BABA YANGU MCHUNGAJI.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki zangu wote.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU Kwa njia hii.


◼️Lengo la Ujumbe ni ili Watumishi wa MUNGU watakaoupata Kwa njia yeyote waufanyie kazi kwa faida ya Mwili wa KRISTO.


➡️Hapa Nazungumzia Wachungaji ambao MUNGU amewapa Neema ya kumtumikia kwa uaminifu miaka mingi na Sasa ni wazee sana, Hawa wanastahili heshima sana kutoka kwa watu wote.


1 Timotheo 5:17 "Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha."


✔️Baba yangu Mchungaji.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana sana kwa Utumishi wako mkubwa kwa KRISTO ulioufanya kwa miaka mingi.


✔️Imani ya Wokovu wa KRISTO umeilinda na mwendo uko tayari kumaliza.


✔️Umemtumikia Bwana YESU KRISTO Kwa uaminifu sana kwa miaka mingi, hongera sana sana, hata Mimi natamani nifikie hatua ya kumtumikia Bwana YESU KRISTO miaka 40 au 50 au 60 au 70 kama Wewe Mtumishi wa MUNGU ulivyotumika miaka mingi.


✔️✔️Unastahili heshima kubwa sana.


➡️Baba ninalo Neno Moja tu kwako, nisamehe sana kama nitakukwaza.


Kwa Nini nalisema Neno hili?


➡️Ni kwa sababu hadi Wewe Kuna wakati huwa unasema "Sisi tumezeeka, tuna miaka michache ya kutumika na kuishi, nyie Vijana ongezeni juhudi kumtumikia Bwana YESU KRISTO maana mna muda mrefu sana wa kutumika"


➡️Baba yangu kama hadi Wewe mwenyewe umegundua una muda mchache, Je kama Musa umeshamwandaa Joshua kuchukua nafasi Yako ukiondoka?


◼️Ni vizuri kufanya kama alivyofanya Musa kwa Ufunuo wa MUNGU alipokuwa mzee sana


Hesabu 27:18-23 " BWANA akamwambia Musa, MTWAE YOSHUA, mwana wa Nuni, MTU MWENYE ROHO NDANI YAKE, UKAMWEKEE MKONO WAKO; kisha UKAMWEKE MBELE YA Eleazari kuhani, NA MBELE YA MKUTANO WOTE; ukampe mausia mbele ya macho yao. Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii. Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia. Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa."


➡️Je Wewe kama Eliya umeshamwandaa Elisha kuchukua nafasi Yako ili kazi ya Injili ya KRISTO katika Kanisa iendelee?


1 Wafalme 19:15-16 " BWANA akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu. Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na ELISHA mwana wa Shafati wa Abel-Mehola MTIE MAFUTA AWE NABII MAHALI PAKO."


➡️Eliya alipojulishwa na MUNGU kwamba muda wa kuondoka Duniani umekaribia alianza process za kumwandaa Mtu atakayechukua nafasi yake ambaye ni Elisha.

Elisha alikuwa busy na kilimo lakini MUNGU alitaka huyo huyo achukue nafasi ya Elisha katika utumishi.


1 Wafalme 19:19 "Basi, akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima, mwenye jozi za ng'ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa vazi lake juu yake."


◼️Hata wewe Mtumishi wa Bwana YESU KRISTO Leo katika uzee wako Usikubali huduma ife baada ya Wewe kuondoka, Bali andaa Mtu sahihi wa kuchukua nafasi Yako.


➡️Utajisikiaje Mfano ungepata nafasi ya kujua kwamba ulikusanya maelfu ya watu kwa YESU na wakabaki na YESU Kwa usahihi wakati Wewe ukiwepo lakini ulipoondoka tu wale watu wakatawanyika na kumwacha YESU maana hukuweka watu wa kuchukua nafasi Yako?

Nina hakika utajisikia vibaya sana, hivyo wakati huu Sasa Ukiwa na Nafasi Anza kuandaa Mtu wa kuchukua nafasi, Anza kumpa na Nafasi za Utumishi, mtambulishe mbele ya Kanisa na waase watu wamsikilize maana MUNGU amemchagua kwa ajili yao.

Eliya alitimiza wajibu wake kwa MUNGU Kwa kumwandaa Elisha ambaye alikuja kuchukua nafasi yake na kufanya mambo makubwa sana hata kuliko Eliya mwenyewe.


2 Wafalme 2:9 "Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu."


➡️Wewe kama Daudi umeshamwandaa Suleiman kuchukua uongozi katika Kanisa?


1 Wafalme 1:33-35 " Naye mfalme akawaambia, Twaeni pamoja nanyi watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu wangu mimi mkamtelemshe mpaka Gihoni; kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie mafuta huko, awe mfalme juu ya Israeli; kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Sulemani na aishi! Kisha pandeni juu nyuma yake, naye atakuja ili aketi katika kiti changu cha enzi; kwa maana atakuwa mfalme badala yangu; ndiye niliyemweka awamiliki Israeli na Yuda."


◼️Hata wewe katika Kanisa Leo unayo nafasi ya kuandaa Viongozi wa Kanisa watakaochukua nafasi  hata wakati Wewe haupo.

Ubarikiwe sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292

Amen.

Comments