MAMBO YANAYOAMBATANA NA KUMSHUKURU MUNGU.

 

Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.

◼️Ni vizuri sana kumshukuru MUNGU wa Mbinguni.

1 Wakorintho 15:57 "Lakini MUNGU na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu YESU KRISTO."

◾Kumshukuru MUNGU ni Nini?

◼️Kumshukuru MUNGU ni kusema maneno yanayoonyesha  kuridhika na wema uliofanyiwa na MUNGU.

2 Wakorintho 2:14 "Ila MUNGU ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika KRISTO, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu."

◼️Kumshukuru MUNGU ni kuonyesha ishara inayo tafsiri kulidhika na kile MUNGU amekufanyia.

Zaburi 140:13 "Hakika wenye haki watalishukuru jina lako, Wenye adili watakaa mahali ulipo Wewe."

◼️Kushukuru MUNGU ni kufanya mambo yanayoonyesha  unamfurahia MUNGU kwa anayo kutendea au aliokutendea kwenye Maisha yako.

Zaburi 92:1 "Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu."

◼️Kumshuru MUNGU Katika KRISTO YESU ni jambo zuri sana na la muhimu sana kwa kila mtu aliyetendewa na MUNGU.

Wafilipi 4:6 "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na MUNGU."

➡️Kumshukuru inatakiwa kuwa automatic ndani ya moyo wa mkristo yaani kumshukuru MUNGU huja moja kwa moja moyoni bila hata kuambiwa na mtu.

1 Wathesalonike 5:18 "shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya MUNGU kwenu katika KRISTO YESU."

◼️Kumbuka wema wa MUNGU haukomi.

◾Kuna mambo huambatana na watu wanaomshukuru MUNGU katika KRISTO YESU kwa yale aliyowatendea, baadhi ni haya.

1. Kumshukuru MUNGU huambatana na Kuwajulisha watu alichokofanya MUNGU.

1  Nyakati 16:8" Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake."

Kumshuru MUNGU kuliko kuzuri Zaidi sio kimya kimya bali kusema alichokofanya MUNGU.

Mfano hai ni huu

Luka 2:38 "Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru MUNGU, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake."

2. Kumshukuru MUNGU huambatana na Kinywa chako kujaa jina la MUNGU Wakati wa kumshukuru MUNGU.

2 Samweli 22:50 "Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako."

Kuliimba Jina la MUNGU maana kulitaja Jina la YESU KRISTO kutokana na alichokutendea.

➡️Wengi hujaza vinywa vyao majina ya Watumishi, madhehebu na sio Jina YESU anayetenda hayo ni makosa jaza, Ndugu jaza jina la YESU KRISTO kinywani Mwako ambae ndiye amekutendea.

1  Nyakati 29:13 "Basi sasa, MUNGU wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu."

3. Kumshukuru MUNGU huambatana na Kutoa ushuhuda kwa watu alichokifanya   MUNGU kwako.

Zaburi 9:1 "Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;"

 ◼️Hii ni kuwaambia watu kwa uwazi nini  MUNGU katika KRISTO YESU amefanya kwako.

4. Kumshukuru MUNGU huambatana na Maombi ya  shukrani 

Filemoni 1:4 "Namshukuru MUNGU wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu;"

➡️Maombi haya huja bila kupanga ndani ya moyo wa mtu.

1  Nyakati 23:30 "nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA, na jioni vivyo hivyo;"

5. Kumshukuru MUNGU huambatana na wimbo wa shukrani moyoni.

Ezra 3:11 "Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa."

➡️wimbo huu huja automatic ndani ya moyo wa mtu mwenye moyo wa shukrani, unaweza kuwa ni wimbo anaoujua kutoka katika nyimbo za Watumishi wa Bwana YESU au hata wimbo mpya ambo ROHO MTAKATIFU anauweka ndani yake wakati huo.

Zaburi 28:7 "BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru."

➡️Unaweza kuwa ni wimbo wa taratibu au wimbo wa sifa.

Zaburi 109:30 "Nitamshukuru BWANA kwa kinywa changu, Naam, nitamsifu katikati ya mkutano."

6. Kumshukuru MUNGU huambatana na Sadaka ya shukrani.

Zaburi 50:23 Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU.

➡️Mtu mwenye moyo wa shukrani kwa MUNGU hujiona kama hayuko sawa asipotoa sadaka ya shukrani baada ya MUNGU kumtendea.

Zaburi 107:22 "Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba."

7. Kumshukuru MUNGU huambatana na  nia ya mtu kutaka kuwa Mtakatifu.

Wakolosai 1:12 "mkimshukuru BABA, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru."

 ➡️kuna wengine hadi hulia kwa furaha wakimshukuru Bwana YESU na wakati huo nia zao zikiimarika kwenye utakatifu ili wasimkosee tena MUNGU aliyewapa Neema ya ushindi.

Warumi 6:17 "Lakini MUNGU na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;"

◼️ Ndugu penda kumshukuru MUNGU kwa aliyokutendea.

1 Timotheo 1:12 "Nami namshukuru KRISTO YESU Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;"

➡️Nina mengi ya kumshukuru MUNGU, una mengi ya kumshukuru MUNGU .

Zaburi 139:14 "Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,"
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe. 

Comments