WATU 7 AMBAO HAWATAKIWI KUONEKANA KATIKA KANISA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Tunafahamu Waisraeli walikuwa Kanisa wakati wa kutoka Misri,hiyo ipo.


Matendo  7:37-38 " Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, BWANA Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. Yeye NDIYE ALIYEKUWA KATIKA KANISA JANGWANI PAMOJA NA YULE MALAIKA ALIYESEMA NAYE KATIKA MLIMA WA SINAI, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi."


➡️Kumbe Waisraeli wakati wanaotoka Misri walikuwa Kanisa, Sasa hawa Kanisa  la kwanza MUNGU aliwaambia kuna aina ya watu wasionekane kwenye hilo  Kanisa.


➡️Hata Kanisa la leo watu hawa hawatakiwi kuwepo Kanisani akija mtu huyo atubu na kuacha mabaya hayo ili asiweko Mtu wa hivi Kanisani.


◼️Kanisa hilo la Jangwani MUNGU aliwaambia katika  Kumbu 18:10-11 " kwamba  wasionekane kwao watu hawa " Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu."


◾Watu ambao hawatakiwi kuonekana katika Kanisa la MUNGU.


1. Mtu anayetambika.


Yeremia 32:35 "Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala halikuingia moyoni mwangu kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda."


➡️Mtu anayetambika ni Mtu gani?


➡️Kutambika kufanya ibada za kishetani au kufanya  tambiko la jadi kwa lengo la kuwasiliana na kuheshimu mizimu, miungu ya jadi, au mababu, kufanya hivyo ni machukizo makuu kwa MUNGU wa Mbinguni.


➡️kutambika Ni Mtu anayefanya ibada ya kimila ili kuhusika na mizimu ya ukoo au mizimu ya kabila au ya eneo.


◼️Mtu wa namna hii hatakiwi kuwa miongoni mwa Wana Kanisa la MUNGU katika KRISTO YESU,  hivyo akija Kanisani anatakiwa atubu na kuokoka na kuacha kutambika, ila ikitokea Mtu hutambika Kisha anaenda Kanisani bila kuacha kutambika; hayo ni machukizo makuu kwa MUNGU.


➡️Kuna Mtu alijaribu kuwa Kanisani la MUNGU huku akitambika MUNGU alimwadhibu, Mfano ni huyu Mfalme Ahazia.


    2 Wafalme 16:3 "Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli."


➡️Mtu ampitishaye mtoto wake kati ya moto pia ni mtu anayetambika.

Kwa kosa hilo ulikuja Unabii wa kifo chake na kweli akafa.


2 Wafalme 1:15-17 " Malaika wa BWANA akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme. Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana."


➡️Hivyo Mtu anayetambika hatakiwi kuwa miongoni mwa watu wa Kanisa, kama yupo aache kutambika ili libaki Neno la MUNGU linalosema "Asionekane kwako Kanisa Mtu anayetambika"

Najua wako watu zamani kabla hawajaokoka walikuwa watambikaji wazuri ila walipoamua kumpokea YESU KRISTO waliacha habari za matambiko maana Neno la MUNGU linasema kwa Kanisa kwamba "Asionekane kwako Kanisa Mtu anayetambika "


➡️ Ndugu unayetambika na unaenda Kanisani Hakikisha Unaacha kutambika ili uwe Kanisa hai la MUNGU maana baada ya kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako MUNGU hataki kukuona Tena ukitambika.


2. Mtu atazamaye bao au nyakati mbaya .


Kumbu18:10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,


➡️Mtu atazanaye bao au atazamaye Nyakati mbaya ni Mtu gani?


◼️Mtu huyu  ni mpiga ramli kwa Jina lingine.


➡️Kupiga ramli ni elimu ya nyota au unajimu ihusuyo ubashiri juu ya jambo lililotokea, litakalotokea kwa kutumia majini, hii ni kazi ya wanajimu ambao ni mawakala wa shetani.

Wapinga ramli MUNGU wa Mbinguni hawezi kukaa kwao.


Isaya 2:6 "Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni."


➡️Kupiga ramli ni kitendo cha kutabiri kwa kutumia majini au kubashiri mambo yaliyojificha kwa kudanganywa na majini au mashetani kwa Jina lingine.


◼️Hivyo Kanisani hatakiwi kuwepo mpiga ramli, kama Yuko aamue Kuokoka na aache Kupiga ramli maana maelekezo ya MUNGU ni kwamba katika Kanisa asiwepo Mtu mpiga ramli.


◼️Katika Kanisa Kanisa hatakiwi kuwepo Mtu anayesema kwamba ana nyota yake ambaye ameelekezwa na wanajimu kwani hao ni mawakala wa shetani.

Nyota zote za wanajimu ni ushetani unaotokana na Kupiga ramli, ni Maelekezo ya majini au mashetani na sio maelekezo ya MUNGU wa Mbinguni.


3. Mwenye kubashiri.


1 Samweli 28:7-8 " Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.

 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako."


➡️ mbashiri  ni mganga wa kienyeji anayeagua.

Katika andiko hapa juu  tunaona Sauli akienda kwa mbashiri yaani akienda  Kwa mganga wa kienyeji anayeagua, kilichofuata kwa Sauli ni Unabii wa kifo chake.


1 Samweli 31:6 "Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo."


➡️Ndugu zangu, hatakiwi kuwepo mganga wa kienyeji Kanisani, wapo watu kabla ya Kuokoka walikuwa waganga wa kienyeji ila walipookoka waliacha uganga na Sasa wanamtumikia Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Ila kwa Mtu ambaye Sasa anajiita Mkristo na Kanisani anaenda ila pia yeye ni mganga wa kienyeji ni makosa makubwa sana, Biblia Iko wazi sana kwamba katika Kanisa hai hatakiwi kuwepo mganga wa kienyeji.


Zekaria 10:2 "Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji."


4. Msihiri.


Kumbu18:10 "Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,"


➡️Msihiri ni Mtu gani?

Msihiri Huyu ni anayefanya ushirikina ili kudhuru watu.


◼️Mtu wa namna hii Hatakiwi kuwepo katika Kanisa la KRISTO YESU.


Kama Wewe ni Msihiri na uko Kanisani Acha ushirikina wako, amua Kuokoka upya ili uwe Sasa Kanisa hai la MUNGU wa Mbinguni.


5. Mtu alogaye.


Mambo ya Walawi 20:27 Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.


➡️Mtu alogaye  ni mchawi.

Mchawi hatakiwi kuwepo Kanisani.

Najua Kuna watu walikuwa Wachawi zamani ila walipookoka waliacha uchawi, ila kwa Mtu ambaye Leo anajiita Mkristo lakini ni Mchawi Neno la MUNGU linasema hatakiwi kuwepo mchawi katika Kanisa hivyo aache uchawi wake haraka kabla hajachelewa na kukutana na adhabu ya MUNGU.


6. Apandishaye pepo.


2 Wafalme 17:17-20 " Wakawapitisha watoto wao, waume na wake, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza nafsi zao wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha. Kwa hiyo BWANA akawaghadhibikia Israeli sana, akawahamisha mbali na uso wake; wala hapana aliyesalia ila kabila ya Yuda peke yake. Hata na watu wa Yuda hawakuyashika maagizo ya BWANA, Mungu wao, lakini walikwenda katika amri za Israeli walizokuwa wamezifanya wenyewe. Basi BWANA akakikataa kizazi chote cha Israeli, akawatesa, na kuwatia katika mikono ya watu wenye kuwateka nyara, hata alipokwisha kuwatupa, watoke machoni pake."


➡️Apandishaye Pepo Huyu ni mlozi.


 ➡️Mtu Huyu sio Mtu mwenye mapepo ya kawaida ambayo tunaona huombewa Makanisani mapepo hayo yanatoka,  Huyu anayezungumzwa hapa  ni mganga wa kienyeji ambaye anapandisha mapepo mwenyewe ili aende kwa shetani n.k  yaani anahusika na faraki.

Anapandisha mashetani na kuanza kufanya uganga kwa maelekezo ya mashetani au majini ndani yake, Mtu wa namna hiyo hatakiwi kuwepo katika Kanisa la MUNGU wa Mbinguni.

Ni machukizo kwa MUNGU.


Isaya 47:9 "lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kitimilifu, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno."


7. Mtu awaombaye wafu .


➡️Huyu ni mwenye kutaka kauli kwa mizimu ,mapepo au wafu.


Kumbu 18:11-12 " wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako."


Kuomba wafu ni dhambi hivyo watu wa kweli wa MUNGU katika KRISTO YESU hawatakiwi kamwe kuomba wafu.


  Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments