![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe rafiki.
Jifunze kitu kupitia ujumbe huu unaotokana na mambo aliyonieleza rafiki yangu mmoja ambaye husoma masomo yangu Mtandaoni.
◼️kupitia Ujumbe huu ninachoweza kusema ni kwamba Hata Makanisani Kuna Watumishi hutafuta Mafanikio kupitia vitu ambavyo sio MUNGU amewaagiza hasa vitu vya upako.
➡️ Mtu mmoja aliniandikia ujumbe huu chini juu ya Mafuta ya upako ambayo yamejaa baadhi ya Makanisa kwa kuiga, yaani Mafuta ya upako yanapogeuka kazi ya shetani na kudhuru watu.
➡️Ndugu huyo aliniandikia hivi
"Mtumishi wa Mungu, Bwana Yesu asifiwe,namshukuru Mungu kwaajili yako jinsi ambavyo umekuwa ukisaidia watu wengi nikiwemo na Mimi.
Mtumishi ngoja nikueleze maisha halisi niliyo nayo sasa. mimi nina watoto wawili na baba wa hao watoto tumetengana lakini nilikuwa sijafunga nae ndoa wala hakunitolea mahali kwa wazazi. baba yangu kabla hajafariki alikuwa akinisisitiza jambo hilo lakini mazingira yakawa ni magumu na huyo mwanaume akawa ananinyanyasa na ukorofi nami roho ya kufunga nae ndoa ikafa kabisa nikawa natamani kuondoka lakini watoto ikawa ndio kifungo nawapeleka wapi na sikuwa na kazi imeendelea hivyo baba na mama wakafariki bila kupewa mahali yangu. sasa baada ya kufahamu kuwa wazazi wangu wamekufa manyanyaso yakazidi sana, hakuna cha kuwahudumia watoto, mimi ndio nikawa baba badala ya kuwa mama kila hitaji la ndani ni mimi yuniform nguo yeye baba hausiki lakini nikawa naugua moyoni nikasema iko siku Mungu atanitoa kwenye huu utumwa. mwaka juzi nikabahatika kupata kiwanja na katika eneo la karibu na Kanisani kwetu. Na aliyeniulizia kiwanja nikamwambia unaniuzia hili eneo lakini mume wangu asijue na wewe mwenyewe umekuwa ukiona mambo anayonifanyia. basi ikaendelea hivyo nikabahatika kujenga na mpaka sasa nimeipaua tayari. sasa baba watoto akasikia kuwa nimejenga tena ni karibu na Kanisa akaanza kufatilia. kweli akaiona ile nyumba baada ya kuiona akaanza vituko mara anasema ntajinyongea kwenye nyumba yako nitie nuksi, juzi tuko kwenye ibada maana nyumba yangu iko karibu na Kanisa na yeye akaja, nilipomuona alinitoa kwenye uwepo kwakweli. tulipomaliza ibada watoto wakamsalimia akawambia waniite mimi alivyoniona akawa ananinyooshea kidole eti weweeeee nikasema kwani vipi !!
Mtumishi mbele ya watoto wangu akaanza matusi na mbele ya Mchungaji alafu ile huduma tumeianza ina wiki ya 3 washirika ndio wageni wengine ni watoto wachanga kiroho. Alinitukana matusi mabaya sana.
Mtumishi nilinyanyua kiti nusu nimpige nacho lakini kuna roho ilinambia niache, Mchungaji akamtoa akaondoka amekuwa akinifanyia vituko alienda kwa mtumishi mmoja nabii akapewa mafuta, yale mafuta alipoyaleta akanivizia nimelala akachukua bomba la sindano akanidunga mguuni mi kwa maumivu nikashtuka na kupiga kelele, nilipo muuliza kwanza akakana nilipopiga kelele zaidi sababu mguu ulikuwa unatoka damu ndio akakili kwamba amefanya kitendo hicho, yaani amekwenda kwa nabii anayetumia mafuta ya upako na ameyachukua mafuta hayo na kuamua kunifanyia kitendo hicho. Baada ha hapo ndipo Mimi nikaamua kubeba kilicho changu na kuondoka pale nyumbani.
kiufupi ndio hayo Mtumishi, Sasa usiku huu mpaka nakuomba ushauli nimeota hivi(nilikuwa maeneo ya kijijin kwetu nimebeba mtoto mgongoni natembea mara mtu akatokea nyuma yangu amevaa suruali chafu akanipita kwa kasi mbele kulikuwa na daraja akaokota majani akawa anataka kutumbukia kwenye daraja akawa anaokota uchafu pale aliponiona akaanza kunishambulia akaokota miudongo akampiga mtoto mgongoni ambae ni mtoto wake nami nikaingilia kati nikaokota mchanga kutaka kumpiga nao yeye tulipovuka daraja kulikuwepo njia panda yeye akaingia kushoto lakini anatukana anataka kunidhuru na huyu mtoto mi nikanyoosha barabara nikashtuka ndotoni ) naomba unisaidie maana ya hii ndoto mtumishi wa Mungu"ubarikiwe sana na asubuhi njema.
Majibu ya Mtumishi Peter Mabula.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana kwa Imani Yako thabiti kwa YESU KRISTO Mwokozi, unafanya vyema sana kuendelea na YESU KRISTO katika Wokovu wake katika hali zote.
Kumbuka tu jambo Moja Kuna kufutwa machozi na MUNGU Mwenyewe ukishinda ukaingia uzima wa Milele.
Ufunuo 7:17" Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na MUNGU atayafuta machozi yote katika macho yao."
Nakuomba endelea na Bwana YESU KRISTO daima.
Kwa yote hayo Mume wako alifika mbali sana ila nakupongeza sana Wewe kwa kuendelea kusimama imara na Bwana YESU KRISTO hata kama kwa muda mrefu umepitia magumu.
Mimi katika Maombi yangu nitakuombea sana na MUNGU akupe furaha, baraka na ushindi katika yote.
Huo mlima wa matatizo na visa ulivyokaa muda mrefu MUNGU akuondoa katika mlima huo Kwa namna ya kwake.
Kumbu 1:6 "BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha;"
Endelea na Bwana YESU KRISTO utamuona MUNGU wa Miujiza kwenye Maisha Yako.
Kuhusu ndoto ni Nina machache ya kusema ambayo ni hayo Nina uhakika nayo ila tafasiri ya Kila tukio la Ndoto Sina.
Ni kwamba umeota uko Kijijini kwenu maana Yako kwenye ulimwengu wa roho ni kwamba tatizo linalokutesa Sasa chanzo chake kiroho ni kule ulikowahi kuishi Zamani, katika Maombi pambana na mizimu ya Ukoo na vunja madhabahu ya giza iliyokushikilia kutokea huko.
Ndoto inaonyesha Maisha Yako yalipangiwa Mateso na manyanyaso ya kipepo, ndio maana unaona Mwanaume wa hivyo anakufuata ili kukudhuru Wewe na uzao wako, hapo kwa Maombi katika jina la YESU KRISTO utaroka katika mpango wa shetani juu Yako na hivyo Licha ya Maombi mengine omba pia ukiharibu madhabahu za giza.
Mwanaume wa Ndotoni sijui kwa usahihi ila anaweza kuwa ni Mumeo au ni mizimu ya Ukoo inayofuatilia Wewe na kizazi chako, ila ndoto inaonyesha ulitaka kumuombea kifo na angekufa kweli ungeomba hivyo, ndio maana ya kumrushia mchanga maana yake kumtamkia kifo.
Jambo la mwisho ni kwamba Ukiona kitu Ndotoni haijalishi ni kitu kikubwa kiasi gani maana yake Maombi Yako yamefanya kazi ya kufungulia ushindi wako hivyo umepewa Wewe kuamua iweje ndio maana ya kutoa ndoto.
Hivyo ukiomba kama nilivyokuambia utashinda haraka sana.
Jambo ukiliona Ndotoni katika baadhi ya ndoto kama hiyo Yako maana yake umepewa kuamua iweje.
Uliacha tu itakuwa kama ulivyoona na ukiomba unashinda kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi.
Ubarikiwe sana
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi.

Comments