SABABU 7 ZITAKAZOWAJULISHA WATU KWAMBA MUNGU YUKO PAMOJA NA WEWE.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Zipo sababu ambazo zinaweza kuwajulisha watu kwamba MUNGU wa Mbinguni Yuko pamoja na Wewe, Biblia sehemu nyingine inaita "Matunda"


 Mathayo 7:20 "Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua."


➡️Maana yake Mtawatambua kwa matokeo ya kazi zao.


◼️Hivyo Kuna vitu au Kuna matunda ambayo yanaweza kuonyesha kwamba Mtu Yuko na MUNGU wa Mbinguni.


  Mambo 7 yatakayowajulisha watu kwamba MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


1. Watu wanapogundua una kibali ambacho hakitokani na juhudi za kibinadamu ila ni uwezo wa MUNGU.


1 Samweli 18:12-14 " Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli. Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe akida wake juu ya askari elfu; naye akatoka na kuingia mbele ya watu. Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye BWANA alikuwa pamoja naye."


➡️Sauli aligundua MUNGU yupo pamoja na Daudi hivyo Sauli akaanza kumuogopa Daudi.

Lakini kitu ambacho kilimfanya Sauli agundue kwamba MUNGU yupo pamoja na Daudi ni kibali alichokuwa nacho Daudi mbele ya watu wote.


Mfano wa ajabu ni  huu yaani Waisraeli walimpenda sana Daudi kwa sababu tu alikuwa na tabia kuwaongoza vitani na kuwarudisha salama.


1 Samweli 18:16 "Lakini Israeli wote na Yuda wakampenda Daudi; kwa kuwa alitoka na kuingia mbele yao."


◼️Kuna kibali Cha ajabu Cha ki MUNGU ambacho kinaweza kuwafanya watu wagundue Wewe uko na MUNGU katika KRISTO YESU.


➡️Sizungumzii vibali vya kipepo ambavyo wahusika huua watu wao wa Karibu na kutoa kafara au kuingia maagano na shetani ili kupata kibali ambacho ni Cha muda tu Kisha uharibifu na hata jehanamu vinamfuata mhusika, Mimi Nazungumzia kibali Cha ki MUNGU ambacho ni MUNGU Mwenyewe anakupa hadi watu wanagundua Wewe una MUNGU wa Mbinguni.


2. Watu Wanapokuona unakuwa chanzo cha baraka kwa wengine bila kutumia nguvu zako bali MUNGU.


◼️Mfano hai ni Mzee Labani ambaye mapema sana aligundua MUNGU Yuko pamoja na Yakobo maana mambo yote kwenye familia yake yalibadilika baada ya Yakobo kuanza kuishi hapo.


Mwanzo 30:27 "Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako."


➡️Kumbuka MUNGU alikuwa ameshaahidi kwa Yakobo kwamba atakuwa pamoja naye.


Mwanzo 28:15 "Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia."


◼️ Labani akagundua MUNGU yupo pamoja na Yakobo akaanza kumsihi   Yakobo asiondoke hapa ili na yeye Labani aendelee kufaidika na baraka za MUNGU zinazotokana na uwepo wa Yakobo pale.


◼️Watu watagundua MUNGU Yuko pamoja na Wewe pale wanapoona unakuwa chanzo Cha baraka kwa wengine kwa sababu ya uwepo wako tu.


3. Watu Wanapoona MUNGU katika KRISTO YESU anafanya kazi na wewe kupitia ishara au miujiza au ufunuo wa ROHO MTAKATIFU.


Marko 16:20 "Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, BWANA akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]"


◼️Hii inawahusu Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO, watu watatambua MUNGU Yuko pamoja na Wewe watakapoona MUNGU anakutumia kwa ishara na Miujiza.


➡️Kumbuka Bwana YESU hawezi kukutumia kwa Miujiza kama hauko pamoja na Wewe, lazima awe pamoja na Wewe kwanza ndipo atakutumia kwa Miujiza.


Matendo  5:12 "Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;"


4. Watu Wanapogundua kazi Fulani au jukumu Fulani ni la kwako na ni MUNGU amekupa ulifanye Wewe.


1 Samweli 3:20-21 " Nao Waisraeli wote, toka Dani mpaka Beer-sheba, walitambua ya kwamba huyo Samweli amewekwa kuwa nabii wa BWANA. Naye BWANA akaonekana tena huko Shilo; kwa kuwa BWANA akajifunua kwa Samweli huko Shilo, kwa neno la BWANA. Nalo neno la Samweli likawajia Israeli wote."


➡️ Waisraeli wakatambua kwamba Samweli amewekwa na MUNGU kuwa Nabii kwa nchi nzima.

Hivyo jukumu la Kiongozi wa kiroho kwa wakati ule waligundua wote ni la Samweli, hivyo walitambua MUNGU Yuko pamoja na Samweli kwa njia hiyo.


◼️Hata wewe watu wanaweza kugundua kwamba MUNGU yupo pamoja na Wewe watakapokuona ukimtumikia Bwana YESU KRISTO Kwa uaminifu katika kile alichokupa ufanye, wataona mafanikio na watajua ni MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


5. MUNGU anaposema na Wewe na Watu wanagundua  anasema na wewe.


 1 Samweli 3:8" BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto."


◼️MUNGU anaposema na Wewe ni ishara mojawapo kwamba Yuko pamoja na Wewe, isipokuwa tu pale anaposema na Wewe kama njia ya kukuonya ili uache njia mbaya.


◼️Kama Mara kwa mara MUNGU Kwa njia ya ROHO MTAKATIFU atakuwa anasema na Wewe au kupitia Wewe hiyo ni njia inayoonyesha  Yuko pamoja na Wewe, na Kwa njia hiyo watu watajua MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


6. Watu Wanapogundua unaposhinda vita ambayo bila MUNGU usingeshinda.


◼️Kuna vita ya kiroho au ya kimwili bila MUNGU katika KRISTO YESU huwezi kushinda, hivyo unaooshinda vita ya namna hiyo ni kwa sababu tu MUNGU wa Mbinguni Yuko pamoja na Wewe.


➡️Na MUNGU siku zote hupenda kuwa pamoja na Wateule wake  katika KRISTO YESU  katika vita ili washinde.

Mfano ni huu.


Waamuzi 6:16 "BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.''


Kama MUNGU atakuwa pamoja na Wewe hakuna vita utashindwa, hata kama maadui Wana Nguvu kubwa kiasi gani Wewe utashinda kwa sababu MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


Yeremia 1:19 "Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe."


➡️Mfano hai ni Daudi Kijana Mdogo kuwashinda Simba na Dubu na  kumshinda Goliathi jitu ambaye alikuwa ameshindikana kwa mamilioni ya watu, ila kwa Daudi akapigwa Tena kwa kudhalilishwa kwa sababu MUNGU alikuwa pamoja na Daudi.


1 Samweli 17:37 "Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe."


◼️Hivyo watu watajua MUNGU Yuko pamoja na Wewe pale utakaposhinda vita ya kiroho au kimwili ambayo wanashinda walio na MUNGU katika KRISTO YESU tu.


7. Udhihirisho wa nguvu za ROHO MTAKATIFU.


➡️Mfano hai ni Paulo ambaye hauhitaji kuwaza mara mbili mbili kama kweli MUNGU Yuko pamoja naye.


Matendo  13:9-11 " Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa ROHO MTAKATIFU, akamkazia macho,

 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za BWANA zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa BWANA u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza."


◼️Udhihirisho wa Nguvu za ROHO MTAKATIFU huonyesha MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


◼️Unapotumiwa na ROHO MTAKATIFU hiyo huonyesha MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


◼️Unapoomba katika ROHO MTAKATIFU hiyo huonyesha MUNGU Yuko pamoja na Wewe.


Yuda 1:20-21 " Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU, jilindeni katika upendo wa MUNGU, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu YESU KRISTO, hata mpate uzima wa milele."


➡️Ndugu, Je mbona unatumia nguvu nyingi kujionyesha wewe kwamba MUNGU yupo pamoja na wewe?


➡️Unaweza ukamsikiliza Mtumishi muda wote huongea akijionyesha kwamba  MUNGU yupo pamoja na yeye. 

Watumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO hawahitaji kujitangaza sana kwamba MUNGU yupo pamoja nao ila Watu wengine ndio wataona na kusema  MUNGU yupo pamoja nao.


◼️Usijitambulishe acha MUNGU akutambulishe, usijitetee acha MUNGU akutetee.

Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments