
Na Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
➡️Siku Moja wakati naandaa Neno la MUNGU ghafla nikapewa rohoni somo hili hivyo nilivyomaliza kuandaa somo la kwanza nikaandaa na hili.
➡️Ni kwamba Kanisa ambalo Mchungaji au Viongozi wa Kanisa wamekataza habari za kunena kwa lugha kwa waumini wa Kanisa hilo, hao Viongozi wa Kanisa hawajitambui.
◼️Kwanza Kunena kwa lugha ni kuzungumza na MUNGU.
1 Wakorintho 14:2 "Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na MUNGU; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake."
➡️Kama kunena kwa lugha ni kuzungumza na MUNGU, Je Wewe Kiongozi wa dhehebu unayekataza watu kuzungumza na MUNGU, Wewe unamtumikia MUNGU yupi?
➡️Hapa Nazungumzia Kuna madhehebu Viongozi wao wamekataza waumini wao habari ya kunena kwa lugha, hayo ni makosa sana.
Kuna Wachungaji wamekataza washirika kunena kwa lugha iwe nyumbani, kwenye Maombi au ibadani, hilo ni kosa kubwa sana la Viongozi wa Kanisa
◾ Kwanini nasema haya?
◼️Kama ni Watumishi wa kweli wa MUNGU lazima wamfuate Bwana YESU KRISTO, lakini Bwana YESU ndio aliagiza Kanisa lake wawe wananena kwa lugha
Marko 16:17 "Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;"
➡️Hivyo Watumishi hao hawamfuati Bwana YESU, na Je kama hawamfuati Bwana YESU ndio watakuwa wanamfuata nani?
◼️Kama humfuati YESU ni hatari sana maana nje na Yeye unafuata mipango ya shetani.
◾ Kwanini nasema haya?
➡️Viongozi hao wa kiroho husema wanamfuata Mtume Paulo kama Biblia inavyosema.
1 Wakorintho 11:1 "Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata KRISTO."
◼️Lakini Mtume Paulo yeye anasema ananena kwa lugha sana.
1 Wakorintho 14:18 "Namshukuru MUNGU ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;"
➡️Hivyo Viongozi hao wa Kiroho hawamfuati Paulo.
➡️Baadhi ya Viongozi wa Kanisa hutumia andiko hili kukataza watu kunena kwa lugha kwamba kama hakuna Mtu anayetafasiri Mtu asinene.
1 Wakorintho 14:28 "Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na MUNGU."
➡️Paulo hapa alikuwa anatoa utaratibu wa kunena kwa lugha Kanisani wakati Ibada ikiendelea na vipindi vingine Ibadani vikiendelea.
Hakumaanisha kwamba ni marufuku kunena kwa lugha kama hakuna kufasiri, ndio maana Paulo anasema ananena sana kwa lugha.
1 Wakorintho 14:18 "Namshukuru MUNGU ya kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote;"
◼️Paulo anasema ananena sana kwa lugha akiwa peke yake nyumbani, Je huko Kuna Mtu alikuwa anafasiri?
Jibu ni hapana hivyo utaratibu wa Ibadani hatutakiwi kuwa zuio la dhehebu kuacha kunena kwa lugha.
◼️ Waliohubiri Injili mwanzo hata ikaenea Duniani hakuna Mtu mmoja miongoni mwao ambaye hakuwa ananena kwa lugha.
➡️Mfano hai katika andiko hili Mitume wote akiwemo Petro na Yohana na wengine wote walinena kwa lugha.
Matendo 2:4 "Wote wakajazwa ROHO MTAKATIFU, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama ROHO alivyowajalia kutamka."
➡️Je Wewe unayekataza watu kunena kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU unatokea wapi Wewe?
➡️Je unamfuata nani Wewe?
Dada mmoja alikuwa anaabudu dhehebu Moja ambalo kwao ni marufuku kunena kwa lugha.
Dada huyu hata yeye alikuwa amefundishwa hakuna habari za kunena kwa lugha kwenye dhehebu lao.
Hata yeye kwa kufundishwa muda mrefu kwamba marufuku kunena kwa lugha hadi alichukia kunena kwa lugha na aliwachukia Wanaonena kwa lugha katika Makanisa yao.
Siku Moja akiwa katika Maombi Kanisani kwao, baada ya Maombi ya kutubu, akiweka umakini kwa MUNGU moyoni mwake huku akiomba ghafla alijawa Nguvu za ROHO MTAKATIFU akaanza kunena kwa lugha.
Jambo hilo lilileta kikao Cha Viongozi wa Kanisa, Dada yule akawa ananyanyasika Kanisani hadi akaniomba Ushauri.
Nikamwambia kama amepata Neema ya kunena kwa lugha basi amepata Moja ya Miujiza mikubwa zaidi hivyo aanze kujifunza kuhusu ROHO MTAKATIFU na kazi zake na Kwa sababu wanamnyanyasa Kanisani hapo kwa ajili ya kipawa Cha MUNGU basi ahame, aende Kanisa safi la Kiroho wanaomhubiri YESU KRISTO na kukemea dhambi akajiunge huko, akafanya hivyo.
➡️Najua Kuna baadhi ya Wachungaji hawaneni kwa lugha Kabisa, hilo Wala sio tatizo ila Kwa sababu wao hawaneni kwa lugha wamekataza na washirika wao kunena kwa lugha ili isije kuonekana Wachungaji sio wa Kiroho hilo ndio tatizo baya sana. kumbe kunena kwa lugha wakati Mwingine ni kipawa Cha ROHO MTAKATIFU hivyo sio Kila Mtu anacho.
1 Wakorintho 12:8-10 " Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;"
◼️Kipawa hicho Cha kunena kwa lugha anaweza kuwa nacho mshirika huku Mchungaji hana.
Waefeso 4:7 "Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake KRISTO."
◼️Hivyo usiwakataze watu kunena kwa lugha kwa sababu tu Wewe hukupewa kipawa hicho Cha kunena kwa lugha.
➡️Swali ni Moja, Viongozi wa dhehebu au Kanisa wanaokataza Watu kunena kwa lugha wanakuwa wanamfuata nani?
◼️Maana KRISTO anataka watu wanene kwa lugha kama andiko hapo juu lilivyosema
◼️ Mitume wanataka Wateule wa MUNGU wanene kwa lugha
1 Wakorintho 14:39-40 " Kwa ajili ya hayo, ndugu, takeni sana kuhutubu, wala msizuie kunena kwa lugha. Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu."
◼️ Biblia inatoa utaratibu Ibadani wa kunena kwa lugha ili mambo yote yafanyike kwa Uzuri na utaratibu ila haikatazi kabisa watu kunena kwa lugha majumbani au kwenye Maombi binafsi ya Mtu.
➡️Mfano Mtu aliyekuja Kuokoka siku hiyo au ni mshirika mpya anahitaji zaidi kufundishwa Neno la MUNGU kwanza ili ajengwe, hivyo katika Ibada kunena kwa lugha kwa watu wachache Kuna faida zaidi kama Kuna atakayepewa kutafasiri ili kuwajenga waumini wapya.
1 Wakorintho 14:22-23 " Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio. Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?"
➡️Hivyo katika Kanisa ushauri wangu wakati wa kipindi Cha Maombi Kila anayepewa kunena kwa lugha anene, ila kuwe na wakati wa utulivu ambapo angalau Mtu mmoja anene na ikitokea Mtu Mwingine amepewa kutafasiri basi wengine wote tunyamaze tusikilize.
1 Wakorintho 14:30 "Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze."
◼️Lakini Ukiwa katika Maombi Yako uko peke yako ukipewa kunena kwa lugha Nena sana.
◼️Au uko nyumbani kwako ukipewa kunena kwa lugha Nena hata kama ni masaa mengi.
Kumbuka unaponena kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU unazungumza na MUNGU Moja kwa Moja.
◼️Ni vizuri sana kuzungumza na MUNGU wa Mbinguni Kwa njia ya kunena kwa lugha.
◼️ Hivyo dhehebu waliopiga marufuku kunena kwa lugha kwa washirika wao, hao Viongozi hawajamfuata MUNGU, hawajamfuata YESU KRISTO, hawajamfuata ROHO MTAKATIFU na Wala hawajamfuata Mtume yeyote wa YESU KRISTO katika Biblia.
◾Je hao watakuwa wamemfuata Nini?
Ukweli watakuwa wamemfuata shetani.
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.
Comments