![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
◾Kuna mambo mengi Biblia imesema yatatokea baadae katika safari ya Maisha ya mwanadamu Duniani.
◼️Baadhi ya yatakayotokea ni ishara kwa Kanisa kwamba ni siku za mwisho na YESU KRISTO Mwokozi wetu yu Karibu kurudi.
Marko 13:29-30 " nanyi kadhalika, myaonapo mambo hayo yanaanza, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatimie."
◼️Na mengine yatatokea sio ishara ya siku za mwisho ila yatatokea kwasababu MUNGU alisema yatatokea.
➡️Najua yapo mengi mno ya kutokea katika safari ya Mwanadamu nimekuchagulia machache ili tupate kitu cha kujifunza kama Kanisa hai la KRISTO YESU Duniani katika majira yetu haya tunayoishi.
Mambo yatakayotokea baadae katika safari ya Maisha ya Wanadamu Duniani.
1. Kutokea Siku ya Hukumu, Wenye dhambi kuhukumiwa na MUNGU.
Malaki 4:1 "Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi."
◼️Katika safari ya Maisha ya mwanadamu wote ni muhumu kujua kwamba kuna siku ya mwisho ambayo kwa jina linguine ni siku ya hukumu.
Isaya 13:9 "Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake."
◼️Siku hii ya hukumu itakuja na itawahusu Duniani nzima na atakaye hukumu wanadamu wote waliowahi kuishi duniani ni Bwana YESU KRISTO, walio na YESU KRISTO Watakatifu wataingia uzima wa Milele na Wanadamu wengine wote wa dini zote wasio na Wokovu wa Bwana YESU KRISTO wataenda jehanamu.
Mathayo 24:30-31 " ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu."
➡️Hii imfundishe kila Mtu Duniani kwamba asipookolewa na YESU KRISTO sasa akiwa hai atahukumiwa Kwenda jehanamu.
◼️Ndugu hakikisha umeokoka na unaishi Maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO YESU.
➡️◼️Tukio hili liko mbele ya Kila Mwanadamu anayeishi Sasa Duniani na tukio hili pia liko mbele ya Kila Mwanadamu ambaye amewahi kuishi Duniani ila akafariki.
Ambaye amewahi kuishi hana ila hakuwa na YESU huyo hana nafasi ya kutubu na kutengeneza na MUNGU katika KRISTO YESU.
Ila Wewe unayeishi na Wewe unayesoma ujumbe huu unayo nafasi ya kutubu, Kuokoka na kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU ili usiende jehanamu.
Amua Leo kumpokea YESU KRISTO awe Mwokozi wako Kisha Anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wake.
2. Kutokea kwa Njaa ya kusikia Neno halisi la MUNGU.
Amosi 8:11 "Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA."
➡️Sio kwamba yanayoitwa maneno ya Mungu hayatakuwepo, hayo yatakuwepo tena mengi ya Dini mbalimbali ila Neno la MUNGU aliye hai kwa ajili ya Uzima wa Milele wafundishaji wengi watakuwa hawana Neno hilo.
➡️Injili ya KRISTO YESU iokoayo itapunguzwa masikioni mwa wanadamu labda kwasababu watu wengi hawaitaki hiyo .
➡️Mafundisho ya wapinga KRISTO yatakuwa mengi.
1 Timotheo 4:1 "Basi ROHO anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;"
◼️Wewe unayelisikia fundisho la YESU aokoaye lizingatie sana fundisho hilo maana itafika wakati fundisho kama hilo litakuwa adimu, maana watu watakuwa na mafundisho yao ya uongo.
◼️Hata leo ukimsikia Mtumishi anakwambia uokoke zingatia sana hayo maana inawezekana Watumishi kama hao sio wengi sana.
➡️Wakati huo utakuja kama Neno la MUNGU linavyosema, na Inawezekana kwa baadhi ya Maeneo wakati huo umeshaanza.
3. Wapinga KRISTO wengi wenye dhihaka dhidi ya kweli ya Injili ya KRISTO watakuwa wengi.
2 Petro 3:3 "Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,"
➡️Kuna wakati unatamani asiwepo hata mtu mmoja anayepinga Wokovu wa KRISTO lakini wapo kwasababu taarifa za ujio wao zilitabiriwa.
Yuda 1:18 "ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe za upotevu."
◼️Ndugu, Hakikisha sio Wewe unayedhihaki habari za Kuokoka.
4. Kutakuwa na nyakati za hatari .
2 Timotheo 3:1 "Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari."
➡️Kuna Nyakati za hatari zitatokea Duniani na zingine zimeshaanza kutokea tayari.
Baadhi ya nyakati za hatari zimeanza kutokea mfano corona walipata watu 183,000,000 na 4,000,000 katika yao walikufa kwa mujibu wa Umeona wa Mataifa(UN) tarehe 8 july 2021.
➡️Mambo ambayo yatatokea Duniani katika kuishi kwa Wanadamu mojawapo ni kutokea kwa Nyakati za hatari.
Marko 13:14-23 " Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. Lakini ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku hizo! Ila ombeni yasitokee hayo wakati wa baridi. Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba MUNGU hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Na kama BWANA asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo. Na wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, KRISTO yupo hapa, au yuko kule, msisadiki; kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule. Bali ninyi jihadharini; nimekwisha kuwaonya yote mbele."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments