MAMBO 10 YA KUOMBA MUNGU AKUJALIE KUPATA.

 

Na Mtumishi Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 

Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.

Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.


◼️Kuna mambo yatafanyika tu kama MUNGU akikujaalia.


Waebrania 6:3 "Na hayo tutafanya MUNGU akitujalia."


◾Kujalia au wengine husema kujaalia ni nini?


 ➡️Kujalia ni kufanya jambo liwezekane ambalo kwa njia za kawaida lilishindikana.


➡️Kujalia ni kufanya kitu kiwezekane hata kama mazingira yanakataa kwa wakati huo.


◼️ MUNGU kukujalia ina maana atakuwezesha kupata jambo au kitu hata kama akili ya kibinadamu ilifika mwisho.


➡️Mfano ni hapa ambapo MUNGU aliwajaalia Waisraeli kuwa hodari kuliko adui zao.


Zaburi 105:24 "Akawajalia watu wake wazae sana, Akawafanya kuwa hodari kuliko watesi wao."


◼️ MUNGU ni MUNGU wa yale yasiyowezekana kwa wanadamu, 

MUNGU anaweza kutenda jambo ambalo katika njia za kawaida lilishindikana.


◼️Ndugu, Kuna mambo ili yafanyike ni MUNGU tu katika KRISTO YESU Akujalie ndipo yatawezekana.

 Mfano hai ni kuonana na watu fulani baada ya muda mrefu, ni MUNGU tu kujaalia maana hakuna anayeweza kuishi kesho kama sio MUNGU kumlinda.


Matendo  18:21 "bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, MUNGU akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,"


◼️Anaitwa MUNGU wa yale yaliyoshindikana.


Yeremia 32:27 "Tazama, mimi ni BWANA, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?"


➡️Sasa MUNGU kukujalia ni kukupa kitu ambacho bila yeye usingekipata, ni kupitia Maombi yako katika Jina la YESU KRISTO tu unajibiwa.

Wapo watu walioomba na MUNGU wa Mbinguni akawajaalia kupokea.

Mfano hai ni Yabesi.


1  Nyakati 4:10 "Huyo Yabesi akamlingana MUNGU wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye MUNGU akamjalia hayo aliyoyaomba."


◼️ MUNGU kukujalia maana yake Bwana YESU  kukutendea jambo ambalo hakuna mtu duniani angeweza kukutendea.


➡️Mfano hai ni kipofu tangu kuzaliwa alijaliwa kupona ndani ya sekunde chache tuu.


Marko 10:51-52 " YESU akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. YESU akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani."


◾Maombi 10 ya kuomba kwa MUNGU akujalie.


1. Omba MUNGU akujalie Neema ya KRISTO iliyozidi ili uendelee vizuri kiroho,kiuchumi,kiafya,kihuduma ya Injili n.k


Yakobo 4:6 "Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, MUNGU huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu."


2. Omba MUNGU akujalie kupata kibali kwa watu.


Danieli 1:9 "Basi MUNGU alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi."


3. Omba MUNGU akujalie kukaa salama.


Zaburi 4:8 "Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, BWANA, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama."


4. Omba ROHO MTAKATIFU akujalie kunena kwa lugha katika yeye.


Matendo  2:4 "Wote wakajazwa ROHO MTAKATIFU, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama ROHO alivyowajalia kutamka."


5. Omba MUNGU akujalie kuokoka/kupona mbele ya adui zako wenye nguvu.


Luka 1:74 "Ya kwamba atatujalia sisi, Tuokoke mikononi mwa adui zetu, Na kumwabudu pasipo hofu,"


6. Omba Bwana YESU KRISTO akujalie kuwaona adui zako ili uwashinde.


Zaburi 59:10 "MUNGU wa fadhili zangu atanitangulia, MUNGU atanijalia kuwatazama adui zangu."


7. Omba MUNGU awajalie kutubu na kuokoka  watu wanaokuhusu unaotamani wasiende jehanamu kwasababu unajua hawana Wokovu wa Bwana YESU KRISTO.


Matendo  11:18 " Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza MUNGU, wakisema, Basi, MUNGU amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima."


8. Omba MUNGU akujalie kupendelewa na watu.


 Kutoka 12:36 "BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara."


9. Mwanamke uliye kwenye Ndoa omba MUNGU akujalie kubeba mimba na kuzaa Watoto.


Ruthu 4:13 "Basi Boazi akamtwaa Ruthuu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume."


➡️Kama ni Mwanaume omba MUNGU akujalie kupata Watoto kwa Mke wako wa Ndoa, pia muombee Mke wako MUNGU amjalie kubeba mimba na kuzaa.


Mwanzo 17:16 "Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake."


10. Wewe Mtumishi wa MUNGU uliyeokolewa na Bwana YESU omba MUNGU akujalie ishara na maajabu yake kupitia mikono yako wakati ukimtumikia Bwana YESU KRISTO.


Matendo  14:3 *Basi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa ushujaa katika BWANA, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao."


Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.

MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.

By Mwl Peter Mabula 

Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)

Ubarikiwe.

Comments