na kwa upendo mbele za MUNGU na sio kutoa kwa sheria kama watu wa Torati.


✔Wengi sana Wanaopinga kutoa Zaka kwa ni watu ambao hawajui Kanuni za MUNGU au wanaziona mzigo.


✔Na anza uchunguzi kuanzia Leo hautakuja kamwe kumuona asiyetoa zaka anakua kiroho.


✔Wasiotoa Zaka huvamiwa na roho ya kifarisayo na kuwa wabishi tu siku zote wa Neno la MUNGU.


2 Wakorintho 9:6 " Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu."


✔Mkristo akizijua vyema faida za Fungu la kumi kiroho hawezi kamwe kuacha kutoa Fungu la kumi.


✔ Mtu akizijua kazi za fungu la kumi kiroho hakika anaweza kuwa anatoa zaidi ya fungu la kumi yaani anakuwa anatoa fungu la kumi kamili kisha anaongeza juu yake dhabihu.



Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe

Comments