![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
➡️Ujumbe wa Leo ni wa tofauti kidogo ila umebeba ushindi wa ajabu kwako.
◼️MUNGU aliyeweka makerubi katika bustani ya Edeni ili kuilinda aweke makerubi kukulinda, kulinda familia Yako, kulinda Ndoa Yako uliye na Ndoa, kulinda Watoto wako uliye na Watoto na kulinda kazi Yako.
Mwanzo 3:24 "Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima."
◼️MUNGU aliyeweka makerubi katika bustani ya Edeni ili kuilinda aweke Malaika kulinda mwili wako dhidi ya mawakala wa shetani na dhidi ya Nguvu zozote za giza za kutumwa ili kuleta madhara kwako.
◼️Ndugu, katika KRISTO YESU MUNGU anaweza kukulinda Kila uendako.
➡️Mfano hai alimlinda Yakobo Kila anendako.
Mwanzo 28:15 "Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia."
◼️MUNGU aliyemlinda Yakobo Kila aendako akulinde Kila uendako, akulinde usiku na Mchana, akulinde Ukiwa safarini au Ukiwa nyumbani.
◼️MUNGU wa Mbinguni ailinde familia Yako na alinde uzao wako na afya Yako.
◼️MUNGU wa Mbinguni akubariki na kukulinda Ukiwa ndani ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.
Hesabu 6:24-26 " BWANA akubarikie, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani."
◼️MUNGU wa Mbinguni akulinde dhidi ya mabaya yote yaliyokusudiwa kwako mwaka huu na mwaka ujao wote.
Zaburi 121:7 "BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako."
◼️Ndugu, Hakikisha umeokoka na YESU KRISTO ni Mwokozi wako Kisha omba MUNGU wa Mbinguni akulinde atakulinda.
Isaya 42:6-8 " Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa. Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu."
Ndugu, omba kulingana na Ufunuo wa Leo na MUNGU wa Mbinguni atakutendea sawasawa na Maombi Yako katika Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments