KUNA WATU UKIWABARIKI NDIPO UTABARIKIWA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.


◼️Kuna watu ukiwabariki unabarikiwa.


◼️Kuna watu MUNGU amewapa baraka za watu wengine ndani yao, hivyo ukiwabariki hao ndipo utabarikiwa.


Mfano hai ni huu


Mwanzo 12:3 "nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa."


➡️‘’akubarikiye nitambariki’’ kumbe mtu aanze kumbariki kwanza huyo aliyebeba baraka ndio na yeye atabarikiwa.


Mfano Mwingine ni huu.


Hesabu 24:9" Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye."


➡️Elewe Neno "Abarikiwe akubarikiye" yaani maana yake Mtu akikubariki naye anabarikiwa.


➡️Najua kuna vyanzo vingi vya baraka za MUNGU kwa Mtu na chanzo kimojawapo cha Baraka ni kuwagundua Watu waliobeba Baraka kisha ukawabariki ndipo na wewe  milango ya baraka itafunguliwa. 


◼️Watu hao ambao ukiwabariki utabarikiwa, wala sio wengi sana 

watu ambao ukiwabariki unaweza kubarikiwa, wanaweza kuwa ni matajiri’’ kama Ibrahimu lakini wanaweza kuwa ni maskini sana ila wamebeba baraka yako.


Kumbu 15:9 "Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako. Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako."


✔️Biblia inasema mpatie Mtu huyo bila kusitasita ndipo MUNGU atakubariki.


◼️Na Kundi kubwa zaidi la watu ambao ukiwabariki utabarikiwa ni Watumishi waaminifu wa Bwana YESU KRISTO wanaomtumikia kwa uaminifu.


➡️Mambo ya rohoni ni tofauti na mambo ya mwilini yaani Mtu ni maskini na hajabarikiwa lakini wewe ukijaribu tu kumbariki Mtu huyo unabarikiwa.


◾Mfano  kuna Mtu mmoja alifanya jambo zuri sana katika ujenzi wa Kanisa kijijini, Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye ni maskini sana wa mali akambariki kwa maombi miezi michache baadae alifanikiwa sana maana baraka ziliambatana naye tangu siku ile alipobarikiwa na Mchungaji.


◼️Kuna Watu wamebeba utajiri wako hata kama wao ni maskini kwa sasa.

Biblia inasema hivyo katika andiko hili.


 2 Wakorintho 6:10 "kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.''


✔️Kuna kundi dogo la Watu MUNGU amewaamuru wabebe baraka kwa ajili ya wengine, mfano mojawapo ni Waisraeli ukiwabariki unabarikiwa.


Mwanzo 22:18 "na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu."


◼️Yaani kuna baraka za watu wa mataifa yote duniani,baraka hizo zipo kwa Waisraeli kwa njia ya kuwabariki tu, usipowabariki  baraka inayopita njia hiyo hutaipata kamwe.


Mwanzo 26:4 "Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia."


◼️Kuna watu ukiwabariki kisha   na wao wakakubariki  hata wakiondoka duniani baraka waliyo itamka juu Yako  inaweza kukufuatilia hadi itatimia.


Mwanzo 26:24 "BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni MUNGU wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu."


◼️Hata Yakobo alibarikiwa na Isaka baada ya yeye kumbariki kwanza Isaka kwa chakula kizuri.


Mwanzo 27:23 "Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki."


◼️Baraka ya isa6ka kwa Yakobo ilikuwa kama mhuri ambao hauwezi kufutika ndio maana ilitimia hata wakati Isaka hayupo Duniani.

 

Mwanzo 27:33" Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa."


✔️Ndio maana hata Yakobo alipoenda kuishi kwa Labani  walipo mbariki kwa kumkaribisha na wao walibarikiwa ajabu hadi wakataka wawe wanamlipa mshahara ili asiondoke.


Mwanzo 30:27 "Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako."


◼️ Ndugu kuna watu MUNGU ameweka utajiri wako ndani yao ,kazi yako Wewe ni kuwabariki tuu au kufanya jambo la Baraka kwao utakalofanya wakubariki na  wewe.


Mwanzo 28:14 "Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa."


➡️Ndugu kuna watu MUNGU katika KRISTO YESU ameweka utajiri wako ndani yao kazi yako  wewe ni kuwabariki tu au kufanya jambo la Baraka kwao litakalowafanya wakubariki na Wewe.


➡️Inawezekana hata wao hawajui kama wamebeba baraka zako ili ukiwabariki tu na wao watakubariki hivyo utabarikiwa sana.


✔️Mfano hai ni Potifa mpagani lakini alipombariki Yusufu kwa kumkaribisha katika Nyumba yake alimbarikiwa kwa sababu ya Yusufu.


Mwanzo 39:5 "Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa BWANA ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba."


➡️Ndugu kuna watu wana baraka Wewe  wabariki tu ili wakubariki.


Hesabu 22:6 ''Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu, kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa."


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments