MIMI NINATAKA KUOKOKA.

 

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda Kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 


Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU la wito wa Wokovu.

◼️Mwanadamu ukihitaji uzima wa Milele mpokee YESU KRISTO awe Bwana na Mwokozi wako.

Mathayo 19:29 "Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele."

 ◼️Haijalishi Ndugu zako hawataki au dini Yako haitaki ila kama unautaka kweli uzima wa Milele mpokee YESU KRISTO awe Mwokozi wako na Anza kuishi katika Wokovu wake.

➡️Ila kama huutaki uzima wa milele endelea na dini Yako iliyo kinyume na Wokovu wa Bwana YESU.

➡️Kama huutaki Uzima wa Milele watii  watu au wazazi wako au Ndugu zako au rafiki zako wanaokukataza kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.

◼️Maamuzi Yako kwako ndio maana nakusihi sana Hakikisha umeokoka na unaishi Maisha Matakatifu katika Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.

Yohana 3:14-18 " Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."

◼️Ndugu, amua kumpokea YESU KRISTO awe Mwokozi wako Leo.

➡️Kama  unapenda Kuokoka tamka kwa kinywa chako Sala hii ya toba hapa chini Kisha kesho jumapili nenda Kanisani ukamwambie Mchungaji kwamba umeamua Kuokoka.

Sala ya toba.

Ee MUNGU Baba wa Mbinguni.
Ninakuja mbele zako katika KRISTO YESU Mwokozi wangu.
Mimi ni mwenye Dhambi.
Ninaomba unisamehe dhambi zangu zote, zile dhambi ninazozikumbuka na zile dhambi nilizozisahau.
Baba wa Mbinguni ninaomba pia unisamehe maovu yangu yote na makosa yangu yote.
Bwana YESU ninaomba ulifute Jina langu kwenye Kitabu Cha Hukumu na ulifute pia Jina langu kwenye vitabu vya kuzimu vyote.
Na Sasa Bwana YESU KRISTO ninaomba uliandike Jina langu kwenye Kitabu chako Cha Uzima wa Milele.
Kuanzia Leo ninamkataa shetani na kazi zake zote.
Kuanzia Leo nakupokea Bwana YESU KRISTO uwe Mwokozi wangu Milele.
Kuanzia Leo ninatangaza nimeokoka na Bwana YESU KRISTO ndio Mwokozi wangu Milele.
Ninakushukuru MUNGU Baba kwa kunisamehe dhambi zangu zote, maovu yangu yote na makosa yangu yote.
Ninakushukuru Bwana YESU KRISTO Kwa kuniokoa na kuniandika jina langu kwenye Kitabu Cha Uzima Mbinguni.
Katika Jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea Wokovu.
Ameeeen.

Ubarikiwe sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la MUNGU Mwenyezi.
0714252292.
Amen.

Comments